Naileta kwenu: hosts file kwa ajili ya ad-blocking!

Naileta kwenu: hosts file kwa ajili ya ad-blocking!

Habari Wakuu?

Nimetengeneza hosts file kutoka vyanzo/sources mbalimbali na nitakuwa nai-update mara kwa mara!
Pakueni hiyo hosts file kupitia 1hosts.cf!

Hizi ni baadhi ya apps ambazo unaweza kuzitumia kufanikisha adblocking kupitia hiyo hosts file.
Android:- DNS66 / AdAway / NetGuard
Windows:-uBlock Origin

Kwenye Android, kama simu yako iko rooted unaweza kuitumia hiyo hosts file + Adguard kwa wakati mmoja!


Wana-tech nyote karibuni!
CC: Chief-Mkwawa, Damushin, elmagnifico
Safi sana mkuu yani haya sasa ndiyo mambo mazuri siyo kila day tutumie vya wahindi...
 
Je!Hii adguard mpaka simu iwe rooted au hata ambayo haiko rooted
 
Mkuu Nijuze Kidogo Kuhusu Hiyo Kitu
Kila website ina IP address yake.

Hosts file ni text file ambayo kazi yake ni ku-redirect websites fulani kwenda IP addresses fulani (kwa lugha nyepesi).
Mfano:-
104.25.213.115 jamiiforums.com

Hivyo,
Kwenye hosts file uki-redirect Jamiiforums.com kwenda 185.60.219.35 instead of IP yake i.e 104.25.213.115, basi kila uandikapo Jamiiforums.com kwenye browser na ku-bofya "ENTER" utajikuta unapelekwa Fesibuku!
Mfano:-
185.60.219.35 jamiiforums.com

Tukija kwenye ku-block matangazo/ads, kwenye hosts file huwa tuna-redirect list ya websites ambazo ndizo zenye kuleta hayo matangazo kwenda IP address "0.0.0.0".

0.0.0.0 itaifanya hiyo website ya matangazo isipatikane/isiji-load pindi ukiperuzi websites mbalimbali.

Umenisoma, Mkuu?
 
Hongera mkuu kwa kazi nzuri sana..... Iko poa.
 
Hongera mkuu kwa kazi nzuri sana..... Iko poa.
Ikitokea ukakutana na website yeyote iliyokuwa blocked kimakosa kupitia hiyo hosts file usisite kunijulisha, Mkuu!

Ahsante kwa mrejesho wako!
 
Safii sana mkuu adguard iko vzur
Kama simu yako iko rooted ukitumia AdAway (kupitia hiyo hosts file) + Adguard inakuwa poa zaidi!

Advanced users, najiribuni hii coz ina-save RAM & CPU.
 
Back
Top Bottom