Kwa nini mwajiri wa Mulugo ndio wababaishaji kuliko hata Mulugo mwenyewe! Kwa nini boss wake hatoi tamko juu ya hii sintofahamu??????
Au Mulugo ana akili sana - taifa litakosa mchango wake kwenye wizara hii nyeti ya Elimu hasa kipindi hii ambacho wanahitaji mtu mwenye uwezo kama Mulugo kuweza kuwaondoa kwenye kitanzi cha kufeli!!!!!!!!1 Wizara ya Elimu ni kitovu cha Uzembe.
Katika hali ya mfumo wa Rais kuteua mawaziri kwa vigezo anavyojua yeye, sisi kama wananchi wa kawaida tunapaswa tu kujua hapo Mheshimwa Rais kuna fadhila anailipa kwa kumpa hiyo nafasi. Maana haingii akilini ni kwanini huyu bwana ha-step down au hasimiamishwi ili kupisha uchunguzi huru ufanyike kuhusu elimu yake. JK na Mulugo hawaoni ugumu uliopo katika kuupata ukweli iwapo Mulugo akiendelea kuwapo ofisini?? Je Mulugo haoni kama uwepo wake ofisin unawanyima nafasi watu walio chini ya ofisi yake hasa baraza la mitihani na wizara kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha katika kubaini ukweli. Yeye hatoona raha ukweli/utata juu ya elimu yake ukiwa cleared??
Aidha, nilitaka na yeye Mulugo afahamu kuwa muungwana msuli ukidondoka, hatimui mbio uchi. Badala yake anatakiwa kuchuchumaa na kuliokota. Anachokifanya sasa kulumbana kupitia magazeti ni kujichafua zaid, kama ana uhakika na elimu yake na mambo yake, si amuandikie tu Rais barua ya kumwomba akae nje ya huo unaibu waziri wa miezi kadhaa ili kupisha uchunguzi?? anaogopa nini kufanya hivyo?? si amesema anauhakika na mambo yake ya elimu???Haoni kuwa atapata credits zaid kama itakuwa proven yupo clean????? Haoni kuwa atafunga huu mjadala kwa mbwembwe???
Kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa last time baada ya Sugu kuibua hili sakata, Naibu Waziri Philipo Augustine Mulugo, Hamimu Hassan,
Hamimu Augustino, Dickson Mulungu (nadhan sijasahau jina) alipigiwa simu na mwandishi akasema kuwa yupo safarin na akifika ofisini basi atakuwa na wakati mzuri wa kulisemea hilo. Kwli hakujitokeza teeeeeeeeeeena hadi leo sakata hili lilipoibuka upya. Anavyosema kuwa ameshalijibia karibu mara 20, mbona kama napata shida kuelewa??? Kalijibu ndani ya mipaka ya nchi hii hii au kajibia wap na kamjibu nani?? Anadhan kama majibu yake yalieleweka kwann wananchi waendelee kumzonga???Lakini pia ubadilikaji wa hayo majina umeambatana na viapo vya mahakamani???
Kwako JK baada ya kuona mtu anaelimu ya kuvundika, kwann unamuacha aendelee kukaa katika wizara inayoongoza kwa kufanya vibaya??? Does it mean that huna uchungu na kuporomoka kwa kiwango cha Tanzania na kufail kwa watoto wetu wewe hakukuhusu?? Hivi kweli Mhe. hakuna mtu competent kuliko hawa waliorundikana kwenye hii wizara inayoongoza kwa ku underperform??? Nini mchango wa hawa mawaziri wako katika hii wizara??? Au huyu bwana ndiye mtaalamu na mshauri hadhimu wa Ndugu yako Kawambwa na bila huyu Kawambwa hawezi kukaa ofisin???
Maswali haya yakijibiwa na viongozi wa chama tawala ambao ni members humu yatanisaidia sana kuupa relief ubongo wangu kulingana na GB zilizobebwa na haya maswali in my brain/Hard Disk Drive.