Naichukia sana CCM, naombeni msaada wa kisaikolojia

Msukuma Original

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
928
3,330
Mwenzenu kila nikisikia neno CCM napata kichefuchefu. Nikiona mtu kavaa nguo za CCM huwa nahisi kutapika. Nikisikia mtu anaongea kwa kuonyesha kuipenda CCM huwa naziba masikio, kama nipo kwenye daladala huwa nashuka kituo kinachofuata hata kama kituo changu cha kushukia hakijafika ili nisiendelee kusikia neno CCM.

Kuna huyu mwana CCM anayetuambia tuhamie Burundi namchukia huyu mtu. Hivi hakuna dawa ya kumroga maisha yake yaharibike kabisa halafu yeye ndio ahamie Burundi? CCM naichukia halafu huyu anatuambia kwa dharau tuhamie Burundi utadhani Tanzania ni nyumbani kwakwe na sisi wengine katukaribisha kwakwe hivyo keshatuchoka anatufukuza.

Naombeni msaada wa kisaikolojia nadhani chuki niliyonayo dhidi ya CCM inaweza kunifanya nijinyonge ili nisiendelee kuisikia CCM au kukejeliwa na viongozi wa CCM, yaani nahisi bora nife kuliko kuishi nadharaulika kwenye nchi yangu.

Kule Bungeni nikifikiria wabunge wote ni wa CCM huwa nakaribia kupasuka kwa hasira. Kuiondoa CCM madarakani haiwezekani maana haiheshimu maoni yetu kwenye sanduku la kura kwa kusaidiwa na vyombo vya dola, CCM naichukia zaidi hata ya neno lenyewe. Kama hii chuki ni ugonjwa naombeni msaada kabla sijajipoteza mwenyewe badala ya kuipoteza CCM.
 
Sawa mkuu. Naomba msaada wa kisaikolojia.

shida sio msaada ila unaendekeza sana siasa! kila kitu unakichukulia personal, Mtaji wa siasa na media ni uoga, wanapenda watu kma nyie ambao mkiepewa headlines zenye herufi kubwa sana mnapanic

Nikupe mfano:
1626817417161.png

- Hutakaa uskie media inasema watu mil 175 wamepona corona ila hao Mil 4 watatengenezewa headlines mpaka ukome

-- Pia uchumi sio mbaya kama unavoaminishwa, hakuna sku kutakua hakuna mzunguko wa ela kwa sababu wanaochapisha pesa ndo hao hao wanachukua kodi, hii ni mifano michache ila usiendekeze siasa sana na media shirikisha akili pia, hata hao unaowaona nafuu wakina mbowe wote ni ccm, wakina lissu wote! Nani alisifiwa chadema kama halima mdee? yupo wap saaahv?

- kuna wengine hawa apa
1626817676696.png


Ushauri wangu kwako ni
1) Fanya kazi, jali zaidi uzao wako pamoja na familia yako
2) Hakikisha unaweka mazingira mazuri kwa watoto wako, kama ni shule kama ni ubunifu wajengee uwezo wa kipekee
3) Kama una watoto unatoa wap mda wa siasa?
5) Umiza kichwa katika mambo yenye manufaa mfano kujaribu biashara tafauti, kushirikiana na watu katika miradi na mawazo mapya
6) Epuka wimbi la motisha kwenye siasa haswa wanaotumia jina la vijana
7) Hakikisha akaunti yako pia imenona hayo mengine ni yale yale kutengeneza tataizo alafu kulitatua mwenyewe
 
Mwenzenu kila nikisikia neno CCM napata kichefuchefu. Nikiona mtu kavaa nguo za CCM huwa nahisi kutapika. Nikisikia mtu anaongea kwa kuonyesha kuipenda CCM huwa naziba masikio, kama nipo kwenye daladala huwa nashuka kituo kinachofuata hata kama kituo changu cha kushukia hakijafika ili nisiendelee kusikia neno CCM...
Watanzania wengi 60% wanaichukia sana. Ni vile tu inalindwa na mabomu na mitutu hawana la kufanya
 
Mwenzenu kila nikisikia neno CCM napata kichefuchefu. Nikiona mtu kavaa nguo za CCM huwa nahisi kutapika. Nikisikia mtu anaongea kwa kuonyesha kuipenda CCM huwa naziba masikio, kama nipo kwenye daladala huwa nashuka kituo kinachofuata hata kama kituo changu cha kushukia hakijafika ili nisiendelee kusikia neno CCM...
Wewe umeambiwa na MWENYE NCHI Mwigulu rudi kwenu Burundi sasa kwanini ufie nchi jirani kwa kinyongo wakati kwenu Burundi kupo?
 
KWELI na POLe
Kama baba wataifa kwamdomo wake aliwa tamka ccm sio mama yake ,wewe sijui nikushaurije ila Fanya haya
Jikite kufanya kazizako kwasasa mudamwingi kama pana ng'ombe kachunge ukirudi umechoka unaoga unalala
 
Mwenzenu kila nikisikia neno CCM napata kichefuchefu. Nikiona mtu kavaa nguo za CCM huwa nahisi kutapika. Nikisikia mtu anaongea kwa kuonyesha kuipenda CCM huwa naziba masikio, kama nipo kwenye daladala huwa nashuka kituo kinachofuata hata kama kituo changu cha kushukia hakijafika ili nisiendelee kusikia neno CCM...
Mwone Polepole
 
shida sio msaada ila unaendekeza sana siasa! kila kitu unakichukulia personal, Mtaji wa siasa na media ni uoga, wanapenda watu kma nyie ambao mkiepewa headlines zenye herufi kubwa sana mnapanic....
Ndugu mtoa mada coment hii inaweza kukusaidia kutibu taitzo lako kama utafungua moyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom