Najibu hoja za ndugu Humphrey Polepole kuhusu mwelekeo mpya wa nchi yetu

Walau wewe umetoa na suluhu ya mjadala

Kifupi bwana polepole kanyang'anywa tonge mdomoni so anajaribu kutuliza maumivu kwa kukosoa

Siyo mchezo kutoka VITAMU HADI VICHUNGU

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Ad hominen fallacy!!!
Mkosoe Polepole kuhusu hoja zake.
Hapa umemshambulia yeye badala ya kushambulia hoja zake kwa kupitia hoja zako.
 
Hoja kuu ya Polepole ni unyonyaji na ukandamizaji unaofanywa na nchi za Magaribi (Ulaya na Marekani) kwa nchi masikini kama zetu.
Ni kwa bahati mbaya sana ndugu Polepole anazungumza kama mpigania uhuru wa miaka ya 60.
Polepole anapaswa kufahamu kwamba hakuna mtu atakeyetoka nje ya nchi yetu akatupendelea kuliko yeye anavyojipendelea. Kwa dunia ilipofikia sisi kama nchi zinazoendelea hatuwezi kuachana na nchi za magharibi na kukua kivyetu. Tunawahitaji kama wabia wa maendeleo.

Tunahitaji kufanya nao biashara, tunahitaji misaada yao, tunahitaji uwekezaji wao. Katika yote hiyo hatuwezi kujidanganya kuwa watafanya kwa masilahi yetu. Daima watafanya kwa masilahi yao. Ni jukumu letu kujua ni kwa namna gani nasi katika sahani ileile tunayokula na wazungu nasi tunashiba.

Polepole anasema mbona China imeweza kukua. Mtu yeyote anayedhani China imeendelea bila Magharibi basi ni mjinga. China imefika ilipo kwa kuweka mikakati mizuri ya kufaidi mahusiano yake na Magharibi. Kabla ya kuondoka kwa mwenyekiti Mao, China ilikuwa masikini. Baadaye waliochukua mamlaka ya China waliingiza falsafa za Magharibi. Wakapewa hadhi ya kupendelewa zaidi na Marekani (Most Favoured Nation). China ikapeleka watu wake kusoma Marekani na Ulaya, Ikafanya biashara na Magharibi bila vikwazo. China ilipoona imesomesha vizuri kwenye shule za Magharibi ikaruhusu kampuni za magharibi kuwekeza Wachina wakakopi teknolojia kiurahisi na sasa ndio wauzaji wa kila kitu pale Kariakoo.

Sisi tumefanya nini? Elimu yetu ni duni. Tunazo rasilimali lakini hatuwezi kuzitumia ipasavyo kwakuwa ni mbumbumbu. Dunia inapohitaji dhahabu huwezi kuigomea kwakuwa kanuni ya kiuchumi ni kwamba rasilimali zitaenda kule zinakohitajika. Ili kushindana katika rasilimali ni lazima ujenge uwezo wa ndani katika matumizi ya rasilimali. Vinginevyo hautazuia watu wa nje kuzitumia. Leo hii unafungua shule ya sekondari isiyo na maabara wala walimu wa sayansi. Nani mbaya kati ya sisi na magharibi? Wazungu waliacha shule zilizokamilika hapa. Miaka 60 baadaye unafungua shule nusu. Upumbavu.

Pia ni ujinga kufikiri kuwa China ni mtu mzuri kuliko magharibi. Pengine China ni mbaya kuliko Marekani na Ulaya. China anatukopesha kirahisi lakini anatudai kibabe. Anatumia mikopo yake kutawala masoko yetu na hivyo kuua uwezo wetu, ubunifu wetu. Mpaka sasa Tanzania hatuwezi kubuni kitu kwakuwa bidhaa zote zinatoka China kwa bei rahisi, ila ubora utajua mwenyewe mteja. Hakuna nafasi kwa vijana wetu kufanya chochote zaidi ya kuwa machinga wa kuzurura na takataka za China. China imezibana pumzi nchi kadhaa masikini kupitia mikopo yake. Mkopo wa China aghalabu hauna vigezo vingi wala ufuatiliaji. China hajali mkopo utatumikaje na hivyo kuweka mwanya kwa wabadhirifu kutumia mikopo hovyo na kuongeza deni la taifa bila manufaa kwa umma.

Hizo enzi ambazo Polepole anasifia kuwa zilionesha kupambana na magharibi zimemdanganya jamaa huyu. Kilichofanyika ni kuhamisha maadui kwa muda. Polepole anafahamu kuwa tuliendela kutegemea fedha za magharibi kwenye sekta nyeti za elimu na afya.

Sasa kama mtu anafadhili elimu ya watu wako, afya ya watu wako unasemaje unaondokana naye kama sio kudanganya wajinga?

Mimi nafikiri kinachopaswa kufanyika ni serikali kujenga uwezo wa watu wetu kwenye maarifa na baadaye mitaji ili waweze kupambana vema kwenye uchumi wa dunia. Mambo ya harakati dhidi ya magharibi kwa mtindo wa upigania uhuru hayana tija na ni kujidanganya. Kwa sasa kinachoweza kutusaidia ni diplomasia na intelijensia ya kiuchumi.

CHINA HANA HURUMA, MAGHARIBI HAINA HURUMA
Moja ya makala yenye akili niliyopata kusoma humu JF kwa mwaka huu 2021.
 
Back
Top Bottom