Nakataa kabisa, hali sivyo kama inavyodaiwa

Jamani!

Watu wanakula bata kama kawa.

Watu wanajenga kama kawa.

Watu wananunua ndinga kama kawa.

Watu wanaanzisha miradi kama kawa.

Watu wanakula starehe sana sana usiku kucha nchi nzima.

Watu wanavaa vizuri.

Shauri yako.
 
TRUE..!!
¤maisha bado yko bomba! anaebisha itakuw hana ramani tu mwenyew..
 
Watu wakula bata kwa kwenda mbele kama huna hela basi pambana acha kulia lia kama mtoto
 
Juzi juzi nimeenda bar fulani kubwa siku ya katikati ya wiki nikakuta wahudumu tu ndio wamekaa kwenye viti wanapiga stori. Wakati huo huo nafahamu bar nyingine 2 kubwa na nightclub 1 zimefungwa hapa town.
 
Shabaan Robert alikuwa mwandishi mzuri sana wa riwaya za namna hiyo ukiacha hiyo kufikirika ipo nyingine inaitwa kusadikika. Tell him to enjoy
hahahahaha
mkuu sidhani kama anaelewa
 
Jamani!

Watu wanakula bata kama kawa.

Watu wanajenga kama kawa.

Watu wananunua ndinga kama kawa.

Watu wanaanzisha miradi kama kawa.

Watu wanakula starehe sana sana usiku kucha nchi nzima.

Watu wanavaa vizuri.

Shauri yako.

IMF wansemaje?

Je number za uchumi zikoje ?
 
Makamanda wameacha siku hizi kupiga kelele kuhusu uchumi!
 
Huku mitandaoni sasa kumeshakuwa ni sehemu ya uhalisia mbadala [alternate reality].

Ukiishi huku utaambiwa na kuaminishwa kuwa huku uraiani sasa hivi hakukaliki. Utaaminishwa [na kama ukiwa mjinga, mvivu, na zuzu, utaishia kuamini kweli] hali ya maisha ni mbaya mno. Hayo utayoaminishwa yatakufanya ujenge taswira nyingi mno kichwani.

Unaweza ukapata taswira ya kwamba sasa hivi Watanzania wengi wanalala njaa. Watanzania hawana nguo za kuvaa. Maduka hayana bidhaa. Watu wanakula nyasi na panya kama ilivyokuwa huko Zimbabwe miaka kadhaa iliyopita. Watoto wa shule hawana kalamu wala daftari. Watu hawanywi pombe. Hawali kitimoto. Hawaogi. Hawana magari. Hawachepuki. Na mengineyo lukuki.

Lakini mtu ukiachana na hayo maneno ya kwenye mitandao na uingie mwenyewe uraiani ujionee na upate tajiriba ya uhalisia wa mambo, utaishia kuhitimisha kuwa huko kwenye mitandao kuna upotoshaji na utiaji chumvi mkubwa sana.

Tembea tu huku na kule jijini Dar, nenda mikoa mingine na wilaya zake, utaona maisha ya watu yanaenda tu kama ilivyo siku zote.

Mara umekutana na msafara wa harusi. Umekaa kwa Mangi unakunywa Konyagi yako ya kupimiwa mara ghafla unaona kigoma kinapita na watu, wake kwa waume, wakubwa kwa watoto, wanajiachia tu.

Sasa kama uko ni mtu wa tafakuri, utajiuliza, ‘mh...hivi hiyo hali mbaya inayozungumziwa huko kwenye mitandao ndo ipi hasa’?

Kwa hiyo, kusema ukweli mimi nakataa kabisa. Nabisha. Nasema hali si mbaya. Hali iko vile vile tu ambavyo imekuwa karibu siku zote, ukiondoa labda enzi zile ambapo watu tulikuwa tunaenda kupanga mstari kwenye maduka ya ugawaji kununua mikate ya Siha, sukari, sabuni za Mbuni na Mbunju, na mahitaji mengine.

Zaidi ya hapo, kelele kelele za huko mitandaoni hazina mashiko. Ni za watu wanaotapa tapa tu. Wafamaji.

Wakatabahu,

Alhaji N. Ngabu [emoji6].
Usifikiri watu wote wanahali kama yako.
 
Waliodai tuna hali mbaya mitandaoni naona hawajaja nyumbani toka waondoke, kwa kweli hali ni nzuri, namba wani, fanya kazi au biashara halali, kwa nguvu zote, fuata sheria bila shuruti, ishi maisha yako, angalia matumizi ya kipato chako, jali familia yako zaidi na zaidi, utashangaa waishi poa tu na hata bata utakula mpaka utalichoka, sasa ukitaka ya vurugu na kuvunja amani shauri yako, nenda mwenyewe uone cha mtema kuni...
 
Huku mitandaoni sasa kumeshakuwa ni sehemu ya uhalisia mbadala [alternate reality].

Ukiishi huku utaambiwa na kuaminishwa kuwa huku uraiani sasa hivi hakukaliki. Utaaminishwa [na kama ukiwa mjinga, mvivu, na zuzu, utaishia kuamini kweli] hali ya maisha ni mbaya mno. Hayo utayoaminishwa yatakufanya ujenge taswira nyingi mno kichwani.

Unaweza ukapata taswira ya kwamba sasa hivi Watanzania wengi wanalala njaa. Watanzania hawana nguo za kuvaa. Maduka hayana bidhaa. Watu wanakula nyasi na panya kama ilivyokuwa huko Zimbabwe miaka kadhaa iliyopita. Watoto wa shule hawana kalamu wala daftari. Watu hawanywi pombe. Hawali kitimoto. Hawaogi. Hawana magari. Hawachepuki. Na mengineyo lukuki.

Lakini mtu ukiachana na hayo maneno ya kwenye mitandao na uingie mwenyewe uraiani ujionee na upate tajiriba ya uhalisia wa mambo, utaishia kuhitimisha kuwa huko kwenye mitandao kuna upotoshaji na utiaji chumvi mkubwa sana.

Tembea tu huku na kule jijini Dar, nenda mikoa mingine na wilaya zake, utaona maisha ya watu yanaenda tu kama ilivyo siku zote.

Mara umekutana na msafara wa harusi. Umekaa kwa Mangi unakunywa Konyagi yako ya kupimiwa mara ghafla unaona kigoma kinapita na watu, wake kwa waume, wakubwa kwa watoto, wanajiachia tu.

Sasa kama uko ni mtu wa tafakuri, utajiuliza, ‘mh...hivi hiyo hali mbaya inayozungumziwa huko kwenye mitandao ndo ipi hasa’?

Kwa hiyo, kusema ukweli mimi nakataa kabisa. Nabisha. Nasema hali si mbaya. Hali iko vile vile tu ambavyo imekuwa karibu siku zote, ukiondoa labda enzi zile ambapo watu tulikuwa tunaenda kupanga mstari kwenye maduka ya ugawaji kununua mikate ya Siha, sukari, sabuni za Mbuni na Mbunju, na mahitaji mengine.

Zaidi ya hapo, kelele kelele za huko mitandaoni hazina mashiko. Ni za watu wanaotapa tapa tu. Wafamaji.

Wakatabahu,

Alhaji N. Ngabu [emoji6].
Wanafiki bhana
Inamaana wewe hujui vitu vimepanda bei karibu mara dufu na mshahara ule ule zaidi ya miaka mitano?
Inamaana wewe hujui kama marupurupu kazini eidha yamepunguzwa au yamekatwa?
MFANO ni Allowance ya chakula kwa jeshi wakati wa Jakaya ilikua sh. 10 000 kwa sasa ni sh 3 000
Sasa niambie chakula kumepanda bei mara dufu 3000 utakula milo mitatu?
Wakati chakula bei chini 10 000 kwa siku ilikua inatosha mpaka inabaki ya vocha

Anyways ninyi wengine mpo kwenya Mavi 8 hamuwezi kujua kinachoebdelea
 
Attachments

  • ma V8.mp4
    4.3 MB
Back
Top Bottom