Naibu Waziri Sagini azindua mfumo wa Kidigitali wa URA Mobile Money

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Jeshi la Polisi nchini limezindua Mfumo wa kidijitali wa huduma za kifedha uitwao (URA MOBILE MONEY) utakaotumika na Viongozi pia Wanachama wa URA SACCOS katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Jijini Dar es Salaam Leo Septemba 30, 2023.

Akizungumza katika hafla fupi ya Uzinduzi wa Mfumo huo Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini, amelipongeza Jeshi la Polisi nchini kwa kutambua umuhimu wa kuwa na huduma za kifedha zinazotolewa na kupatikana kwa gharama nafuu kwa Watumishi wake na hivyo kuanzisha Ushirika wa kuweka Akiba na Kukopa (SACCOS) miaka 17 iliyopita.

"Nafahamu kama ilivyoelezwa kwamba, tangu kuanzishwa kwa Ushirika huu Tarehe 6 Septemba 2006, na kuutambua katika Kanuni za Kudumu za Utendaji za Jeshi la Polisi (P.G.O 212) fursa mbalimbali zimetolewa kwa Watumishi kama vile uwekaji wa akiba na utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu ukilinganishwa na taasisi nyingine za kifedha," amesema Mhe. Sagini.

Pia amesema kuwa uwepo wa URA SACCOS kumechangia ustawi wa Watumishi kiuchumi, kurahisisha utendaji, kuongeza ufanisi katika kazi na kuongeza heshima kubwa kwa Watumishi wa Jeshi la Polisi kwa kuboresha maisha na kuwaepusha kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa pindi wanapokabiliwa na mahitaji ya kifedha kwa ajili ya maendeleo yao.

"Kwa kufanya hivi mmeunga mkono kwa vitendo juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, ambaye kwa nyakati tofauti amesisitiza kuwekeza kwenye matumizi ya Tehama katika utekelezaji wa majukumu ya Umma," amesema Mhe. Sagini.

Pia Naibu Waziri Sagini alimpongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, Bodi ya URA SACCOS na watendaji wa URA SACCOS kwa ubunifu, ueledi na umahiri wa kukivusha Chama kutoka kwenye mfumo wa analojia kwenda kwenye kidigitali kwa lengo la kuongeza uwazi na uwajibikaji.

Aidha URA SACCOS LTD ni miongoni mwa taasisi zenye kutoa mikopo yenye riba nafuu kuliko taasisi nyingine za kifedha lakini pia kutambua mafanikio muhimu yaliyopatikana katika Chama tokea kuanzishwa kwake mwezi Septemba 2006 ni kuongezeka kwa idadi kubwa ya wlWanachama wanaofikia 45,142 kufikia Juni 30, 2023 ikilinganishwa na Wanachama 4,300 waliojiunga mwaka 2006 chama kilipoanzishwa.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Back
Top Bottom