Nakataa kabisa, hali sivyo kama inavyodaiwa

Nakataa kabisa, hali sivyo kama inavyodaiwa

Nami nipo mtaani humu humu. Nazunguka huku na kule. Naona kwa macho yangu mwenyewe. Siongelei mambo ambayo siyaoni au ambayo siwezi kuyaona.

Lakini ukiwasikiliza hawa wanaharakati wa mitandaoni unaweza kudhani huko nyuma tulikuwa nchi yenye uchumi wa nchi za dunia ya kwanza na sasa uchumi huo umebadilika kabisa kisa Rais Magufuli.

Halafu sasa, hawa wanaolalamika mitandaoni wanazitoa wapi hela za kununua bando na kuja kulalamika eti hali ni mbaya.

Kama hali ni mbaya si waache kununua bando na wanunue chakula wale.

Bando na chakula kipi cha muhimu?
Maisha yanaendelea, watu wanakula bata uswazi,watu wanakula bata ushuani. Biashara zinafungwa nyingine zinafunguliwa wapiga kelele wengi ni wafuata mkumbo Tu.
Mambo magumu inabidi ubadilike kulingana na mazingira badala ya kulialia mitandaoni.
#KazinaBata hamna wa kukuzuia kula bata....
 
Why should I go to he'll? I am responding to your stupid comments which you thought they were wise ones. Kuwa limbukeni katika maisha ni kitu kibaya sana. Nyani wewe ni limbukeni. Watu kama wewe ukiwaangalia background wametokea familia zenye umaskini wa kunuka, lakini mkipewa vifedha kidogo, niko tayari hata kuuza mama zenu, kisha mnajifanya kujua kila kitu. Kwa taarifa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. At the end you are the one who will go to he'll.

Sent from my HUAWEI GRA-L09 using JamiiForums mobile app

If you don’t want to go to hell then just kick rocks.
 
Sijui mtu ataniambia nini nimuelewe, achana na vigoma sijui harusi, kujenga imekua mtihani mgumu usio na huruma na kwa mwananchi. Vifaa vya ujenzi bei juu kuliko kawaida, kwa wanaojenga sasa nadhani wanajua chungu tamu wanayokutana nayo.
 
Neno, japo Wenye hekima na wazalendo wa kweli hawasubiri taifa likwame Kabisa, wapo makini na kuonya kila dalili mbaya kwa uchumi wetu,ustawi na umoja wa taifa letu.
Ki ukweli hali inazidi kuwa mbaya, uwezo watu kununua unazidi kupungua( purchasing power)
Bei bidhaa isipokuwa chakula zinapaa kila uchao mfano vifaa ujenzi,bidhaa za mafuta
" were in right truck" " no free lunch" tupambane
Hakika ndugu, vifaa vya ujenzi hali ni tete, ni pasua kichwa. Kama una pumzi fupi cha moto utakiona.
 
Huku mitandaoni sasa kumeshakuwa ni sehemu ya uhalisia mbadala [alternate reality].

Ukiishi huku utaambiwa na kuaminishwa kuwa huku uraiani sasa hivi hakukaliki. Utaaminishwa [na kama ukiwa mjinga, mvivu, na zuzu, utaishia kuamini kweli] hali ya maisha ni mbaya mno. Hayo utayoaminishwa yatakufanya ujenge taswira nyingi mno kichwani.

Unaweza ukapata taswira ya kwamba sasa hivi Watanzania wengi wanalala njaa. Watanzania hawana nguo za kuvaa. Maduka hayana bidhaa. Watu wanakula nyasi na panya kama ilivyokuwa huko Zimbabwe miaka kadhaa iliyopita. Watoto wa shule hawana kalamu wala daftari. Watu hawanywi pombe. Hawali kitimoto. Hawaogi. Hawana magari. Hawachepuki. Na mengineyo lukuki.

Lakini mtu ukiachana na hayo maneno ya kwenye mitandao na uingie mwenyewe uraiani ujionee na upate tajiriba ya uhalisia wa mambo, utaishia kuhitimisha kuwa huko kwenye mitandao kuna upotoshaji na utiaji chumvi mkubwa sana.

Tembea tu huku na kule jijini Dar, nenda mikoa mingine na wilaya zake, utaona maisha ya watu yanaenda tu kama ilivyo siku zote.

Mara umekutana na msafara wa harusi. Umekaa kwa Mangi unakunywa Konyagi yako ya kupimiwa mara ghafla unaona kigoma kinapita na watu, wake kwa waume, wakubwa kwa watoto, wanajiachia tu.

Sasa kama uko ni mtu wa tafakuri, utajiuliza, ‘mh...hivi hiyo hali mbaya inayozungumziwa huko kwenye mitandao ndo ipi hasa’?

Kwa hiyo, kusema ukweli mimi nakataa kabisa. Nabisha. Nasema hali si mbaya. Hali iko vile vile tu ambavyo imekuwa karibu siku zote, ukiondoa labda enzi zile ambapo watu tulikuwa tunaenda kupanga mstari kwenye maduka ya ugawaji kununua mikate ya Siha, sukari, sabuni za Mbuni na Mbunju, na mahitaji mengine.

Zaidi ya hapo, kelele kelele za huko mitandaoni hazina mashiko. Ni za watu wanaotapa tapa tu. Wafamaji.

Wakatabahu,

Alhaji N. Ngabu [emoji6].
Kama mambo ya mitandaoni siyo ww umefata nn?
 
Leo jiwe kajichanganya wala haeleweki, kasema hali ya uchumi ni nzuri sana,hali ya inflation ni nzuri, halafu ETI hali ya uokotaji kodi ni MBAYA SANA.
Hivi anajua uhusiano uliopo kati ya hali ya uchumi,inflation na kodi!???? Nimechoka kabisa aisee.uchumi ukue kodi hakuna????inflation ishuke uchumi ukue?baba tafadhali wafute kazi washauri walokuandalia hotuba, kama watoa kichwani basi nakusamehe maana ulishasema ni kichaa.
 
Nabisha!

Jumanne naenda mnadani pale Kidinda.

Najua watu watajaa mpaka pomoni.

Mbuzi watachinjwa, nyama zitachomwa na kuliwa papo hapo, na Balimi zitanyweka.

Kuhusu watu kuacha magari yao na kupanda daladala....

Watu huwa na sababu nyingi tu za kufanya hivyo:

Wengine kupanda daladala ni kufanya mazoezi.

Wengine hupanda daladala kwa sababu ya convenience.

Wengine hupanda daladala just for the hell of it.

Wengine hupanda daladala kwa sababu hawapendi kuendesha magari yao maana uendeshaji wa Dar, kwa mfano, unahitaji uwe na moyo mgumu kweli kweli.

Licha ya hayo, mbona foleni jijini Dar hazijapungua sasa kama watu wameacha kuendesha magari yao na kuamua kupanda daladala kwa sababu ya ugumu wa maisha?

Hela za nauli za kupandia daladala wanazitoa wapi?

Bado nabisha. Hali si mbaya kama tunavyoaminishwa.

Hali ingekuwa ni mbaya kihivyo basi hata wewe usingepata hela ya kununulia salio uje hapa JF na kutoa maoni yako kama ilivyo kwa wengine wanaotoa mawazo yao kwingineko huko mtandaoni.

Nabisha.
Chanzo cha Imani ni kusikia,kwakuwa umeshasikia kuwa hali ni mbaya mitaani,IPO siku utaamini wakati, ukimwi umeingia baadhi ya nchi zilitangaza kuwa ugonjwa huo ni janga la kitaifa. South Africa walikataa kuwa siyo janga kwao. Mpaka walipokubali kuwa ni janga,madhara yalishakuwa makubwa. Na hili MUDA UTASEMA
 
anaongea mbeba boksi aliyepo marekani,pathetic,M MESCREw up KISHENZI,MMEHARISHIA UCHUMI,CLEAN UP YOUR MESS harufu mbaya inatukera
 
Wala haikusaidii na kingereza chako cha kipumbavu njoo na lugha iliyo na mawaaa lugha ya kiswahili, tunaambiwa tusibishane na mpumbavu tukaja kuwa wapumbavu

Umeshindwa kuendelea kwa Kiingereza teh teh
 
Back
Top Bottom