Najibu hoja za ndugu Humphrey Polepole kuhusu mwelekeo mpya wa nchi yetu

Fight ClimateChange

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
294
261
Hoja kuu ya Polepole ni unyonyaji na ukandamizaji unaofanywa na nchi za Magaribi (Ulaya na Marekani) kwa nchi masikini kama zetu.

Ni kwa bahati mbaya sana ndugu Polepole anazungumza kama mpigania uhuru wa miaka ya 60.
Polepole anapaswa kufahamu kwamba hakuna mtu atakeyetoka nje ya nchi yetu akatupendelea kuliko yeye anavyojipendelea. Kwa dunia ilipofikia sisi kama nchi zinazoendelea hatuwezi kuachana na nchi za magharibi na kukua kivyetu. Tunawahitaji kama wabia wa maendeleo.

Tunahitaji kufanya nao biashara, tunahitaji misaada yao, tunahitaji uwekezaji wao. Katika yote hiyo hatuwezi kujidanganya kuwa watafanya kwa masilahi yetu. Daima watafanya kwa masilahi yao. Ni jukumu letu kujua ni kwa namna gani nasi katika sahani ileile tunayokula na wazungu nasi tunashiba.

Polepole anasema mbona China imeweza kukua. Mtu yeyote anayedhani China imeendelea bila Magharibi basi ni mjinga. China imefika ilipo kwa kuweka mikakati mizuri ya kufaidi mahusiano yake na Magharibi. Kabla ya kuondoka kwa mwenyekiti Mao, China ilikuwa masikini. Baadaye waliochukua mamlaka ya China waliingiza falsafa za Magharibi. Wakapewa hadhi ya kupendelewa zaidi na Marekani (Most Favoured Nation). China ikapeleka watu wake kusoma Marekani na Ulaya, Ikafanya biashara na Magharibi bila vikwazo. China ilipoona imesomesha vizuri kwenye shule za Magharibi ikaruhusu kampuni za magharibi kuwekeza Wachina wakakopi teknolojia kiurahisi na sasa ndio wauzaji wa kila kitu pale Kariakoo.

Sisi tumefanya nini? Elimu yetu ni duni. Tunazo rasilimali lakini hatuwezi kuzitumia ipasavyo kwakuwa ni mbumbumbu. Dunia inapohitaji dhahabu huwezi kuigomea kwakuwa kanuni ya kiuchumi ni kwamba rasilimali zitaenda kule zinakohitajika. Ili kushindana katika rasilimali ni lazima ujenge uwezo wa ndani katika matumizi ya rasilimali. Vinginevyo hautazuia watu wa nje kuzitumia. Leo hii unafungua shule ya sekondari isiyo na maabara wala walimu wa sayansi. Nani mbaya kati ya sisi na magharibi? Wazungu waliacha shule zilizokamilika hapa. Miaka 60 baadaye unafungua shule nusu. Upumbavu.

Pia ni ujinga kufikiri kuwa China ni mtu mzuri kuliko magharibi. Pengine China ni mbaya kuliko Marekani na Ulaya. China anatukopesha kirahisi lakini anatudai kibabe. Anatumia mikopo yake kutawala masoko yetu na hivyo kuua uwezo wetu, ubunifu wetu. Mpaka sasa Tanzania hatuwezi kubuni kitu kwakuwa bidhaa zote zinatoka China kwa bei rahisi, ila ubora utajua mwenyewe mteja. Hakuna nafasi kwa vijana wetu kufanya chochote zaidi ya kuwa machinga wa kuzurura na takataka za China. China imezibana pumzi nchi kadhaa masikini kupitia mikopo yake. Mkopo wa China aghalabu hauna vigezo vingi wala ufuatiliaji. China hajali mkopo utatumikaje na hivyo kuweka mwanya kwa wabadhirifu kutumia mikopo hovyo na kuongeza deni la taifa bila manufaa kwa umma.

Hizo enzi ambazo Polepole anasifia kuwa zilionesha kupambana na magharibi zimemdanganya jamaa huyu. Kilichofanyika ni kuhamisha maadui kwa muda. Polepole anafahamu kuwa tuliendela kutegemea fedha za magharibi kwenye sekta nyeti za elimu na afya.

Sasa kama mtu anafadhili elimu ya watu wako, afya ya watu wako unasemaje unaondokana naye kama sio kudanganya wajinga?

Mimi nafikiri kinachopaswa kufanyika ni serikali kujenga uwezo wa watu wetu kwenye maarifa na baadaye mitaji ili waweze kupambana vema kwenye uchumi wa dunia. Mambo ya harakati dhidi ya magharibi kwa mtindo wa upigania uhuru hayana tija na ni kujidanganya. Kwa sasa kinachoweza kutusaidia ni diplomasia na intelijensia ya kiuchumi.

CHINA HANA HURUMA, MAGHARIBI HAINA HURUMA
 
Achana nae huyu Babu kijana fikra za kijamaa zimemharibu akili

Ubongo wake unadhani mpaka Leo Moscow Ipo

USSR

Kumbe ilishatoka huko kitambo

Leo inaitwa Russia!
 
Tunawahitaji kama wabia wa maendeleo. Tunahitaji kufanya nao biashara, tunahitaji misaada yao, tunahitaji uwekezaji wao. Katika yote hiyo hatuwezi kujidanganya kuwa watafanya kwa masilahi yetu
Mara kadhaa huyu Humphrey ameshawahi onyesha hadharani jinsi akili yake ilivyoshindwa kuona mbali na kuwa na mawazo mgando. Most of frim in China are from western country, mazingira ya uwekezaji china ni maxuri mnoo.

Huyu jamaa niliona ni chenga pale alipoongelea juu ya chanjo ya covid !!!! Ni aibu kubwa sana
 
Mwambie huyo Mjinga sijui polepole angalia sasa CHINA anayo isifia sn imeendelea wakati huu wa sasa wanavyo hangaika watu wanavyo poteza ajira DUNIA imeshaishutukia CHINA kwani makampuni mengi ya Western countries pamoja na Japan na South Korea wameanza kuondoa viwanda vyao CHINA.

Kama huwaelewi wa China vizuri nenda kaishi huko kwao kwa muda ndio utawajuwa vizuri hawa watu ni AJABU SANA kuna miradi huko ni FAKE tupu ubora ni Zero na kunarushwa ya kufa Mtu .....as long una GOD FATHER kwenye chama Chao hicho cha CCP basi.
 
Huwa nashindwa kuelewa watu wakiwa nje ya selikari wanakuwa na madini sana mtakumbuka huyo polepole akiwa nje ya mfumo akina bashe nk huyu mtoa mada ameongea kisayansi yani daa
 
Dunia inapohitaji dhahabu huwezi kuigomea kwakuwa kanuni ya kiuchumi ni kwamba rasilimali zitaenda kule zinakohitajika. Ili kushindana katika rasilimali ni lazima ujenge uwezo wa ndani katika matumizi ya rasilimali. Vinginevyo hautazuia watu wa nje kuzitumia.
Nilitaka kukuelewa ila hapo umechemka, hapo hapo kwenye hiyo kanuni ya uchumi kuna kitu tunasema kama unazalisha kile kisichozalishwa na mwingine basi tumia fulsa hiyo kufanya thamani ya mali yako iwe yenye thamani hata kuizuia ili thamani isiyumbe.

👉🏾Mf. Una binti mrembo na ana heshima, umemlisha thamani yake na akakubali ila kila kijana akipita anaondoka naye vipi thamani itakuwaje?.
 
Sawa umejibu hoja za polepole. Ila Mimi nasimama na Polepole na ninaona wewe ndio umeandika bila uelewa thabiti kwa kiasi kikubwa.
 
Nilitaka kukuelewa ila hapo umechemka, hapo hapo kwenye hiyo kanuni ya uchumi kuna kitu tunasema kama unazalisha kile kisichozalishwa na mwingine basi tumia fulsa hiyo kufanya thamani ya mali yako iwe yenye thamani hata kuizuia ili thamani isiyumbe.

👉🏾Mf. Una binti mrembo na ana heshima, umemlisha thamani yake na akakubali ila kila kijana akipita anaondoka naye vipi thamani itakuwaje?.
Ni kweli unachosema lakini unakuwa na nguvu pale tu unapojitegemea. Sisi hatujafika kiwango cha kujitegemea nakuwa na nguvu ya kuwa na kiburi. tunahitaji vitu vingi toka kwa wenzetu. Kama misaada inavyohitajika kuja kwetu basi na dhahabu zinahitaji kwenda zinakotakiwa duniani. Huo ni utaratibu wa kawaida kabisa. hakuna haja ya kuwa na hasira. mpaka tutakapojitegemea kimaarifa na rasilimali.
 
Sawa umejibu hoja za polepole. Ila Mimi nasimama na Polepole na ninaona wewe ndio umeandika bila uelewa thabiti kwa kiasi kikubwa.
Nakupata lakini jua tu kuwa sijaamua kuzungumza kama mwanasiasa. Nimejibidisha sana kusoma historia za nchi mbalimbali kiuchumi. Nchi zote zimeendelea kwa namna moja tu ambayo sisi hatutaki kuifuata. Soma Japan ilivyoweza kuwa kinara wa automobiles mbele ya watu walioanzisha technolojia hiyo. Soma historia ya uchumi wa China ambayo kwakweli ni ya juzi tu. Utajua mengi.
 
Back
Top Bottom