Najuta kuoa mwanamke mwenye mtoto

Najuta kuoa mwanamke mwenye mtoto

Waheshimiwa habari za mida,

Mimi ni IT specialist kwenye shirika moja lisilo la kiserikali mshahara wangu ni wa kati si mkubwa sana wala si mdogo sana. Lakini pia mimi ni lecturer part time nafundisha jioni wafanyakazi katika chuo kimoja hapa DSM, Nimeoa na nina watoto wawili, huyu mke wangu ni chotara wa Kiarabu.

Wakati tumeanza kudate hakuniambia kama ana mtoto na kwa kweli alivyo mzuri sikutilia shaka kama ana mtoto maana hata nyonyo zake zilikua zimesimama kama mtoto anaebalehe.Baadae mapenzi yaliponoga ndipo akaniambia kuwa ana mtoto alie darasa la kwanza yupo kwa mama mzazi yaani bibi wa mtoto.

Kwa kuwa nilikua tayari nimezama kwenye mahaba mazito ikabidi nikubali tu maana by that time nilishatangaza ndoa ilikua ni point of no return. Ila mchumba alinihakikishia kuwa mtoto wake hatakua kikwazo kwenye ndoa yetu na kwamba huduma zote za malezi ikiwa ni pamoja na shule, malazi, maradhi na mengineyo yatakua chini ya baba wa mtoto.

Huo ndio ukawa mkataba wetu na kwamba mtoto ataishi kwa bibi na baadae atahamia kwa baba mzazi ambae ni Mwarabu mwenzie. Akabadli dini kuja ukristo tukafunga ndoa haikua shida maana mama ake pia ni mkristo baba ndio muislam na aliwatelekeza siku nyingi.

Miezi sita baada ya ndoa akamleta mtoto kwetu kuishi permanent kinyume na mkataba wetu, anyway nikawa na roho ya utu nikasema haina shida kuepusha shari. Mtoto wake alipofika darasa la nne wakampeleka boarding sisi hapo tuna watoto wawili mapacha wa miaka minne kasoro nadhani mimi ndie nililipa ada ya boarding.

Siku moja katikati ya wiki nilibeba mahitaji kadhaa nikampelekea yule mtoto shuleni, niliomba wakaniruhusu kuingia pale Surprisingly Matron akaniambia huyo mtoto mbona ana vitu vya kutosha. Mama yake na baba yake walikua hapa juzi siku tano hivi zimepita. Akaniuliza kwani wewe ni nani wa mtoto nikamweleza, akashangaa akaniambia mbona walikua wamekaa na mtoto kama ni familia inayoishi pamoja.

Akanipa kama umbea flani hivi nilishangaa kwa kuwa mke wangu hakuniambia kama alienda kwa mtoto na mzazi mwenzie alikuwepo. Visiting day moja nikaenda na watoto wangu kumuona mwenzao, mke wangu aliondoka mapema akatangulia tulipofika pale tukakuta jamaa nae yupo wamekaa na mtoto na wife.

Mshikaji akaaga bila kunisalimia akaondoka zake nilishindwa kumwelewa, nikazuga tukaendelea na mengine hatimae yule mtoto akamaliza la saba. Mama yake akamtafutia shule nzuri sana yenye matokeo mazuri kila mwaka kimbembe kikaja kwenye ada, mimi nikamwambia mwisho wangu ilikua ni la saba.

Sasa walipe wenyewe maana watoto wangu pia wameanza shule ya Mapadre Lieberman ada wote wawili ni million sita kwa mwaka bado nina mdogo wangu wa kike anasoma chuo nalipa mimi ingawa ana mkopo asilimia ishirini. Bado gharama za uendeshaji familia za kila siku, hivyo nikamwambia sitaweza kulipa, ni vema babaake ajipange kulipa.

Wakuu kwa kauli yangu hiyo ulizuka mgogoro mkubwa, Huduma zote muhimu nilisitishiwa pamoja na za chumbani akaondoka akarudi kwao kwa mwezi mzima baada ya kusuluhishwa akarudi mimi nikashikilia msimamo kuwa silipi ada.

Hivi karibuni wakati hayupo nimeingia kwenye mapenzi na mdada jirani yangu amepanga upande anaishi na ndugu, wife amerudi sina hamu nae tena. Huyu mdada jirani nimekua nikimpa lift asubuhi kwa muda mrefu sasa na ndipo tukaelewana na anajua matatizo yetu, alikua akitusaidia sana nyumbani wakati wife ameondoka.

Nimedhamiria kumuacha wife mazima nimeshachoka, juzi baba amekuja akaniambia nilikushangaa ulipojifanya mjuaji kuoa mwanamke mwenye mtoto tukakuzuia ukalazimisha sasa umeyaona.

Wakuu nipo njia panda, ushauri tafadhali

Mimi nakupa ushauri wa kiroho ( Katika perspective ya African Spirituality ). Katika ulimwengu usio onekana, ukimuoa mwnamke ambaye tayari ana mtoto maana yake ni kwamba, una uhusiano wa kiroho na huyo mtoto. Wewe na huyo mtoto wa huyo mwanamke mliwahi kuwa na uhusiano wa damu, katika maisha yenu yaliyopita (Previous life ). Uhusiano huo wa kiroho unaweza kuwa wa heri au shari. Wa heri kwa maana ya kwamba, amekuja kulipa fadhila ulizo mfanyia katika maisha yenu yaliyo pita, na wa shari kwa maana amekuja kulipa kisasi kwa mambo mabaya uliyo mfanyia katika maisha yenu yaliyo pita. So kuwa na mwanamke ambaye tayari ana mtoto sio tatizo sana, kama unaamini katika hicho nilicho kiandika. BUT IF U DONT BLV ON THAT! MTAANI HUKO WANASEMAGA " unajifanya unajua sana kulea watoto wasio kuhusu". But all in all. Kuoa mwanamke mwenye watoto tayari kuna changamoto sana. Mtaani kwetu kuna jamaa mmoja alikuwa na watoto wawili, baadaye akaoa mwanamke ambaye na yeye alikuwa na watoto wawili. Kwa pamoja wakazaa watoto w engine watatu. Siku moja mume akakuta watoto wao wa nje ( wale wanne ) wanawapiga watoto wao wale watatu. Basi jamaa akampigia simu mke wake akimwambia " MY WIFE COME HOME EARLY, BECAUSE MY CHILDREN AND YOUR CHILDREN ARE BEATING OUR CHILDREN "
 
marehemu baba . inshaa,allah m/mungu amfanyie wepesi kaburini .na kumbuka alishawai kunihambia nita kapopata wepesi wa kuowa nisije howa mwanamke mwenye mtoto .hivyo basi broo kabla ya kuhowa kwanza ungetafuta ushauri hila na kusisitizia usimsomeshe huyo dogo .mitoto ya siku hizi haina akili baadae hata kutenda
 
usimwache huyo mkeo wa kiarabu wala huyo bint cheza kote kote kama alivyokufanyia yeye dawa ya moto ni moto kaka
 
hapa napata picha kua huyo mkeo na mzazi mwenzie wanakulana pia behind your back. ikiwa mawasiliano yako heavy hivyo wanaenda shule pamoja, hapa jamani Paulsen.paulsen hesabu mke unasaidiwa, BCB = baby come back, ipo ya nguvu ndio maana taarifa hupewi. inawezekana kwa sababu moja ama nyingine hawakuweza kuolewa na mzazi mwenzie, maana kila kitu kinapangwa na mungu lakini mapenzi walikua nayo. Mwarabu aliamua kuolewa na wewe si kua anakupenda sana ila ni baada ya kuona keshazalishwa, akakupata wewe kama bahati, hivyo akaona atoe gundu, lakini ukweli ni kwamba mapenzi mazito yako kwa mzazi mwenzie. Tuna ndugu na marafiki zetu pia waliooa wanawake wenye watoto lakini sijasikia kua kuna mawasilisiliano ya siri na wazazi wenzao mpaka kuonana bila mume mwenye mke kuhusishwa. hapa akili kumkichwa kaka. Ila na wewe penzi la jirani limezidi kunoga maana huku nyumbani kumesha kua disturbed na mama kuwasiliana na mzazi mwenzie. hapo lazima uvunjike moyo, na ndio maana unaona jirani mambo safi, japo yanaweza yasiwe safi kama unavyodhania. hapo unasukumwa na frustration za ndoa, hivyo kua mwangalifu.
 
Ushauri mzuri na kutambua kosa wengi wameeleza kwa uzuri ila mimi ushauri wangu weye hukutakiwa kuja hapa kuomba ushauri kwa suala ambalo lipo wazi hapo kuna kigugumizi gani?
 
Aisee inauma sana, sijui kwa nini wanakuwaga hv hawa watu. Single mother kama hajapata wa kumuoa ni mpole kweli, akiolewa usumbufu mtupu!
 
Inataka moyo kuishi na mwanamke mwenye mtoto, na tena usije kuta huyo jamaa aliezaa nae ndo aliemtoa bikira.. Kisanga man, hawezi msahau na unaweza kuta ulivyo kuwa unawakuta shule walikuwa wanakumbushiana. Lakin mi sioni point ya kumwacha mwanamke kwasababu ya ada, labda kama una mengine
 
Duh hii inanitisha wadau nina mahusiano na mwanamke mwny wwatoto wawili nimefall kweli kweli na nafikiria kutangaza nia lakini hili hua linaniumiza kichwa kweli kweli, dah nimepata funzo hapa
 
Pole hujajua habari za Machotara (Waarabu) ni lazima watarudiana tu,
kwani huyo Mkeo kule alishaonekana ni Haramu toka kwa Mama yake aliyezalishwa na mwarabu
akaja kuzaliwa yeye chotara wa kiarabu na akaenda kuzaa na mwarabu hicho kizazi hakutakupenda nata huyo mtoto akikua atakudharau tu
ACHANA NAO TAFUTA ANATEKUFAA
 
hapa napata picha kua huyo mkeo na mzazi mwenzie wanakulana pia behind your back. ikiwa mawasiliano yako heavy hivyo wanaenda shule pamoja, hapa jamani Paulsen.paulsen hesabu mke unasaidiwa, BCB = baby come back, ipo ya nguvu ndio maana taarifa hupewi. inawezekana kwa sababu moja ama nyingine hawakuweza kuolewa na mzazi mwenzie, maana kila kitu kinapangwa na mungu lakini mapenzi walikua nayo. Mwarabu aliamua kuolewa na wewe si kua anakupenda sana ila ni baada ya kuona keshazalishwa, akakupata wewe kama bahati, hivyo akaona atoe gundu, lakini ukweli ni kwamba mapenzi mazito yako kwa mzazi mwenzie. Tuna ndugu na marafiki zetu pia waliooa wanawake wenye watoto lakini sijasikia kua kuna mawasilisiliano ya siri na wazazi wenzao mpaka kuonana bila mume mwenye mke kuhusishwa. hapa akili kumkichwa kaka. Ila na wewe penzi la jirani limezidi kunoga maana huku nyumbani kumesha kua disturbed na mama kuwasiliana na mzazi mwenzie. hapo lazima uvunjike moyo, na ndio maana unaona jirani mambo safi, japo yanaweza yasiwe safi kama unavyodhania. hapo unasukumwa na frustration za ndoa, hivyo kua mwangalifu.

Unaweza kunisaidia mawazo kuhusu tatizo sugu la ada ya mtoto maana ndilo tatizo lililonileta hapa kuomba ushauri
Hilo la uzinzi lina ngazi ya familia na wazee walishahusika nalo
Kama ingekua ni uzinzi pekee nisingekuja hapa lina mahala pake

Hili LA mtoto ndio limeondoa amani ya nyumba na limeshindikana kwenye ngazi zote
Watu wengi wananipa ushauri kwa jambo ambalo sijaomba ushauri (uzinzi) na ambalo Nina suluhisho tayari
Wanaacha kichwa cha somo husika ambacho ndio kimebeba dhana nzima ya somo hili
 
kwa haraka haraka nakuona hupo makini katika suala la kuoa. Kwanza unaangalia zaidi urembo wa mke na sio tabia yake naa vigezo vingine. Unajiamini nini kuoa mtu asiye wa dini au imani yako. Mbaya zaidi muarabu, ulifikiri ungeweza kuishi na binti mwenye asili ya kiarabu.
Kama huyu anakusumbua sana, tulia kwanza utafakari kabla ya kukurupuka na mchepuko huo unausema jirani yako, sijui unaupa lifti nk. Huyo nae atakuja kukufrustrate mpaka utahisi dunia haikupendi kumbe wewe hupo makini katika kufanya maamuzi ya mwanamke wa kuoa.

Kosea jambo lingine lakini sio mke wa kuoa. Utajutaje? Pole
 
Duh hii inanitisha wadau nina mahusiano na mwanamke mwny wwatoto wawili nimefall kweli kweli na nafikiria kutangaza nia lakini hili hua linaniumiza kichwa kweli kweli, dah nimepata funzo hapa

Wewe huyo mwanamke endelea naye, unajua kila mtu ana experience yake. Yaliomkuta huyu don't think na wewe utapata.
 
Well, kwa nn unasema nisimwache mke wangu hadi nithibitishe amezini wakati juu umesema in a big picture kuna zinaa?

Kumwacha mke wangu kunatokana na kushindwana kwetu juu ya gharama za malezi ya huyo mto, kuzini hata asingekua na huyo mtoto anaweza kuzini tu
Na pengine hata humu ndani watu wengi wana migogoro ya uzinzi wanajua wenyewe inavyotatulika
Hakuna mtu kati yetu alieoa au kuolewa anaweza kusimama kifua mbele kusema kuwa mwezie ni mwaminifu 100%

Tunaishi kwa imani tu na wenzetu
Ivyo ndugu addict namuacha mke wangu kwa kuushindwa mgogoro niliohangaika nao kwa miaka kadhaa Wa mtoto wake

Huyu mtoto amegeuka mwiba kwa maisha yangu na watoto wangu tumekwenda kila sehemu unayoijua kusuluhishwa imeshindikana
Hivyo simuachi mke wangu kwa uzinzi namuacha kwa kuwa mtoto wake kawa kikwazo cha furaha ya familia yangu

Wachangiaji wengi wameshauri sawa sawa na nilivyoamua
Huyo mtoto bado ana safari ndefu ya maisha ina maana tutasumbuana siku zote za maisha ya huyu mtoto

Kama ingekua ni uzinzi pekee na si mtoto basi wala usingeniona hapa nawashirikisha katika hili

Tunakubaliana na wewe tu kuwa kuzini angazini tu, hapa umeleta tatizo la mtoto, lakini tatizo tulilo liona sisi sio mtoto, kuna kamchezo unachezwa, kwanza kumfumania au kupata taarifa kuwa anakwenda kumuona mtoto bila ya taarifa yako, pili kwenda pamoja na baba yake mtoto shuleni bila ya kuwapo wewe.
Tatu kulazimishwa wewe umlipie ada mtoto mtoto.

Jee wewe binafsi haya masuala unayo majibu gani?
Toka uwanze kulipa ada ni miaka mingapi? Una jua hao watu washaonana mara ngapi bila ya wewe kujua?
Suala moja tu la kutoka kwako kwenda kuonana na haram yake ni kosa kubwa kwako na kwa Allah.
Sisi waislam suala hilo ni kubwa sana, mi naweza vunja n guu yake na red card juu
 
Mkuu look at the bigger picture

Hapo kuna Usaliti...Kama huuoni labda ni kwa namna wewe ulivyoiandika hii stori inatufanya tufikirie hilo.

Why akufiche kwenda kuonana na baba Mtoto?

Hapo kuna tatizo...na tatizo hili ni la ndani...la kwenye pichu...ndio limesababisha haya yote....

Kaa na mke wako...Usimwache mke wako.....hadi pale inapobidi sana....utawatesa watoto mno.....Msimamo wako usilipe tena ada....Ulikosea tangu mwanzo wewe mwenyewe kukiuka hayo makubaliano na kuanza kulipa....Yo have set the precedence......

Usimwache mkeo isipokua tu utakapothibitisha kuna zinaa

Mwenyewe kakuambia mengine kayaweka tu ili uelewe ukubwa wa tatizo na tabia za mkewe,
Ila kubwa kwake ni huyo mtoto kumlipia ada ndio ugomvi wao mkubwa.
 
haaaaaaaaaaaa! haaaaaaa.ebwanaee.haaaaaaaaa.we acha tu.hawa wanawake ni mama zetu.lkn! ebu tumia akiri yako kwani hii ni inssue inayohusu maisha yako yote uliyobakiza duniani.ila mungu atakusaidia kwani unajitaidi kuhakikisha wanao wanavuka.
 
marehemu baba . inshaa,allah m/mungu amfanyie wepesi kaburini .na kumbuka alishawai kunihambia nita kapopata wepesi wa kuowa nisije howa mwanamke mwenye mtoto .hivyo basi broo kabla ya kuhowa kwanza ungetafuta ushauri hila na kusisitizia usimsomeshe huyo dogo .mitoto ya siku hizi haina akili baadae hata kutenda

kwani mkuu wewe UMESHAHOWA au bado hupo hupo sana?
 
Back
Top Bottom