najiuliza..

Nailyne

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
350
111
Mke kapata safari nje ya nchi, (training) safari hiyo inahusisha kikundi cha watu sita kutoka Tanzania,(funded trip) siku moja akiwa nyumbani kwake na mumewe anapigiwa simu na mmoja wapo wa wale watu sita ambao anatarajia kusafiri nao kuwa safari imesogezwa siku 10 mbele.Mke anamtaarifu mumewe kuwa amepata simu kuwa safari imehairishwa, na anamtajia jina la huyo aliyepiga simu, mume akahamaki akadai huyo jamaa yeye anamjua vizuri sana ni muhuni sana, hakuishia hapo akaanza kumlaumu mkewe iweje amempa namba huyo mwanaume? na kwa nini huyo mwanaume anampigia simu mkewe?

Mke akamjibu mumewe kuwa huyo mwanaume anatarajia kusafiri naye, na wamefahamiana kwa sababu ya hiyo safari na wamepeana namba ili wajulishane yanayojiri kipindi wanajiandaa na safari na hiyo simu amepigiwaa kumpa update ya safari, na akamuuliza mumewe je kwa kuwa huyo mwanamme amempigia simu mkewe basi hicho ni kigezo tosha kuwa ameshalala nae? mume akahamaki kwa nini amejibiwa hivyo,akaanza kumpiga mkewe kwa hasira, mkewe akafanikiwa kutoroka humo ndani na baadae akarudi. Bahati mbaya huyo mke alikuwa mjamzito, na matokeo yake mimba ikatoka usiku wa tukio hilo. Huyo mke alienda training yake na akarudi ila hajarudi kwa mumewe akarudi nyumbani kwao kwa wazazi wake,hamtaki tena mumewe, na anadai hiyo sio mara ya kwanza kupigwa.

Binafsi najiuliza hivi mtu akioa basi anakuwa amepewa rungu la kumpiga mkewe? Ee Mungu ninusuru mja wako.
 
Hakuna mwanaume hapo,huyo ni wa kiume tu.
Utampigaje mkeo kwa kujitungia mambo kama huko na tena mjamzito.
Tena alitakiwa kwenda kumshtaki kabisa.
OTIS.
 
Huyo Jamaa inawezekana ana matatizo ya Kisaikolojia, badala ya kumlaumu tafuteni namna ya kumsaidia kuondokana na tatizo lake!
 
Huyo Jamaa inawezekana ana matatizo ya Kisaikolojia, badala ya kumlaumu tafuteni namna ya kumsaidia kuondokana na tatizo lake![/QUOTe

inawezekana usemalo,maana inashangaza kwa mtu mzima kuact that way
 
hana matatizo yoyote. Mtu mwizi humuona mwenzie ni jambazi. Huyo mwanaume ni fuska ndo maana anafikiri na mkewe anafanya kama yeye.
 
Wanaume wengine bwana! baada yakutafuta njia yakumthibiti mkewe kwa penzi anamdhibiti kwa fimbo sasa awaachie wenzie wale kwa raha zao...
 
mwanaume ama mwanamke ambae hajiamini hafai kuwa partner wa mtu kabisaa! utamjua mtu ambae hajiamini kwa behaviour zake tu toka wakati mna-date. sie wanawake tuna tabia ya kujifariji kuwa 'jamaa ana obsessions kwa sababu bado hajanioa, ama mie ni mzuri sana' etc. tunasahau kuwa watu hawabadiliki unless they want to! tabia haina dawa, tena hapo ndo jamaa gauge ya kujiamini imeshashuka hadi 0, akirudi kwake ndo itakua kila kitu anahisi unafanya becoz of that incident. ila ya wanandoa mengi banaa,utashangaa siku unawaona wanapita wameshikana mikono,wanasaka mimba ingine!
hivi insecurity dawa yake nini?
 
Wanaume wengine bwana! baada yakutafuta njia yakumthibiti mkewe kwa penzi anamdhibiti kwa fimbo sasa awaachie wenzie wale kwa raha zao...

nikatika maswali niliyokuwa najiuliza sikupata majibu,ukimpiga ndio utafamya mkeo akupende zaidi? au ndio unaongeza tatizo lingine? kweli akili ni nywele
 
mwanaume ama mwanamke ambae hajiamini hafai kuwa partner wa mtu kabisaa! utamjua mtu ambae hajiamini kwa behaviour zake tu toka wakati mna-date. sie wanawake tuna tabia ya kujifariji kuwa 'jamaa ana obsessions kwa sababu bado hajanioa, ama mie ni mzuri sana' etc. tunasahau kuwa watu hawabadiliki unless they want to! tabia haina dawa, tena hapo ndo jamaa gauge ya kujiamini imeshashuka hadi 0, akirudi kwake ndo itakua kila kitu anahisi unafanya becoz of that incident. ila ya wanandoa mengi banaa,utashangaa siku unawaona wanapita wameshikana mikono,wanasaka mimba ingine!

yawezekana kuna vitabia aliviona lakini hilo la kumpiga halikuwepo kabla ya ndoa, na hilo lakurudiana kwa kweli ntashangaa lakini as u said mambo ya wanandoa huwa hayatabiriki, ila kwa mtazamo wangu its likely jamaa akarudia tena kumpiga maana watu wenye hizi tabia mhhhh
 
mi naona lazima huyo mwanaume atakua anamfaham yule mpiga sim katika njia zisizo halali na akaona either jamaa atampenda mke wake (kwa maana ya kumpenda physicaly) au atamwambia mambo yao huko waliko kutana na uoga wa optiona na b (or even combo) akaamua aue hiyo safari.
Mke asirudi kwa huyo mwanaume tena, anedelee na maisha yake. Mwambie abusive men wanamaneno matam sana yanaweza kumconvince ila asirudi kabisa!!!
 
Nikisikia mwanaume anampiga mkewe nashindwa kabisa kuelewa. Unampiga ili iweje? Unamfundisha tabia wakati kesha komaa?

Ila nikisoma hii thread kuna something wrong. Nani alikuwa ana fund hiyo safari? Kama ni foreign institution, naona kuna utata wa kumpa taharifa third part aje amwambie huyo dada kuwa safari imesogezwa. Je huyo jamaa alikuwa ni coordinator? Naona safari imekaa ki informal informal.

Kingine huyo mdada alikuwa hajuhi tabia za mumewe. Ukijua mumeo ana mawivu ya kupitiliza inabidi uepuke kugawa namba za simu kwa kila mtu.
 
mke kapata safari nje ya nchi, (training) safari hiyo inahusisha kikundi cha watu sita kutoka tanzania,(funded trip) siku moja akiwa nyumbani kwake na mumewe anapigiwa simu na mmoja wapo wa wale watu sita ambao anatarajia kusafiri nao kuwa safari imesogezwa siku 10 mbele.Mke anamtaarifu mumewe kuwa amepata simu kuwa safari imehairishwa, na anamtajia jina la huyo aliyepiga simu, mume akahamaki akadai huyo jamaa yeye anamjua vizuri sana ni muhuni sana, akuhishia hapo akaanza kumlaumu mkewe iweje amempa namba huyo mwanaume? na kwa nini huyo mwanaume anampigia simu mkewe?mke akamjibu mumewe kuwa huyo mwanaume anatarajia kusafiri naye, na wamefahamiana kwa sababu ya hiyo safari na wamepeana namba ili wajulishane yanayojiri kipindi wanajiandaa na safari na hiyo simu amepigiwaa kumpa update ya safari, na akamuuliza mumewe je kwa kuwa huyo mwanamme amempigia simu mkewe basi hicho ni gezo tosha kuwa ameshalala nae? mume akahamaki kwa nini amejibiwa hivyo,akaanza kumpiga mkewe kwa hasira, mkewe akafanikiwa kutoroka humo ndani na baadae akarudi. Bahati mbaya huyo mke alikuwa mjamzito, na matokeo yake mimba ikatoka usiku wa tukio hilo. Huyo mke alienda training yake na akarudi ila hajarudi kwa mumewe akarudi nyumbani kwao kwa wazazi wake,hamtaki tena mumewe, as anadai hiyo sio mara ya kwanza kupigwa.

Binafsi najiuliza hivi mtu akioa basi anakuwa amepewa rungu la kumpiga mkewe? Ee Mungu ninusuru mja wako.

Kaaazi kweli kweli! wasameheane, mke arudi nyumbani.
 
Nikisikia mwanaume anampiga mkewe nashindwa kabisa kuelewa. Unampiga ili iweje? Unamfundisha tabia wakati kesha komaa?

Ila nikisoma hii thread kuna something wrong. Nani alikuwa ana fund hiyo safari? Kama ni foreign institution, naona kuna utata wa kumpa taharifa third part aje amwambie huyo dada kuwa safari imesogezwa. Je huyo jamaa alikuwa ni coordinator? Naona safari imekaa ki informal informal.

Kingine huyo mdada alikuwa hajuhi tabia za mumewe. Ukijua mumeo ana mawivu ya kupitiliza inabidi uepuke kugawa namba za simu kwa kila mtu.

una akili mno wewe.....
tumesahu hili.kidume kimpe mkeo taarifa kikiwa kama nani??//
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom