Tunaishi kwenye nchi yenye watu 60M+ ambayo wenye uhakika wa ajira ni Rais wa JMT na Zanzibar tu

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Mfumo wetu wa ajira nchini hasa ajira rasmi upo mikononi mwa wanasiasa. Leo wanasiasa wanaweza wakaamua Nani aajiriwe kwenye sekta binafsi au sekta ya umma. Wanasiasa pia wanaweza kuamua Nani afanye business Nani asifanye business. Kwa msingi huu wapo watu wawili Tu wenye uhakika wa ajira nchini; watu hao ni Mhe. Rais wa JMT na Rais wa Zanzibar.

Kwa tafsiri nyingine ni kwamba usijiachie Sana ukajiona unajimudu; mwenye kusema unajimudu au la ni mmoja. That's y hakuna mwanasiasa WA upinzani aliyeajiriwa kwenye utumishi wa umma; si Kwa Sababu Hana vigezo Bali mfumo unamtaka mwasiasa yeyote awe mtii Kwa ccm vinginevyo Hana nafasi yakupata ajira na akipata akaonyesha msimamo wake kisiasa lazima apigwe chini.

Wanasiasa wetu wengi waliojiweka wazi wanabaki kuishi Kwa mishemoshe ikiwemo business ambayo pia wakionekana wanachupua nakupata mpunga Sana wanadidimizwa.

Kwa mantiki nyingine ni vigumu nchi kuendelea Kwa kuamini kwenye fikra za watu wawili ; tulipaswa tuwe na watu wa vyama vyote kwenye sekta ya umma ili tuone mchuano wa idea na uchapaji KAZI.

Katiba mpya itusaidie kuweka usawa WA ajira Bila kujali itikadi za siasa
 
Tuongeze nguvu tupate Katiba mpya KATIBA MPYA itaweka Misingi ya usawa na haki ya kuajiriwa badala ya kuwasuburi Wanasiasa Watuamulie
 
Katiba mpya itusaidie kuweka usawa WA ajira Bila kujali itikadi za siasa
Maneno mazima naongezea ikija tume huru piga kura kwa wapinzani ondoa ccm. Miaka 5 ijayo baada ya wapinzani watakuja viongozi halisi wa kuongoza nchi wenye akili sio wenye itikadi.
 
Back
Top Bottom