Naibu Waziri Sagini awataka wafungwa kumuomba Mungu ili wakitoka wakute wenza wao wako salama

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,331
12,952
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini (Mb) amewasisitiza wafungwa na mahabusu wanaotarajia kumaliza kutumikia adhabu zao Gerezani waongeze juhudi katika kumuomba Mungu ili wakirudi uraiani wakaanze maisha mapya ikiwa pamoja na wapenzi wao wakiwa salama.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukamilisha Ziara ya Siku mbili Mkoani Simiyu ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi ameeleza kuwa katika Gereza la Bariadi wafungwa na mahabusu Wanaume waliomba msamaha wa Rais ulegeze masharti ili watoke haraka wawahi wake zao kabla hawaja wasaliti.

"Wamenieleza kuwa lengo lao kuomba kulegezewa kwa masharti ya msamaha wa Rais ni kwamba watoke haraka wakutane na wake zao na mimi nikawaambia waendelee kumuomba Mungu wake zao wasitoke nje sababu wao wamefungiwa hivyo basi walioko majumbani watulie wawakute wakiwa salama," amesema Sagini.

Aidha amesema, wafungwa na mahabusu wamemtuma afikishe Salamu za Pongezi kwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mhandisi Hamad Masauni kwa juhudi za kuboresha mazingira ya mahabusu na magereza tofauti na ilivyokuwa hapo awali.


Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ACP Edith Swebe amemshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini kwa Ziara yake ya kikazi Mkoani humo na kuahidi kuyafanyia kazi kwa vitendo maagizo yote yaliyotolewa kwa utekelezaji.
 
Yaani nchi inaongozwa na mazombi matupu, hawa watu wanapataje uteuzi! Kila, kitu sasa hv suruhisho ni kuomba Mungu!

Hawa, ngedere, wanapotaka kuendesha ma V8 Yao huwa wanaanza, kupiga Dua mafuta yatokee kwenye tank, au huenda vituo vya mafuta na kujaza! Watu wapo jera, ushauri wako, ni, kuwataka "waombe Mungu" Matatizo Yao yayeyuke! Kenge kabisa, dunia na universe haiendi hivyo.

Dunia kuna kanuni zake,ni kazi, ya mikono,wapeni ujuzi, na ufundi,waweze kuishi kitaa, sio kuwataka wapige maombi!

Gwajima, jimboni kwake mitaa imejaa maji,amepiga magoti serikalini ijenge mitaro kwemda baharini, kwanini asipige maombi, maji yaende kimiujiza! He knows better, it doesn't work that way! Fuckers
 
Mkeo una lala nae kila siku na anakusaliti leo umefungwa miaka 3 afu kuna mtu anakuja kwambia uombe mungu mkeo asilazwe
 
Back
Top Bottom