Serikali Kuendelea Kuboresha Miundombinu ya Viwanja vya Ndege Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945
Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kujenga na kupanua Miundombinu ya Viwanja vya Ndege ili kujihakikishia utoaji wa huduma ndani ya nchi na nchi Jirani

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kwa kukagua upanuzi wa njia ya kuruka na kutua ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma.

Mkoani Kigoma, Kihenzile amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe .Dkt. Samia Suluhu Hassan inachukulia sekta ya Uchukuzi kwa njia ya anga kama mishipa ya ukuzaji uchumi na shughuli mbalimbali za utoaji huduma kwa wananchi ndani na nje ya nchi ndiyo maana imewekeza fedha nyingi kwenye maboresho, ukarabati na upanuzi wa viwanja vyetu vya ndege na ununuzi wa ndege kwa ujumla

"Uchukuzi kwa njia ya anga ni uchumi pia diplomasia, kadri unavyojenga na kuboresha viwanja vya ndege ndivyo unavyojenga ushawishi kwa jamii inayokuzunguka ndani na nje ya Nchi hivyo kuongeza watumiaji zaidi na mapato kwa maendeleo ya Nchi" - Mhe. David Kihenzile

Ameongeza kuwa kwa mantiki hiyo Serikali inajenga miundombinu ya viwanja vya Ndege nchini ili kulifanya taifa la Tanzania kuwa kubwa na lenye nguvu ya ushawishi kiuchumi kikanda na kimataifa.

Naibu Waziri Kihenzile amewataka Wakala wa barabara nchini TANROAD na Menejimenti ya Uwanja wa Ndege wa Kigoma kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi kumaliza upanuzi huo kwa wakati, kiwango stahiki na kutekeleza ahadi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wa Kigoma ya kuwapa ajira wakazi wa Mkoa wa Kigoma na kuimarisha miundombinu ya uchukuzi mkoani humo.

Akitoa maelezo ya awali Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma Bw. Mbura Daniel amesma kwa sasa Uwanja huo unahudumia abiria elfu 33 kwa mwezi na miruko 102 hadi 105 kwa mwezi

Amefafanua kuwa katika safari sita za juma, tatu kati yake zinahusisha safari za nje ya nchi hasa Burundi zikifanywa na shirika la ndege la taifa ATCL na kuongeza kuwa upanuzi wa Uwanja huo utahusisha njia ya kuruka na kutua Ndege kutoka mita 1,800 hadi 3,000, eneo la maegesho ya Ndege, mnara wa kuongozea na jengo la abiria huku ukitarajiwa kuhudumia abiria laki nne kwa mwaka na kuwekewa taa za kuongozea ndege ili utumike kwa masaa 24 huku ukipokea ndege kubwa zaidi.

WhatsApp Image 2023-11-29 at 14.35.19.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-29 at 14.35.20.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-29 at 14.35.20(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-29 at 14.35.20(2).jpeg
 
View attachment 2828627View attachment 2828628View attachment 2828629View attachment 2828630
Porojo za mdomoni nyingiiiiiii lakini vitendo ni Zero!! Yaani watawala wa Afrika!!?????
 
Back
Top Bottom