In terms of military technology, Russia na China ni za kawaida tu. Na hii imekuja baada ya sote kushuhudia mbungi ya hapo Ukraine.
Tumeshaona namna mambo halivyobana kwa Russia, ametumia Hypersonic Missiles, Laser Weapons, Jets za kisasa n.k na bado vyote hivi havijaweza kufua dafu kama alivyotarajia.
Sasa je, China yeye tec yake itafua dafu huko Taiwan? Russia alitegemea huu mwiba angekaa nao kwa mwezi wa sita sasa? If hakutegemea, Je China ina uhakika gani wa kutumia muda mfupi wa vita hiyo akitaka kuanzisha?
Wakati vita vinaanza, China alitoa msaada kwa waathirika wa Ukraine. Huu ni usaliti mzito mno kwa best yake Russia. China leo akiingia Taiwan, Russia atamuunga mkono kinafki mno China kutokana na sababu mbili, moja ni ile ya yeye kuwa bado ana mwiba wake ambao ni Ukraine. Na mbili ni usaliti wa China kwa Russia.
Japan, India n.k nahisi wao watakuwa na hamu kubwa mno ya kutaka China aingie hapo Taiwan. Tukumbuke pia, endapo Taiwan ikamtikisa vyema China, kuna uwezekano maeneo mengine ya china yakataka kujitenga na China kama Hong Kong n.k
Wakati naandika hii comment kuna kitu hapa nakifkiria mkuu, hivi sio kwamba pengine CIA walipanga Russia apate vita yoyote ya kumsumbua ili ikitokea Vita ya China na Taiwan basi Russia asipate nguvu ya kumtetea China?