Kulipa kisasi baada ya watoa haki kutotoa haki

MIRIMA

Member
Jul 17, 2023
83
265
Leo nimekumbuka tukio la mauaji kijijini kwetu miaka kama 12 iliyopita.Kulikuwa na migogoro ya ardhi jinsi mnavyojua changamoto ya ardhi nchini kwetu , migogoro ilichukuwa muda mrefu sana na kesi ya ardhi ilifika hadi mahakama ya wilayani badae eneo liligawiwa pasupasu na Kila familia ikawekewa mipaka yake.

Kumbe familia moja hawakuridhika na mgao huo wakafanya mbinu wakavamia baba wa familia (upande mwingine wa familia) wakamkata na mapanga wakamuua .Baba yule alikufa kifo kibaya sana nilimwona Kwa Macho ,mwanae tulikuwa tunasoma nae secondary enzi hizo na hata kusoma usiku tulikuwa tunasoma nae (tulikuwa kama tupo ghetto hivi) .

Tuliamka asubuhi na mapema tunaenda shule tukaona watu wamekusanyika nikamwambia jamaa /rafiki yangu (mtoto wa marehemu) tupitie hapa tujue kitu gani kinaendelea mbona Kuna mkusanyiko mkubwa... asee...asee kufika tukamkuta baba wa rafiki yangu amechinjwa kama nyama watu wanasubiri police amefunikwa na kanga...asee ..asee maumivu yalikuwa makali Kwa rafiki yangu pamoja na Mimi mwenyewe.

Badae tulizika na kesi ikaenda mahakamni huko na wawuaji walijulikana mnavyojua nchi yetu jamaa walionga huko mahakamani wakakutwa hawana hatia ,walikuwa na hela hela kidogo wakarudi mitaani . Familia ya rafiki yangu hawakuwa na uwezo wa kukataa rufaa na wao wakaacha hivyo hivyo lakini nakumbuka walisema Kwa Siri WATALIPA KISASI HATA KAMA ITACHUKUWA MIAKA MIA MOJA.


Marehemu alikuwa na vijana watatu kipindi hicho hawakuwa na pesa na walikuwa bado vijana coz wapili ndio alikuwa class mate wangu na tulikuwa tunalingana umri. Baada ya muda tulitawanyika na Kila mtu kaenda kivyake kiutafutaji na hata mawasiliano ilikata coz tulitoka nyumbani Kila mtu akaanza kupambana kivyake.

Sasa bwana wale watumiwa wa mauaji waliondoka pale kijijini wakaenda mikoa tofauti walikuwa mtu na mdogo wake ,Mzee wao alibaki nyumbani ,inasemekana mipango yote alichora Mzee na wanae hao.

Wale familia ya rafiki yangu Mungu aliwabariki wakawa na unafuu wa maisha kibongo bongo tuna sema Middle class hivi..(wana kanyumba na ka usafiri Kila mtu ) .Sasa hawa vijana wenye tuhuma ya mauji wameuwawa huko mwaka moja iliyopita Kwa kuchinjwa chinjwa ikisemekana wameuliwa na majambazi huko mikoani.

Mimi nikiunga dot sina uhakika lakini nawaza WADAU WATAKUWA WAMELIPIZA KISASI . tukio ilifanyika baada ya hao vijana kutembeleana na wakavamiawa na kuchinjwa mpaka kufa. Na hii imetokea baada ya watoa haki kutanguliza rushwa Kwa kutotoa haki .
 
Ila Wahenga walikuwaga na akili sana, ujue walisema ukiua kwa upanga utauliwa kwa upanga.

Ila sio lazima kisasi cha jamaa zako, inawezekana ni karma tu imechukua nafasi yake
 
Back
Top Bottom