Nakaribia kudhulumiwa, naombeni ushauri

Hujawahi kusikia malalamiko ya mwenye nyumba kuzulumiwa na mpangaji?
 
Sasa kama ni hivyo unakwama wapi
 
Nenda kwa mkuu wake wakazi....namaandishi hayo kama ushaidi,utanishukuru baadaye
 
Wote huwa ni wamoja, raia anaweza asisikilizwe.
Sio kweli kuna jamaa ni fundi ujenzi iliwahi mtokea kuna mjeda mmoja *2 alimuita fundi kuja mrekebishia nyumba yake na fundi alivyomaliza jamaa akawa anamzingua kumlipa hela kama laki 5 hivi na ushee kila fundi akikumbushia kuhusu hela yake jamaa anamletea vitisho vingi mixer matusi jamaa akaona sasa amefika ukingoni akaomba ushauri kwa wadau wakampa muongozo jinsi ya kwenda kupata haki yake jamaa akaufuata mpaka akafika kwa mwajiri wake jeshini nadhani ni upanga akapokelewa nakutoa malalamiko yake hapo hapo jamaa akapigiwa simu akaulizwa uko wapi jamaa akasema sijui yuko mwenge akaambiwa nakupa dakika 15 uwe umeshafika hapa, kweli bhana jamaa akafika ile anaingia tu anakutana na jamaa anayemdai akashtuka kilichooendelea hapo ni siri ya kambi ila mkuu wake aliamlisha akatwe kwenye mshahara wake na fundi aliondoka na mzigo wake siku ile ile
 
Inategemea na aina ya bosi
 
Inategemea na aina ya bosi
Inategemea na aina ya bosi
Chief kule makao makuu yao huwezi fanywa kitu chochote maana cdf wao yupogo kule alaf jeshi ni nidham kwanza yule *2 alivyofika tu kwa mwajir wake akaambiwa apunguze urefu mbele ya jamaa aliyepeleka malalamiko ndio akaanza kujibu maswali aliyoulizwa na boss wake ambae ni mwajiri wake ……..kwaiyo iyo kitu unayowaza wewe kule hakuna nii nadhalia tu za mitaani izo tumejimezesha
 
Hawa wajeda wapuuzi sana.
Nilipanga kwa mmoja, ila nyumba ilitaka ukarabati kabla ya kuingia. Jamaa kasema hana pesa, nitangulize kodi ili aitumie kurekebisha nikaona fresh.. nimelipia miezi 6 akasema ndani ya siku tatu kutakuwa tayari. Siku 3,5,wiki, wiki ya pili.. nkaona mazoea yanazidi nikaamua kumjia juu, akasema njoo ulete vitu nyumba tayari. Nikaenda kupaona aisee.. ukarabati low budget.. choo hajaweka mlango. Nkamwambia mwenye nyumba jiheshimu basi, me naingiaje kuko hivi.. eti ooh nimeona una haraka sana, sasa we leta tuu vitu af tutaendelea kupaweka sawa. Nkamwambia siingii nyumba iko hivi.

Maneno yakawa mengi, mwisho wa siku tukashindwana nkamwambia anirudishie kodi yangu siingii kwake tena.. tukenda mpaka kuandikishana kwa mwenyekiti wa mtaa. Kufika kwa Mwenyekiti kumbe wanafahamiana [emoji24] lakini tukaenda hivyo hivyo. Makubaliano yalikuwa anilipe baada ya mwezi. Yaaani anavyonisumbua saivi.. Bora nichukue namba pale juu nimrogee.. maana haiwezekani pesa yangu inisumbue tena kuifuatilia. Yeye kakaa kimya, mimi nna kazi ya kumpigia daily, na kiswahili kingi.. shida saivi tupo mikoa tofauti.. Bora nimroge tuu.. at akifa sio mbaya.
 
Hii scenario yako imenitia moyo sana mkuu. Nashukuru mno! Umebaki utekelezaji tu.
 
Bravo mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…