SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,151
- 7,918
Kuna dalili mbaya toka pre-season hadi jana kwenye Simba Day nimeshaaza kuziona zinazoashiria kuwa Simba inaenda kuwa na msimu mbaya sana.
1. Tukirudi nyuma mwishoni mwa msimu uliopita, kipa Aishi Manula aliumia na kwa sababu za kijinga kabisa Beno Kakolanya, kipa mwenye uwezo akawa anakaa benchi tena katika mechi kubwa na muhimu sana. Hili tumelizungumza sana na nadhani kuna uzi nilishawahi kuuleta. Cha ajabu zaidi, inaonyesha hakuna juhudi zilizokuwa zinafanyika kutafuta kipa mbadala ili kipindi cha usajili kikifika asajiliwe, matokeo yake tumekuja kuokota kipa wa KMC dakika za lala salama.
2. Pre-season baadhi ya wachezaji kucheleweshwa kupelekwa kambini bila sababu za msingi. Baadhi ya wachezaji wapya walikuwa wanazungushwa kwenye matukio hapo Dar wakati wenzao wako kambini na wengine kina Chama na Baleke walichelewa kupelekwa kambini bila sababu za kueleweka. Hapo hapo inasemekana kocha alienda kwenye kozi fupi kwao Brazil (na kama wiki moja kabla alikuwa huko huko Brazil). Kimsingi timu imefanya mazoezi ya pre-season ya pamoja ya labda wiki moja tu.
3. Kwanini timu imejaza mawinga na kuzembea kusajili kiungo mkabaji na beki wa kushoto mbadala wa Zimbwe? Msimu uliopita niliona Simba imefululiza kusajili wachezaji wafupi kwa mkupuo. Nilibaki najiuliza huyu anayefanya usajili ana nia gani, hili halioni au ni makusudi haya? Msimu huu tumebadili gia, tumejaza mawinga, unajiuliza nia ni nini? Ukiangalia mechi ya jana dhidi ya Power Dynamos, utaona shida ya toka msimu uliopita pale eneo la kati ipo pale pale na hili litaisumbua sana Simba. Kuna wakati nilishauri Israel Mwenda ajaribiwe beki wa kushoto na kweli Simba ikatembea na ushauri huo lakini ukiangalia zile mechi alizochezeshwa nafasi hiyo kama ile na Coastal Union bado hakuwa comfortable kucheza upande ule. Ni sawa kumtumia hivyo kwenye dharura ila kwenye dirisha la usajili kulikuwa na nafasi ya kusajili mtu ambaye anaweza kucheza hiyo nafasi kwa ufanisi.
4. Kuendelea kumkumbatia Bocco. Kama mpira ni burudani, mimi siburudiki nikimuona Bocco akiwa uwanjani anachezea Simba hasa ukizingatia wachezaji wenye viwango, uwezo na ambao uchezaji wao unavutia na wanakupa matokeo kama Moses Phiri wapo wanasugua benchi. Mimi naamini Robertinho bado ni kocha mzuri sana na siyo yeye anayemkumbatia Bocco, naamini anafuata amri anayopewa kutoka juu yanayombeba Bocco na yanayompiga pini Phiri. Simba isitegemee mafanikio yoyote ya ndani au nje kwa kumtumia Bocco katika zama hizi. Ni misimu mingapi Simba imekwama na kugotea Robo huko CAF kisa mapungufu ya hawa kina Bocco, kwa nini wahusika hawajifunzi?
Nadhani kuna watu pale kwenye uongozi ndani ya Simba hawana mapenzi ya dhati na timu. Wameshikilia dhamana ya kuwapa furaha wanasimba ila pia wamejiandaa kuitumia dhamana hiyo kuwaumiza kwa maksudi kabisa wanasimba kwa sababu wanazozijua wao wenyewe.
Yanga wana timu ya kawaida mno msimu huu ila pamoja na hilo kwa ninachokiona kinaendelea pale Simba, Yanga watakuwa na mafanikio msimu huu kuizidi Simba.
Nawasilisha.