Naionya China, isijaribu

Naionya China, isijaribu

Yaani wabongo bana😂😂😂, unakaa nchi ya ulimwengu wa tatu, kwenye dampo la dunia, unajitia kuwashauri viongozi na serikali ya Russia na China yenye agents hatari wanayoijua hii dunia?
Umekula ugali wako na muhogo umeshiba unakuja kudhani una ijua kesho ya Russia kuliko FSB? Raisi tu wa Russia ni former KGB, serikali ya Ukraine ina agents wengi tu wana leak data...

Unaijua China kuliko MSS? Chinese wana puppets wengi tu serikali ya Taiwan, tunajua machache sana...

Russia wanajua walifanyalo, walishajiandaa, kila kitu kipo calculated...

Kama umeshiba ugali better ukae chini ufuatilie bifu ya Harmonize na Diamond na udaku wa insta, huwezi ijua China au Russia kama agents wao ambao hawalali, wana risk afya zao na maisha yao, wamesomea ukachero na wanaishi ukachero na wanakula kikachero hata mapenzi ni kikachero, wakipumua ni ukachero... Ogopa sana hio...

Kwamba Russia imeingia mtegoni😂😂😂, Huyo ni mbongo, hivi vile vichwa vyote vya wale wazee pale Moscow vyenye mvi, makachero wabobezi toka USSR hawakujua plans za US?😂😂

Inaskitisha sana kwa kweli..
Well said, nilicho kuja kubaini kutoka kwa wachangiaji walio wengi ni kwamba exposure ina matter sana sana, yaani yeyote ambaye ni broad minded akipitia maelezo/ufafanuzi wako unaonekana wewe ni mwelewa sana katika masuala haya ya Geopolitical tug of war kati ya Western Nations specifically the US na Urusi na kwa
 
Shida iliyopo US wanategemea bidhaa za china, kuanzia chupi hadi mitambo,, sababu viwanda vilihamia china kukwepa gharama za uzalishaji marekani,
Mchina anamtegemea mmarekani zaidi ya mmarekani anavyomtegemea mchina. Ndo maana mara kwa mara mmarekani humuwekea vikwazo mchina na mchina huonekana kutaka wakae chini na mmarekani ili wayamalize.
 
Marekan bado ataendelea kuwa super power kwa sababu ana nguvu kubwa mno za kijeshi, uchumi mkubwa na imara zaidi, ana uwezo wa kutengeneza maadui karibu na mipaka ya adui yake ili awatumie hao maadui ku deal na ww kijeshi na kisaikolojia kama tunavyoona alivyomtengeneza adui wa Russia (Ukraine) na adui wa China (Taiwan) nk.
Na uzuri ni kwamba anawatumia ipasavyo Hawa maadui wa maadui wake,uko Ukraine inaonekana kafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana
 
Hahaha China huko anachokifanya!
Hii ngoma ikuendelea hivi Taiwan na US watapoteza zaidi.
Marekani watapoteza zaidi kivipi na wakati vita sio yake na haipiganiwi mlangoni kwake? Yeye atachofanya ni kuchochea vita ili auze silaha zaidi na wakati huo china itakuwa imedhoofika kwa kupoteza wanajeshi kibao, silaha na uchumi wake kuanguka kutokana na vikwazo vya wababe wa dunia ya kwanza. Usisahau china anauza bidhaa zake za maana zaidi katika nchi za ulaya haswa west countries na marekani. Kwahiyo hao wakimuwekea vikwazo, jumlisha upotevu atakaupata kupitia vita hivyo, basi kwisha habari yake. Marekani wanamtekenya tekenya kusudi aingie ulingoni aangushe uchumi wake na nguvu zake.
 
Attachments

  • Screenshot_20220805-154322.jpg
    Screenshot_20220805-154322.jpg
    69.5 KB · Views: 19
Marekani watapoteza zaidi kivipi na wakati vita sio yake na haipiganiwi mlangoni kwake? Yeye atachofanya ni kuchochea vita ili auze silaha zaidi na wakati huo china itakuwa imedhoofika kwa kupoteza wanajeshi kibao, silaha na uchumi wake kuanguka kutokana na vikwazo vya wababe wa dunia ya kwanza. Usisahau china anauza bidhaa zake za maana zaidi katika nchi za ulaya haswa west countries na marekani. Kwahiyo hao wakimuwekea vikwazo, jumlisha upotevu atakaupata kupitia vita hivyo, basi kwisha habari yake. Marekani wanamtekenya tekenya kusudi aingie ulingoni aangushe uchumi wake na nguvu zake.
Vizuri.

Tuusubiri wakati utafafanua zaidi.
 
Tujikumbushe kwanza Uchina kama sikosei karibia zaidi ya mara tatu ilijaribu kuivamia Taiwan. Hata pia kwa Taiwan kutaka kufanya mpango wa kurudisha utawala wake Uchina kupitia mpango wa Project National Glory.
Mfano upo mgogoro wa mwaka 1954 ambao ulikuwa mkubwa kiasi kwamba Marekani ilitoa onyo la kutumia mabomu ya Nuclear kama utawala wa Mao Zedong utajaribu kuivamia Taiwan hali iliyomfanya Uchina atulie kwa muda kujitathmini upya. Pitia Taiwan strait crisis 1, 2 na 3.

Hivyo kijana mpango wa Uchina kuivamia Taiwan upo pale pale either through diplomatic process or through armed means, kinachomkwamisha Uchina ni uwepo wa Super Power wa Dunia pale Taiwan ambapo kuwepo kwa Taiwan kunamfanya Marekani aweze kum contain Uchina katika eneo la Pacific ya mbali akisaidiwa na Korea Kusini na Japan.
Uzuri ulijitokeza pale Uchina alipoweza kujitahidi kumtengeneza Communist Ally North Korea la sivyo angekuwa amezingirwa pakubwa sana (Wataalamu wanaelewa hapa madhara ya kuzingwa na adui, ndivyo alivyofanya Urusi baada kuona Ukraine inataka kujiunga NATO).
Katika kila namna Uchina itajaribu kila njia kuichukua Taiwan ila uwepo wa US pale ni nightmare kwa Taifa hilo kwa sababu mbalimbali kama vile uchumi na hali ya usalama maeneo ya Far East itakayo mwarhiri yeye vilevile. Wasalam.
Wewe Sasa ndio umeongea kitaalamu na kisomi zaidi👍
 
Mimi kwa maoni yangu naona China kwa Sasa inamuhitaji Rais mwenye kaliba ya Chairman Mao Zedong ili kukamilisha mission ya Taiwan Unification.
 
1
Hamjambo wakuu.

Ndugu wana Jamii Forum baada ya kufuatilia kile kinachoendelea kutokea kule katika mpaka wa kisiwa cha Taiwan, kuhusu mzozo wa China na Taiwan.

Kama ningekuwa na uwezo wa kuwasiliana na uongozi wa China, basi ushauri wangu mkubwa kwao ingekuwa ni kuwaambia wasithubutu kukivamia kisiwa kile.

Ule ni mtego uliotegwa na hawa wababe wa dunia wakiongozwa na baba lao USA.

Ikumbukwe kwamba hata vita ya Ukraine na Russia ilianza hivi hivi, huku Russia ikiwa na uhakika wa kuisambaratisha Ukraine kwa muda wa siku 3 tu au ikichelewa sana ni week. Sasa kinachoendelea leo kila mtu anakiona.

Russia imekuwa ikitumia kila aina ya njia za kijeshi, rasilimali, na jeshi lake la akiba kuimaliza vita hiyo lkn inashindikana.

Leo hii Russia ishatumia kiasi kikubwa cha silaha zake, ishapoteza kiasi kikubwa cha wanajeshi wake, ishayumbisha uchumi wake na kushuka thamani kwa hela yake (na hili ndio USA na nchi zingine za NATO walilitaka) bila kufanikiwa kuiangusha Serikali ya Ukraine wala kuuteka mji mkuu.

Kile kinachoendelea sasa hivi kimetokana na uzembe wa Putin na serikali yake, sasa wanaona yamekuwa magumu kwao, zile siku 3 ikawa week, ile week ikawa mwezi, mwezi sasa imekuwa miezi.

Na kila wanavyoendelea na vita na ndio jinsi wanavyoendelea kupata hasara kwa kupoteza askari, silaha mbalimbali za kijeshi na kudhoofisha uchumi wao.

Na wamarekani wakishirikiana na ndugu zao wa West wataendelea kuijambisha Russia kwa kujifanya wanaitumia Ukraine silaha (japo nyingi ni za kichovu) ili kuichochea Russia izidi kuendeleza mashambulizi na kudhoofisha nguvu zake kwa miaka kadhaa ijayo.

Ni nani kati ya wana NATO asiejua madhara ya kuingia vitani mzimamzima. Leo hii marekani haiwezi kuthubutu kuingia vitani hata na Mexico, japo kijeshi inaweza kutumia hata jeshi lake lililo katika jimbo la California tu kuisambaratisha Mexico, lakn wanaangalia hasara ambayo inaweza kuipata katika vita hiyo.

Marekani inaweza kutuma silaha au vijana wake kadhaa wa jeshi kwenda kusaidia sehem fulan kwa ajili ya masilahi ya marekani ila haiwezi kuingia vitani moja kwa moja kama ilivyofanya Russia.

Ni mara ngapi Iran imekuwa ikiangamiza ndege zisizo na rubani za Marekani, kuzilipua meli za Marekani na pengine kuteka hata meli za washirika hao wa Marekani, lakn kamwe Marekani haikufikiria na haifikirii kuingia vitani, maana inaelewa kuwa vita kuianza ni vyepesi sana lakin kuimaliza ni vigumu.

Sasa inashangaza kuona China pamoja na kuwa na wasomi wengi pamoja na intelejensi kubwa duniani, lakin inataka kuingia mtegoni kama alivyoingia ndugu yake Russia. USA na swaiba zake wana uwezo wa kutoa msaada kwa Taiwan au Ukraine kwa miaka kumi ili mradi lengo lao litimie.
Marekani na swaiba zake sio wajinga, wanajua vizuri kile wanachokifanya.

Na majibu kuhusu uchumi wa Russia na nguvu zake za kijeshi tutayapata baadae baada ya vita kuisha. Kwa sasa bado inachochewa chochewa ili iweze kutumia hata zile silaha ambazo ingetakiwa kutumia pale inapopambana na nchi kubwa kama USA, China, India nk.
Mwisho wa siku ghala la silaha litabaki tupu.

So naionya China kama inataka kuendelea kuwa nchi ya pili kwa uchumi na ya tatu kwa nguvu za kijeshi, basi iachane na wazo la kuivamia Taiwan maana itapoteza nafasi zake zote mbili, kuanzia kwenye uchumi hadi jeshi. Vikwazo itakavyowekewa na wakubwa hao wa dunia vitakuwa sio vya dunia hii, na hapo ndipo atakapoanza kuona madhara ya kuingia vitani kichwa kichwa bila kutumia akili.
 
Na uzuri ni kwamba anawatumia ipasavyo Hawa maadui wa maadui wake,uko Ukraine inaonekana kafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana
Ya ashafanikiwa kwa 80%. Ebu angalia jinsi Russia ilivyozungukwa na maadui waliotengenezwa na Marekani kwa kigezo cha NATO
 
Attachments

  • Screenshot_20220805-183223.jpg
    Screenshot_20220805-183223.jpg
    44.5 KB · Views: 21
Mm nampinga sana Putin kuivamia Ukraine ila siamini kuwa Puttin ni mjinga mjinga. So far kuna mambo mengi ameshaprove kuwa he is smart kwa kiwango cha USA na washirika kutokukurupuka anapodeal naye.

Huenda mtego upo kwenye muda kama unavyosema na kuna member mmoja alishasema Puttin atapigana muda mrefu sana na ni makosa kufikiri atachukua nchi kwa haraka Nyamizi na ni kweli yametokea.

Ila nasema sio mjinga kwa sababu mpaka kufikia sasa ameonyesha kuwa ni smart enough to play along with USA and NATO games. Fuel prices zimekuwa unstable, Food imebidi wakubaliane meli ziachiwe, kuna vikwazo imebidi kuwe na exceptions baadhi ya nchi na hapo ni yeye mwenyewe. Imagine angekuwa na saport ya moja kwa moja ya nchi kama China, Iran, India n.k na wakaamua kusimama nae.

Pamoja na mm kutomtakia mema huyu Puttin huko Ukraine, (Nataka ashindwe awaachie watu nchi yao, kama kuna changamoto diplomacy itumike au njia mbadala za kudeal na mgogoro) lazima tu kukubali kuwa nchi anayoiongoza inahitajika na so far ameonyesha kuhitajika kwake duniani.
 
Tujikumbushe kwanza Uchina kama sikosei karibia zaidi ya mara tatu ilijaribu kuivamia Taiwan. Hata pia kwa Taiwan kutaka kufanya mpango wa kurudisha utawala wake Uchina kupitia mpango wa Project National Glory.
Mfano upo mgogoro wa mwaka 1954 ambao ulikuwa mkubwa kiasi kwamba Marekani ilitoa onyo la kutumia mabomu ya Nuclear kama utawala wa Mao Zedong utajaribu kuivamia Taiwan hali iliyomfanya Uchina atulie kwa muda kujitathmini upya. Pitia Taiwan strait crisis 1, 2 na 3.

Hivyo kijana mpango wa Uchina kuivamia Taiwan upo pale pale either through diplomatic process or through armed means, kinachomkwamisha Uchina ni uwepo wa Super Power wa Dunia pale Taiwan ambapo kuwepo kwa Taiwan kunamfanya Marekani aweze kum contain Uchina katika eneo la Pacific ya mbali akisaidiwa na Korea Kusini na Japan.
Uzuri ulijitokeza pale Uchina alipoweza kujitahidi kumtengeneza Communist Ally North Korea la sivyo angekuwa amezingirwa pakubwa sana (Wataalamu wanaelewa hapa madhara ya kuzingwa na adui, ndivyo alivyofanya Urusi baada kuona Ukraine inataka kujiunga NATO).
Katika kila namna Uchina itajaribu kila njia kuichukua Taiwan ila uwepo wa US pale ni nightmare kwa Taifa hilo kwa sababu mbalimbali kama vile uchumi na hali ya usalama maeneo ya Far East itakayo mwarhiri yeye vilevile. Wasalam.
Swala la kuzuia kuzingirwa na adui tayari Russia ishachelewa. Kwa sasa ishazingirwa pakubwa sana, japo kwa huyu mmoja (Ukraine) ndio kajitahidi kuzuia.
 
Attachments

  • Screenshot_20220805-183223.jpg
    Screenshot_20220805-183223.jpg
    44.5 KB · Views: 18
Back
Top Bottom