Nailyne
JF-Expert Member
- Dec 11, 2010
- 350
- 111
Mke kapata safari nje ya nchi, (training) safari hiyo inahusisha kikundi cha watu sita kutoka Tanzania,(funded trip) siku moja akiwa nyumbani kwake na mumewe anapigiwa simu na mmoja wapo wa wale watu sita ambao anatarajia kusafiri nao kuwa safari imesogezwa siku 10 mbele.Mke anamtaarifu mumewe kuwa amepata simu kuwa safari imehairishwa, na anamtajia jina la huyo aliyepiga simu, mume akahamaki akadai huyo jamaa yeye anamjua vizuri sana ni muhuni sana, hakuishia hapo akaanza kumlaumu mkewe iweje amempa namba huyo mwanaume? na kwa nini huyo mwanaume anampigia simu mkewe?
Mke akamjibu mumewe kuwa huyo mwanaume anatarajia kusafiri naye, na wamefahamiana kwa sababu ya hiyo safari na wamepeana namba ili wajulishane yanayojiri kipindi wanajiandaa na safari na hiyo simu amepigiwaa kumpa update ya safari, na akamuuliza mumewe je kwa kuwa huyo mwanamme amempigia simu mkewe basi hicho ni kigezo tosha kuwa ameshalala nae? mume akahamaki kwa nini amejibiwa hivyo,akaanza kumpiga mkewe kwa hasira, mkewe akafanikiwa kutoroka humo ndani na baadae akarudi. Bahati mbaya huyo mke alikuwa mjamzito, na matokeo yake mimba ikatoka usiku wa tukio hilo. Huyo mke alienda training yake na akarudi ila hajarudi kwa mumewe akarudi nyumbani kwao kwa wazazi wake,hamtaki tena mumewe, na anadai hiyo sio mara ya kwanza kupigwa.
Binafsi najiuliza hivi mtu akioa basi anakuwa amepewa rungu la kumpiga mkewe? Ee Mungu ninusuru mja wako.