Najua nchi pekee duniani ambayo huchaguliwa Rais wa nchi na nchi nyengine ni Zanzibar

Hakuna nchi inaitwa Zanzibar.
Wakati mwingine tuache unafiki tuwe wakweli. Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.
Kwa hivyo rais wa Zanzibar ni sawa na mkuu wa mkoa au sijakuelea vizuri? Sidhani Muheshimiwa anayo musafara "hevi " magari kumi pungufu kiduchu,karibu Zanzibar ushuhudie mwenyewe.
 
Kwa hivyo rais wa Zanzibar ni sawa na mkuu wa mkoa au sijakuelea vizuri? Sidhani Muheshimiwa anayo musafara "hevi " magari kumi pungufu kiduchu,karibu Zanzibar ushuhudie mwenyewe.
Hata Bashite anakuwa na msafara mkubwa tu.
Zanzibar si mkoa, lakini si nchi vile vile.
 
Yes Zanzibar ni nchi nje ya Muungano na ndani ya mipaka tuu ya Tanzania, lakini ndani ya Muungano, Tanzania ni nchi moja tuu ya Jamhuri ya Muungano wa union, Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT. Nje ya mipaka ya nchi ya Tanzania, hakuna nchi yoyote duniani inayoitwa Zanzibar, ila kuna eneo linaloitwa Zanzibar ambalo ni sehemu ya JMT, nchi hi moja tuu, JMT.

Kwa vile nje ya Muungano Zanzibar ni nchi, then rais wa Zanzibar atachaguliwa na Wazanzibari wenyewe, lakini kwa vile ana wajibu wa kuulinda Muungano, then ni jukumu la JMT kuhakikisha, atakayekuwa rais wa Zanzibar ni lazima awe mtu atakaye ulinda na kuudumisha muungano.

Hivyo hata Wazanzibari mkichagua kipenzi cha Zanzibar, kama JMT ina mashaka na Uzalendo wake kwa Muungano, then atakaye tangazwa ni yule mdumisha Muungano wetu adhimu na kuyaenzi yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
P
Baelezee
 
https://www.goodreads.com/author/show/3389.Stephen_King
Some birds are not meant to be caged, that's all. Their feathers are too bright, their songs too sweet and wild. So you let them go, or when you open the cage to feed them they somehow fly out past you. And the part of you that knows it was wrong to imprison them in the first place rejoices, but still, the place where you live is that much more drab and empty for their departure.
Stephen King
 
Nimeshakufafanulia thread ya juu

Ukiulizwa Zanzibar ni nini basi jibu ifuatavyo:-

Ni sehemu tu ya Jamuhuri ya Muungano....ila ukitatizwa sana unaweza kuita ni mkoa

Bila shaka mwalimu wako alipata shida kubwa kukufundisha, pamoja na mfano huo bado tu huelewi!!?.

Mnasema Zanzibar siyo nchi, kama ni hivyo basi ni nini??, hapa ninahitaji jina lake.

Unasema tuiite ni sehemu ya jamhuri ya Tanzania, mimi sikatai kwa sababu hata Dar, Tanga, Mbeya nk, ni sehemu za Jamhuri ya Tanzania lakini maeneo hayo yanaitwa MAJIJI, au chukua Kigoma,Kagera, Mtwara nk, hiyo ni mikoa ambayo ni sehemu ya jamhuri ya Tanzania.

Swali ni hili Zanzibar ni sehemu ya jamhuri ya Tanzania, sasa tuiite kwa jina lipi??.

Unasema tunaweza kuiita mkoa, wewe unachekesha sana toka lini mkoa ukawa na Rais?!, mawaziri, baraza la wawakilishi??. Isitoshe pia huko kuna mikoa;-- unguja kaskazini, Unguja mjini magharibi, Unguja kusini, wete nk. Sasa kama Zanzibar iitwe mkoa vipi hiyo mikoa yake iitweje??!. Lots of confusions.

Kipindi tunaungana 1964, Zanzibar ilikuwepo kama nchi na hadi sasa ipo kama nchi, ni Tanganyika tu ndiyo iliyokufa, na waanzilishi wa huo Muungano walikuwa na malengo yao zama hizo na kumbuka kwamba kipindi hicho waafrika tulikuwa wachache na wenye elimu na hamasa za kisiasa walikuwa wachache mno, leo ni tofauti na ndiyo maana ipo haja ya kuufanyia "review" huo muungano ili uendane na haja na maslahi ya sasa ninaposema haja ninamaanisha hata kuufuta pia ni haja kwani upande mmoja wa muungano wanasema wanadhulumiwa na kugandamizwa.

Kama wazee wetu Nyerere na Karume wangefufuka leo na kuona muungano bado upo vilevile walivyouacha bila shaka watatuona sisi mazwazwa kwasababu zama hizi ni zama za mabadiliko siyo kama zama zao.
 
Very good insight
 
Mimi binafsi naomba juhudi zenu zifanikiwe. Hatuwezi kuendelea na vitu feki au hewa. Zanzibar irudishiwe utaifa wake iwe mwanachama wa UN. Baada ya hapo tushirikiane Kama majirani wa kawaida. Vitakuwepo virabsha kama kawaida. Sio hoja tutakakwenda tu.

Lakini utaifa wa Zanzibar ukirudi, mchukue tahadhali. Pemba wasije kuona wanaonewa na Unguja. Yatakuwepo lakini busara ya viongozi itahitajika mno.

Kila la heri.
Naona Pascal kaamua kuninyamazia, hivi ni kweli wazanzibari wameridhia? Au hajui maisha ya watu yanavyo wagharimu toka kuasisiwa?
 
Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT, hivyo mtu yoyote ili kutangazwa kuwa rais wa Zanzibar, ni lazima awe ni mtu atakaye ulinda muungano.

Ndio maana kuna mtu kila siku anashinda kwenye sanduku la kura, lakini hapewi, kwa sababu determinant wanajua Muungano wetu adhimu utakuwa mashakani.
P
HUU MUUNGANO??
HUU NI UKOLONI MLIOUVISHA KOTI LA MUUNGANO NA YANAMWISHO WAKE HAYA
 
Naona Pascal kaamua kuninyamazia, hivi ni kweli wazanzibari wameridhia? Au hajui maisha ya watu yanavyo wagharimu toka kuasisiwa?
Mkuu Ghibuu, sijakunyamazia bali nimekueleza kuwa issue ya Zanzibar kuridhia Muungano ni issue kubwa inayojitegemea na mimi nimeizungumza sana humu. Ukipata muda tembelea nyuzi hizi

P
 
Nakumbuka vizuri hii. Nilikuwa UDSM wakati huo. Wanafunzi tulishangilia kwa nguvu zote. Nakumbuka ulikuwa DSTV ukiwa bwana mdogo tu. Nakumbuka pia kuwa DSTV ilipigwa faini kwa jambo hilo. Na TV stations wakati huo zinahesabika. Na wenye TV receivers chuoni walikuwa pia kiduchu. Wakati wa taarifa ya habari ama drama pendwa watu walijikusanya katika vyumba vya wachache wenye TV receivers. Miaka 24 imepita sasa. Waliozaliwa 1995 sasa wamekuwa watu wazima! Sisi tunafikiria kustaafu sasa!
Ni mimi ndiye niliyeutangaza ule ushindi wake wa 1995 na from then, independent tallying ikapigwa marufuku na kuwa ni kosa kisheria.

Numbers don't lie. Nenda NEC kaangalie matokeo ya 2015 ya kura za Magufuli na Lowassa kwa upande wa Zanzibar utanielewa
Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda - JamiiForums.
P
 
Nakumbuka vizuri hii. Nilikuwa UDSM wakati huo. Wanafunzi tulishangilia kwa nguvu zote. Nakumbuka ulikuwa DSTV ukiwa bwana mdogo tu. Nakumbuka pia kuwa DSTV ilipigwa faini kwa jambo hilo. Na TV stations wakati huo zinahesabika. Na wenye TV receivers chuoni walikuwa pia kiduchu. Wakati wa taarifa ya habari ama drama pendwa watu walijikusanya katika vyumba vya wachache wenye TV receivers. Miaka 24 imepita sasa. Waliozaliwa 1995 sasa wamekuwa watu wazima! Sisi tunafikiria kustaafu sasa!
Mkuu Omusolopogasi, ilikuwa ni DTV na sio DSTV.
P
 
Bila shaka mwalimu wako alipata shida kubwa kukufundisha, pamoja na mfano huo bado tu huelewi!!?.

Mnasema Zanzibar siyo nchi, kama ni hivyo basi ni nini??, hapa ninahitaji jina lake.

Unasema tuiite ni sehemu ya jamhuri ya Tanzania, mimi sikatai kwa sababu hata Dar, Tanga, Mbeya nk, ni sehemu za Jamhuri ya Tanzania lakini maeneo hayo yanaitwa MAJIJI, au chukua Kigoma,Kagera, Mtwara nk, hiyo ni mikoa ambayo ni sehemu ya jamhuri ya Tanza lipi??.

We ni king'ang'anizi sana......Tuna nchi moja tu!, nayo ni Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania...ambayo ukipenda kufupisha 'kuokoa muda' unataja neno Tanzania linatosha.

Hakuna nchi nyingine ndani ya nchi ya Tanzania....Na ndio maana nikaandika kwamba ukitatizwa sana we sema Zanzibar ni mkoa, na kiukweli Zanzibar ina hadhi ya kimkoa.
 
Bobwe, kwanza najikubali, mimi ni mjinga kwa mambo yoyote nisiyo yajua, na mtu mwingine yoyote akiwa hajui kitu fulani, akadhani anajua ni mjinga tuu, na kutokujua huko ndio ujinga wenyewe.

Nimesema kwenye muungano wenzetu mmelishwa ujinga mwingi na mkaumeza mazima mazima, kwanza mlidanganywa Karume hakusaini muungano, nikakuletea document yenye saini ya Karume na picha akisaini.

Pili mkasema Zanzibar haikuridhia muungano, nikakuambie Karume aliridhia kwa niaba ya Wanzanzibari.
Japo ni kweli Zanzibar hawakufanya process ya ratification, lakini ukitekeleza ni kuridhia
Mayalla hawa watu hawajui hata wanaloliomba. matatizo ya wazanzibar wengi wana umiss utawala wa Sulatan wa Oman na pia wanataka kuifanya Zanzibar islamic State hivyo chini ya MUungano hilo wanajua halitafanikiwa kabisa. Na zaidi wanaotaka huu muungan uvunjike siyo vijana bali wazee.
 
We ni king'ang'anizi sana......Tuna nchi moja tu!, nayo ni Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania...ambayo ukipenda kufupisha 'kuokoa muda' unataja neno Tanzania linatosha.

Hakuna nchi nyingine ndani ya nchi ya Tanzania....Na ndio maana nikaandika kwamba ukitatizwa sana we sema Zanzibar ni mkoa, na kiukweli Zanzibar ina hadhi ya kimkoa.

Wewe ndiye king'ang'anizi usiyeelewa kitu, nimekupa mifano rahisi huelewi au unajisingizia kutoelewa, ni kupoteza muda tu.

Kwa sababu hata jina "Tanzania" hujui mtu aliyebuni,😁😁--aliyebuni jina hilo ni Mohamed Iqbal Dar. Na alitumia muundo huu:-

Kutoka neno "Tanganyika" alichukua herufi "Tan" na kutoka neno "Zanzibar" alichukua herufi "Zan" na baadaye akaziunganisha kupata herufi "Tanzan", yeye akaona herufi hizo hazina ladha ya kimatamshi akaona aongeze herufi " I " kutoka katika jina lake la "Iqbal", na ikawa neno "Tanzani", hapo bado akaona halijapendeza kimatamshi na akaamua kuongeza herufi "a", herufi ya kwanza kutoka katika jina la dhehebu lake la kiislamu, dhehebu la Ahmadiyya.
Ndipo jina TANZANIA likapatikana.

Hapo utaona kimsingi TANZANIA ni jina lilotokana na muunganiko wa majina ya nchi mbili zilizoungana likitiwa vionjo mwishoni mwake na herufi " ia".

Nchi iliyokufa ni Tanganyika lakini Zanzibar ipo na inayo serikali inayoitwa "serikali ya mapinduzi ya watu wa zanzibar" na inaye raisi na katika sherehe za mapinduzi Raisi wa Tanzania anaalikwa kama mgeni tu kama wageni waalikwa mfano mabalozi.

Ninachotaka kusema ni kuwa "structure" ya muungano iko hovyo sana na ndiyo maana kero zake haziishi licha ya kuwepo kwa chombo cha kutatua hizo kero, nasi tumepumbazwa tukidhani kuwa muungano ni "God created always sacred " na tunasahau kwamba waasisi wake walikuwa binadamu "who can be overtaken by human shortcomings".

Kuna mkuu mmoja kutokana na human "weakness and shortcomings", kwa hadhi yake, alifanya kosa baya la jinai hadharani kwa kumshauri waziri wake avute bangi kwa kificho ili awe mkali katika kutekekeza kazi zake, hapo the die hards watasema ni "ushauri adhimu" kwa kuwa kasema kiongozi 😁😁, halikadhalika katika mambo mengine viongozi wanaweza kukosea au kupatia lakini faida yake ikawa ni ya muda fulani tu na ndivyo ulivyokuwa huu Muungano, a review is inevitable this time around.

Kama Zanzibar ni mkoa basi hata Tz bara ni mkoa.😁
 
Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT, hivyo mtu yoyote ili kutangazwa kuwa rais wa Zanzibar, ni lazima awe ni mtu atakaye ulinda muungano.

Ndio maana kuna mtu kila siku anashinda kwenye sanduku la kura, lakini hapewi, kwa sababu determinant wanajua Muungano wetu adhimu utakuwa mashakani.
P
Sehemu ya JMT yaani ni kama mikoa mingine?
 
Back
Top Bottom