Niliamua kuishi kama Lowassa miaka 24 iliyopita, nimetambua sikufanya makosa. Nipo njiani kwenda Monduli

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Mwaka 2000 niliamua kuishi kama Lowasa, nilishawishiwa sana na upendo uliokuwepo ndani ya wana CCM na jamii dhidi yake. Kuna wakati nilichukia matendo yake hasa pale alipokuwa akifanya kampeni za Arumeru dhidi ya aliyeelezwa kuwa ni mkwe wake.

Lakini baadaye niligundua kwamba kosa halikuwa lake kwani kila mwanasiasa angetamani familia yake isitawaliwe bali itawale. Nilifuta chuki yangu baada ya Kikwete kusogeza watoto na mke kwenye uso wa siasa hasa baada ya yeye kustaafu.

Nilimpenda na kumthamini Lowasa katika mambo yafuatayo ya kisiasa ndani ya nchi yetu na siasa za Afrika
1. Katika maisha yake ya siasa sikuwahi kumsikia akitumika kama CHAWA wa viongozi wake.

2. Katika kila aliloliamini alisonga mbele kwa mikakati mikubwa na mipango iliyosukwa vyema kwenye misingi ya uendeshaji serikali

3. Nilivutiwa sana pale alipoamua kila kata pawe na sekondari, na hapa ndipo tulipolikomboa taifa kutoka shule kufaulisha watoto wawili kwenda sekondari na sasa shule nyingi darasa zima linaweza kuendelea sekondari. Kama siyo maono ya Lowasa leo vision ya kuweka elimu ya sekondari kuwa lazima yasingefikiwa.

4. Alifanya maamuzi magumu yasiyo na athari kwa nchi kwa kusimamia maji yatoke ziwani yaje Kahama. Leo ni jambo la kushangaza Bariadi hakuna maji, Bunda kuna shida ya maji, maswa kuna shida ya maji wakati haya maeneo yote yapo karibu na ziwa Victoria.

5. Jk alipomsaliti hakumtukana wala kumbeza, alikaa kimya. Matokeo yake JK kama boinadamu wengine alikasirika na ukimya wa Lowasa na kumwona kama adui kwake. Yote hayo lowasa hakuwahi kusikika akieleza hasira zake dhidi ya waliomsaliti.

6. Kwa kuwa alikuwa anaamini katika kile alichoambiwa na ubongo wake aliondoka CCM na kwenda Chadema, akapata kura nyingi kupita mgombea wa CCM lakini wakina Januari, Kinana na Nape wakaona kuishi kwao hapa Dunia wametumwa kumdhulumu haki yake kwa goli la mkono. Mungu alivyo mkubwa waliyemsaidia kwenda Ikulu kwa kuwa alijua ni waska tonge aliwaadhibi mmoja mmoja adharani.

7. Baada ya uchaguzi mkwe wake akakamatwa na kuwekwa ndani kwa uhujumu uchumi, ikapelekea akubaliane na mashinikizo ya familia akarejea CCM kama CCM walivyotaka. Baada ya kurejea CCM hakuna siku amewahi kuwadharau wala kuwatusi CHADEMA. Aliendelea kuthamini utu na wema waliomtendea.

Leo mzee wetu amelala, natambua wazi kwamba kuishi kwangu kama yeye kutasaidia wengi kama alivyowasaidia wengi. Ni mwanasiasa pekee ambaye ameondoka Duniani na nchi kuungana pamoja kumlilia kila mmoja akieleza wema na matendo yake yanavyoweza kulisaidia Taifa kufikia hitajio la mweneynzi Mungu la AMANI, UPENDO NA USHIRIKA MTAKATIFU.

Naanza safari Misungwi naamini tutafika salama tulioamua kuishi kama Lowasa.
 
Jk alipomsaliti hakumtukana wala kumbeza, alikaa kimya. Matokeo yake JK kama boinadamu wengine alikasirika na ukimya wa Lowasa na kumwona kama adui kwake. Yote hayo lowasa hakuwahi kusikika akieleza hasira zake dhidi ya waliomsaliti.
Ndiyo maana nataka kauli ya wahenga isemayo "malipo ya dhulma ni hapa hapa duniani" ifutwe.

Kwasabb sijaona ilifanya kazi kwa JK baada ya kumdhulumu Lowasa.
 
Back
Top Bottom