Naibu Waziri wa Nishati: Mgawo wa umeme nchini utaisha mwezi wa tatu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,820
4,572

Mradi wa umeme wa Julius Nyerere ni moja ya mradi unaotekelezeka kwa weledi mkubwa sana, sote tunajua mwezi wa sita mwaka huu ndiyo tulitegemea kuwasha mtambio namba 9 kwa mara ya kwanza lakini kwa jitihada za serikali na wakandarasi tuliweza kusogeza ratiba za kuwasha mtambo huu hadi mwezi wa pili, jana tumefanikiwa kufanya majaribio kwa ukamilifu kwenye mtambo namba 9 na tumeutembeza kwenye uwezo wake wa mwisho wa megawati 235," - Judith Kapinga, Naibu Waziri wa Nishati.

"Tuliahidi mwezi huu tuna ratiba ya kuzindua mtambo huu na ratiba hii iko palepale, tunawashukuru sana Watanzania kwa kuendelea kutuvumilia, matumizi ya umeme yanategemeana tukizalisha mwezi huu mgao utakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa kwa sababu tunazalisha megawati 235 na mwezi wa tatu tutazalisha megawati 235 hivyo zitakuwa megawati 470 uhakika ni kwamba kufikia mwezi wa tatu mgao wa umeme utaisha nchini," - Judith Kapinga, Naibu Waziri wa Nishati.


==========For English Audience Only===========
Announcing an end to power rationing in the country, the Deputy Minister of Energy declared that the third month would mark the conclusion of the long-standing issue.

"The Julius Nyerere power project is one of the projects being executed with great professionalism. We all know that we were expecting to commission turbine number 9 in June this year, but through the efforts of the government and contractors, we were able to adjust the schedule to commission this turbine in February. Yesterday, we successfully conducted comprehensive tests on turbine number 9 and pushed it to its final capacity of 235 megawatts," stated Judith Kapinga, Deputy Minister of Energy.

She further added that"We promised to commission this turbine this month, and that schedule remains intact. We are very grateful to Tanzanians for their patience. Electricity usage depends on our production levels; this month, with 235 megawatts being generated, power rationing will significantly decrease. In the third month, we will produce another 235 megawatts, totaling 470 megawatts. By the third month, power rationing will be a thing of the past in the country,"

Pia soma
 

Huyu kama ndio aliyesema mgao utaisha February 16, 2024, hakupaswa kusogeza tena tarehe mbele, alitakiwa awe ameshajipima na kujiuzulu.

Viongozi wa kiafrika ni kama matapeli vile, hawawezi na hawapendi kuwajibika kwa kauli zao. Ikifika March atasogeza tena tarehe, subirini muone.
 

Mradi wa umeme wa Julius Nyerere ni moja ya mradi unaotekelezeka kwa weledi mkubwa sana, sote tunajua mwezi wa sita mwaka huu ndiyo tulitegemea kuwasha mtambio namba 9 kwa mara ya kwanza lakini kwa jitihada za serikali na

Pia soma
- Februari 16 Serikali ilisema umeme mwisho kukatika. Ulipo umeme upo?
JamiiForums555154368.jpg
 
Umeme si ulikuwepo kabla ya hilo Bwawa. Au tumehamishia matumaini kwenye Bwawa tena.

Wangerudisha ule wa kawaida uliokuwepo kwanza ili wa Bwawa ukija ni kuongezea tu. Maana nyingine sababu za mgao tulizonazo zibqki palepale. Au mimi ndio sijaelewa.​
 
Umeme si ulikuwepo kabla ya hilo Bwawa. Au tumehamishia matumaini kwenye Bwawa tena.

Wangerudisha ule wa kawaida uliokuwepo kwanza ili wa Bwawa ukija ni kuongezea tu. Maana nyingine sababu za mgao tulizonazo zibqki palepale. Au mimi ndio sijaelewa.​
Kila siku kuna watu wanaunganishwa kwenye gridi ya taifa.
Matumizi yanaongezeka.
Vyanzo vya mwanzo havitoshi tena.
 
Back
Top Bottom