Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unavyozidi kuwa wa kipekee na wa mfano wa kuigwa duniani kote

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
327
414
MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR UNAVYOZIDI KUWA WA KIPEKEE NA MFANO WA KUIGWA DUNIANI KOTE.

Na Bwanku M Bwanku.

Kila ifikapo Aprili 26 kila mwaka, Tanzania huadhimisha siku Maalum ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliounganisha Mataifa haya mawili na kuzaa Tanzania hii ya leo.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) mpaka mwaka huu 2023, asilimia 94 ya Watanzania wasasa ni wale ambao wamezaliwa baada ya tukio hili kubwa na la kihistoria la Muungano. Kwa lugha rahisi ni kwamba Watanzania wengi wasasa wamezaliwa baada ya tukio hili na hivyo si wengi wanaofahamu mengi kuhusu Muungano huu.

Mpaka sasa ni asilimia 6 pekee ya Watanzania ndiyo walikuwepo wakati wa Muungano huu adhimu wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa mazingira kama haya, ni muhimu kuchambua na kueleza maana ya Muungano wetu huu na upekee wake. Sasa tusonge.

Baada ya Mataifa mengi ya Afrika kupata Uhuru wake miaka ya 1960's kutoka kwa unyonyaji wa Wakoloni, Mataifa mengi yalihitaji kujenga Dola zenye nguvu kuongoza Mataifa yao na ndipo hoja za Umoja wa Afrika, miungano mbalimbali ilianza kuonekana kama silaha ya kuyapeleka mbele kwa haraka Mataifa ya Afrika baada ya kupata Uhuru wake.

Baada ya Tanganyika kipindi hicho kupata Uhuru wake 9 Disemba, 1961 kutoka kwa Mwingereza chini ya Uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na Zanzibar nayo kufanikisha Mapinduzi yake ya Januari 1964 chini ya Uongozi wa Sheikh Abeid Amani Karume yaliyoondosha utawala wa kinyonyaji wa Kisultani, Mataifa haya chini ya Viongozi wake hao wawili Wakuu walikubaliana kuunda Dola moja ya Tanzania kutoka kwenye Mataifa yao huru ya Tanganyika na Zanzibar ili kujenga Taifa moja imara la Tanzania.

Jumatano Aprili 22, 1964, Viongozi Wakuu waasisi wa Muungano huu kwa maana ya Hayati Mwalimu Nyerere na Hayati Sheikh Karume walikutana Zanzibar na kusaini Hati ya Mkataba wa Makubaliano ya kuunda Muungano (Articles of Union) kabla ya kupelekwa Bungeni Jumamosi Aprili 25,1964 ambako ulipitishwa kwa kishindo na Mabunge yote ya Tanganyika na Zanzibar na hatimaye rasmi Jumapili Aprili 26, 1964 Muungano huu adhimu wa Tanganyika na Zanzibar ukazaliwa na kuunda rasmi Dola moja yenye nguvu ya Tanzania hii tunayoiona leo.

Sasa ni takribani miaka 59 toka kuzaliwa kwa Muungano huu adhimu unaozidi kuimarika siku hadi siku huku ukiwa umeshaleta Mapinduzi makubwa ya Kiuchumi, Maendeleo na Kijamii kwa pande zote mbili huku changamoto na kero mbalimbali zilizopo na zinazojitokeza zikiendelea kutatuliwa kila mara na hivyo kuufanya Muungano huu uendelee kuishi, kuwa imara na kuwa mfano wa kuigwa kote Duniani wakati huu Dunia ikishuhudia Miungano mingi iliyowahi kufanyika Barani Afrika na kote Ulimwenguni ikivunjika na kuparanganyika muda mfupi toka kuundwa kwake, lakini Muungano huu ukizidi kuimarika siku hadi siku na kugeuka kuwa Tunu na kustaajabisha Ulimwenguni kote.

Muungano huu umeendelea kuushangaza dunia kwa namna unavyoendelea kuimarika siku hadi siku na kudumu miaka kwa miaka wakati kukiwa na orodha ndefu na kubwa ya Miungano ya Mataifa iliyokufa na kusahaulika kabisa mingi ikichukua miaka 5 mpaka 7 na mingine ikifa kwa utitiri wa changamoto nyingi sana bila kuwa na matokeo yoyote lakini huu wa Tanganyika na Zanzibar ukiwa wa Kihistoria na Maendeleo makubwa sana ndani yake.

Sasa hapo chini nakuletea dondoo za maajabu kuuhusu Muungano wetu huu unaondelea kuushangaza ulimwengu.

Kwanza; Muungano huu unachukua sura ya Kipekee ya kuwa Muungano ulioasisiwa na Mashujaa wawili, ukiundwa baada ya viongozi wakuu Waasisi na wapambania uhuru wawili wa nchi zao yaani Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanganyika na Sheikh Abeid Amani Karume wa Zanzibar kutia saini na kubadilishana hati za Muungano Aprili 26, 1964 zilizopelekwa Mabunge ya pande zote na kuchanganya mchanga wa Tanganyika na Zanzibar kuashilia kuzaliwa kwa Taifa moja la Tanzania.

Lakini pili, Muungano huu unaweka historia ya kuwa Muungano pekee uliobaki Afrika licha ya kuwa na Miungano mingi sana huko nyuma. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndio Muungano pekee uliobaki baada ya Muungano wa nchi nyingine zote zilizowahi kuungana Afrika kuvunjika na kufa kuanzia ule wa Ghana, Guinea na Mali uliokufa mwaka 1963, wa Senegal na Gambia (Senegambia) uliokufa mwaka 1989, wa Misri na Syria uliokufa 1961, ule wa Cameroon na wa Djibouti na Eritrea.

Muungano uliodumu zaidi Afrika na wa mfano Duniani kote. Mpaka sasa Muungano wetu una miaka 59 toka kuzaliwa kwake Aprili 1964 na bado umeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka. Hakuna Muungano mwingine uliowahi kuishi kwa kipindi kirefu hivyo kuanzia yote iliyoanzishwa Afrika. Ule wa Cameroon ulichukua miaka 6, wa Ghana, Guinea na Mali ndio ulikuwa wa mfupi zaidi kwa kuchukua miaka 5 tu, wa Senegal na Gambia (Senegambia) miaka 7, wa Misri na Syria haukuishi hata miaka 10 n.k.

Zaidi huu ni Muungano uliojaa umoja, amani na mshikamano. Huu unabaki Muungano pekee kwasasa duniani uliobarikiwa kila tunu za upendo, udugu, umoja, amani, masikilizano na mshikamano kuliko tulivyoshuhudia Maungano mengine yote ambayo yalijaa kero, kutosikilizana na mivutano mizito iliyosababisha mpaka ikavunjika na kufa. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeunda Dola moja ya Tanzania inayofanya watu wa pande zote mbili kuingiliana kiuhuru kiuchumi, kijamii, kitamaduni na kisiasa bila bughudha, masharti wala vikwazo vyovyote vile. Leo mtu wa Bara anaweza kwenda kuoa, kufanya biashara, kutembea na kufanya chochote atakacho Visiwani na mtu wa Visiwani vivyo hivyo kwa Bara, jambo lilioufanya Muungano huu kuwashangaza wengi kwa namna ulivyo imara na kuwa mfano wa kujifunza, kivutio na kuigwa kote duniani.

Tuendelee kuulinda, kuuenzi na kuudumisha Muungano wetu huu adhimu kabisa na wa mfano kote duniani.

Bwanku M Bwanku.
Screenshot_20230425-211718.png
 
Hili ni tangazo la gazeti,lipia au upigwe ban

USSR
 
Taja faida Moja ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar?
Yaan hakuna faida yoyote kwa watu wa bara.. kama ni unadhani natania wambie watu wataje watu wabara wanapata nini kwenye huu Muungano uone kama kuna mtu ata taja hata moja..
Ila waambie wataje faida kwa Wanzabari uone watakavyo tiririka mpaka 100
 
Maamuzi kaliyoyafanya miaka ya 60s yamesimama mpaka leo. Ndo maana kanisa katoliki wamemfanya mtakatifu na wanamuomba awaombee!
FB_IMG_1682541285886.jpg
 
Back
Top Bottom