Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,815
- 11,991
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukamilisha Ziara ya Siku mbili Mkoani Simiyu ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi ameeleza kuwa katika Gereza la Bariadi wafungwa na mahabusu Wanaume waliomba msamaha wa Rais ulegeze masharti ili watoke haraka wawahi wake zao kabla hawaja wasaliti.
Aidha amesema, wafungwa na mahabusu wamemtuma afikishe Salamu za Pongezi kwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mhandisi Hamad Masauni kwa juhudi za kuboresha mazingira ya mahabusu na magereza tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ACP Edith Swebe amemshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini kwa Ziara yake ya kikazi Mkoani humo na kuahidi kuyafanyia kazi kwa vitendo maagizo yote yaliyotolewa kwa utekelezaji.