Naibu Waziri Elimu katika kashfa vyeti

Huyu jamaa kweli IQ yake ni ndogo mno ijapo ana ujanjaujanja tu mdomoni na hii ndo shortcoming ya T.I.S.S kulala fofofo
 
Mimi namfahamu Mulugo, alinikuta pale shule na sisi (mimi na jamaa yangu) ndo tulikuwa marafiki zake wa karibu tena sana, nakumbuka tulikuwa tunamfundisha jinsi ya kuaandaa azimio la kazi na andalio la somo (scheme of work & lesson plan) maana alikuwa hajui lolote! Kimsingi, huyu mtu ni tapeli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
hata mi nakumbuka jina la mulungu akiwa meneja kama c mkurugenzi wa southern highland sasa ghafla nikasikia mulugo kwenye siasa...mmh tutafika kweli?
 
Sasa anaona aibu ya nini siajiuzulu tu jamani! kwani hajaona hali ya matokeo ilivyo mbaya mwaka huu ilihali chanzo kumbe ni yeye mwenyewe aliyeshindwa kujieleza nchi za watu.
 
Mtahangaika sana wana CDM.Hivi suala la Mulugo kuhusu jina liliisha tolewa maelezo lakini kwa sababu yeye ameahidi kumg'oa Sugu jimbol a mbeya 2015 mmeanza kutapata.Mwacheni apige kazi.Mbona jina la Wegesa tumeisha sahau?Fanyeni kazi acheni majungu.

haijalish ni mfuasa wa chama au lah,,,hapa kinachojadiliwa ni suala lake lina utata usidhan kila anayeponda huu uozo ni mwana chama wa chama fulan,ufafanuz unakujaje kwa majina zaid ya matatu?hebu tuwe siriaz jaman
 
Tuna Phd fake, lakinio mpaka leo ni wabunge.Je waziri wa fedha ana Phd toka wapi?
 
Mulugo ni sehemu tu ya Matatizo yaliyoko kwenye wateule wa nchi hii.Wako wengi na wengine.Niliwahi kuandika huko nyuma jinsi nilivyoshuhudia majigambo ya Mulugo wakati nasafiri naye nikiwa kiti cha mbele yake kwenye Basi la Sumry toka Mbeya kwenda Dodoma alipokuwa ameitwa kwa mjibu wake mwenyewe kupitia maongezi ya simu yake ya mkononi.Alikuwa akiwasaliana na marafiki zake kuwataarifu kuwa ameitwa Dodoma na wakubwa mara baada ya kupitishwa na jimbo lake kuwa Mbunge bila kupingwa.Ninaporudia kumbukumbu ile ya maongezi yake na haya yanayoandikwa na vyombo vya habari kwa kiasi kikubwa naamini kuna ukweli katika hili.
 
Gazeti limechelewa kwa Habari kama hii
JF walishaeleza kwa undani juu ya ujanja
wa Hamimu lakini kama ana God father

Mpaka sasa Mzee wa Tanganyika&Zimbabwe anapeta tu na per diem za Serikali
Hivi JK kama jf haingii lakini gazeti nalo
halioni jamani.

Hamimu Hassan aachie ngazi japo itauma.

Matokeo ya JF kujadili jambo hilo ndipo gazeti lilizinduka kwenda kufanya utafiti huo, halijachelewa kwa vile kutoa habari hiyo katika media iliyotukuka kwa waziri kunahitaji utafiti wa kujiridhisha kwanza.
 
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo anadaiwa kutumia ujanja katika wasifu na elimu yake ambapo katika maisha yake ya kielimu ametumia majina manne tofauti.
Philipo Augustine Mulugo ndiyo jina lake halisi ambalo alilisomea mpaka alipohitimu darasa la saba kwa mara ya kwanza 1988, lakini kutokana na kwamba hakufaulu kwenda sekondari alirudia darasa hilo.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwa takriban miezi mitatu sasa umebaini kuwa 1989, Mulugo alirudia darasa la saba katika Shule ya Msingi Rukwa ya mkoani Mbeya akitumia jina la Hamimu Hassan.

Imebainika kuwa kabla ya kuhitimu darasa la saba kwa mara ya pili, alibadili jina hilo (kutoka Hamimu Hassan) na kuwa Hamimu Augustino ambalo aliendelea nalo wakati akisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari kutwa ya Mbeya (Mbeya Day) mwaka 1990.

Hata hivyo, Mulugo mwenyewe akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam alipuuza tuhuma hizo kwa kusema kuwa ni njama za kisiasa zinazofanywa na maadui zake. Mulugo anasema madai hayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na amekuwa akiyajibu kwa kuwaonyesha vyeti vyake halali vya shule.

"Hayo madai ni ya muda mrefu, wewe sijui utakuwa mtu wa 20 kuuliza swali kama hilo. Mimi vyeti ninavyo na hata ukitaka ushahidi nitakuonyesha," alisema Waziri Mulugo na kuongeza:

"Haya mambo kabla hata sijachaguliwa kuwa Mbunge, tulivyokuwa bado kwenye mchujo wa ndani, usiku wa manane watu walisambaza huu uvumi na nilivyoenda kwenye kikao nikatoa vyeti vyangu, wakaviona."

Waliomfundisha

Baadhi ya walimu waliomfundisha Mulugo, watu waliofanya kazi naye pamoja na wakazi wa Kijiji cha Udinde alikozaliwa, maelezo yao yanathibitisha mabadiliko ya majina ya Mulugo kwa nyakati tofauti pia ngazi mbalimbali za kielimu.

Uchunguzi unabainisha kuwa baada ya kuhitimu kidato cha nne, alifaulu kwenda Shule ya Sekondari ya Wavulana, Songea ambako alisoma kati ya 1994 na 1996 akiendelea kutumia jina la Hamimu Mulugo.

Baada ya kuhitimu kidato cha sita, uchunguzi ulibaini kuwa Mulugo alirejea Mbeya na 1998 alilazimika kubadili tena jina pale alipotumia cheti cha mtu aitwaye Dickson Mulungu, kuombea kazi ya kufundisha katika Shule ya Sekondari ya Southern Highlands.

Habari zinasema Mulugo alichukua hatua hiyo ili kumshawishi mmiliki wa shule hiyo mfanyabiashara, Gulnoor Dossa (sasa ni marehemu), kumpa nafasi ya kufundisha shuleni hapo.

"Mulugo alilazimika kutumia cheti cha rafiki yake aliyekuwa akiitwa Dick Mulungu ambaye alipata daraja la pili katika Shule ya Sekondari ya Songea Boys, hivyo ikawa rahisi kwake kupata kazi ya ualimu katika shule hiyo," alisema mmoja wa waliofanya kazi naye shuleni hapo (jina tunalihifadhi kwa sasa).

Aliongeza kuwa Mulugo alianza kama mwalimu wa kawaida, lakini baadaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Shule (headmaster) wakati hakuwa hata na cheti cha ualimu. Alichukua nafasi hiyo ya ukuu wa shule baada ya aliyekuwapo kufariki dunia.

"Unajua wale wahindi (wamiliki) walikuwa ni wafanyabiashara kwa hiyo hawakufuatilia kiwango cha elimu ndiyo maana walimpandisha tu madaraja bila kujali kuwango cha elimu," alisema rafiki yake huyo na kuongeza:

"Nilimshauri aachane na cheo hicho kwani kama ungefanyika ukaguzi wa Serikali na kumkuta bila vyeti vya ualimu angechukuliwa hatua, hivyo alinisikiliza na akaachia nafasi hiyo na kujipa cheo cha umeneja wa shule."

Suala la uwezo na elimu ya Mulugo liliibua mjadala siku chache zilizopita baada ya kutoa kauli nchini Afrika Kusini aliponukuliwa akisema Tanzania ni muungano wa nchi mbili ambazo ni Tanganyika na Zimbabwe badala ya Zanzibar.

Alikotokea

Uchunguzi wa gazeti hili ulianzia katika kijiji alichozaliwa cha Udinde, Kata ya Kapalala wilayani Chunya mkoani Mbeya na alisoma Shule ya Msingi ya Rukwa.

Mmoja wa walimu waliomfundisha aliyejitambulisha kwa jina la Nyoni anasema anakumbuka kwamba Naibu Waziri huyo 1989 na wakati huo alikuwa akijulikana kwa jina la Hamimu Hassan.

"Mimi nilihamia hapa 1989 nikitokea Shule ya Msingi Kapalala. Kulikuwa na mwalimu mmoja tu kwa hiyo nikawa wa pili. Namfahamu Mulugo wakati huo akiitwa Hamimu Hassan. Sijui kabla hapo alikuwa akitumia jina gani," alisema Nyoni anayetarajia kustaafu kazi ya ualimu mwakani.

Mmoja wa ndugu wa karibu wa Waziri Mulugo anayeishi kijijini hapo ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini alikiri kuwa awali waziri huyo alikuwa akiitwa Philipo Augustino Mulugo.

"Philipo amesomea hapo Rukwa, ambayo ni Shule ya Msingi na alikwenda Kijiji cha Mkulwe kabla ya kwenda Mbeya kuwa Mwalimu. Sijui kama alirudia shule," alisema ndugu huyo.

Mkazi mwingine wa kijijini hapo, Peter Kayuti alikiri kumfahamu Waziri Mulugo tangu enzi za utoto na kwamba alirudia darasa la saba, lakini alisema hakumbuki jina la pili alilolitumia. "Ni kweli Philipo alirudia shule, lakini sijui kama alitumia jina jingine zaidi ya hilo la sasa," alisema Kayuti.

Mwalimu aliyemfundisha katika Shule ya Sekondari Mbeya ambaye pia aliomba jina lake lihifadhiwe, alikiri kumfahamu kwa jina la Hamimu Augustino, lakini akasema hafahamu lilibadilika lini.

"Ni kweli, nilimfundisha Waziri Mulugo na alikuwa akiitwa Hamimu Agustino. Sidhani kama ni jambo geni kwa wanafunzi hasa wa zamani kurudia shule… Zamani ilikuwa kawaida kwa kuwa shule zilikuwa chache. Sijui alibadilisha jina hilo lini, lakini hilo ni suala la kisheria tu," alisema mwalimu huyo.

Utata wa majina

Mwalimu mwingine aliyewahi kufanya kazi na Waziri Mulugo katika Shule ya Southern Highlands alisema waziri huyo alikuwa na tabia ya kuchanganya majina yake ya awali ili kuficha cheti alichoombea kazi.

"Yule alikuwa mjanja sana, ndiyo maana ukiangalia kadi zake zilikuwa na majina mengi tu na yana badilika. Leo atasaini barua kwa jina hili kesho lile. Mara utaona ameandika kifupisho cha PHDA, yaani Philip Hamimu Dick Agustino, mara Mulungu EDM, mara Mulugu D. Philip," alisema mwalimu huyo na kuongeza:

"Amekuwa akijaribu kulibadilisha jina la Mulungu kuwa Mulugu mwisho amelipeleka kuwa lake la awali la Mulugo. Yote hayo ni kuficha tu ukweli kwamba alitumia cheti cha Dick Mulungu," alisema mwalimu huyo.

Mmoja wa wakuregenzi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (jina tunalihifadhi) alisema: "Ili mwalimu wa sekondari awe headmaster (mkuu wa shule) ni lazima awe na shahada ya kwanza kutoka kwenye chuo kikuu kinachotambulika. Anatakiwa pia kuwa na uzoefu wa kazi wa miaka isiyopungua minane."

Kuhusu kughushi vyeti mkurugenzi huyo alisema, ikigundulika kuwa mwalimu ameghushi cheti anafukuzwa kazi mara moja, lakini alikiri kwamba katika shule binafsi inawezekana walimu wasio na sifa wakapenya, lakini wakaguzi wakibaini hutoa maelekezo wafukuzwe.

"Kwanza siku hizi ili mwalimu aajiriwe ni lazima akabidhi vyeti vyake wizarani na hupelekwa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) ili kuhakikiwa. Zamani ukaguzi haukuwa makini kwa hiyo inawezekana kuna watu wasio na sifa walipenya," alisema.

Kuhusu kurudia darasa la saba, alisema sheria haijawahi kuruhusu watu kurudia darasa la saba na kwamba wale waliorudia hutumia mbinu zao kufanya hivyo.

"Sheria haijawahi kuruhusu watu kurudia darasa la saba. Ni kweli wengi wamerudia sijui wanatumia mbinu gani, lakini hairuhusiwi. Ukishafanya mtihani wa darasa la saba mara moja ndiyo basi," alisema mkurugenzi huyo.

Msemaji wa wizara hiyo, Mtandi Bunyanzu kwa kila swali aliloulizwa alisema hana uhakika hivyo asingeweza kutoa jibu lakini kwa suala la kughushi vyeti, alisema ni kosa la jinai siyo kwa walimu tu bali kwa kila mtu atakayebainika.

"Kughushi vyeti ni kosa la jina siyo kwa walimu tu, hata waandishi wa habari," aliongeza Bunyanzu.

Kwa upande wake, Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) halikuwa tayari kutoa matokeo ya mitihani ya Mulugo na badala yake msemaji wa baraza hilo John Nchimbi alisema matokeo hayo ni siri ya mtahiniwa na hawezi kupewa mtu mwingine.

CHANZO:MWANANCHI
 
Mhmm! Mi nilifikiri hakukanyaga kabisa darasani? Kumbe kaingia darasani ila kwa kutumia jina la mtu mwingine. Mi namsifu maana wkt huo nasikia usipochaguliwa kwenda sekondari sio kwa sababu umefeli, bali nafasi zilikuwa chache. Lkn pia namsifu kuwa alikuwa na nia ya kusoma ndio maana alistruggle, sio mabongo flava wa sasa:yo:
 
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Philipo Mulugo anadaiwa kutumia ujanja katika wasifu na elimu yake ambapo katika maisha yake ya kielimu ametumia majina manne tofauti.Uchunguzi uliofanywa na gazeti la mwananchi umegundua kuwa mwaka 1988 alihitimu darasa la saba na alijulikana kwa jina la Philipo Augustine Mulugo na hakufaulu.Mwaka 1989 alirudia kwa jina la Hamimu Hassani katika shule ya msingi Rukwa mkoani Mbeya.Tena akabadili jina na kuitwa Hamimu Augustino wakati yupo Sekondari ya Mbeya Day mwaka 1990.Mwaka 1998 akaitwa Dickson Mulungo,jina la mwanafunzi mwenzie waliomaliza wote Sekondari yaSongea Boys ambaye alipata division two.
SASA HIVI HUYU MTU NI NAIBU WIZARA YA ELIMU WAKATI YEYE MWENYEWE NI BINGWA WA KUBADILI MAJINA NDIO MAANA WATOTO WANACHORA MAZOMBI.

source;gazeti la mwananchi la leo tarehe 25/03/2013.
 
Kamanda kova acha "double standard" kamata hiyo mutu kisha tia ndani!

Au mpaka Ikulu waseme?!
 
suala la mulugu tulilifanyia kazi sana lakini tulikwamishwa na mtu wizara ya elimu anaitwa mtandi bunyanzi. pale wizarani yaani huyu mtu ni mkorofi sijapata kuona kwa kukataa kujibu maswali simple kama mulugu alikuwa mwalim mwalim huko mbeya je alisomea ualimu wapi?? kulingana na info. tulizo nazo ni kuwa dick mulugu alipata division one mwaka 1996 je ilikuwaje asiende university mpaka mwaka 2004 aje kujiunga na open university tena kwa kujilipia yeye mwenyewe wakati angeweza kwenda udsm na kulipiwa ingawa ni mkopo ?? je alipokuwa sekondari ya highland alifukuzwa kazi je alifukuzwa kazi kwa ajili ya kufanya nini ?? ingawa vyanzo vyetu vinasema alifukuzwa kwa wizi. je mtu huyu anawezaje kuwa naibu waziri wa elimu wakati shule yake aliyokuwa akiongoza ilifungiwa na serikali kwa kughushi mitiani? mulugu ni mfanyakazi wa umma kwahiyo taarifa hizi zote inabidi zipatikane kwa wananchi. he is not a private citizen. unapokuwa mtumishi wa umma watu wana haki kujua taarifa zako muhimu kama hizi kwahiyo chadema wanaweza wakamghaghania mulugo kupitia suala hili na nimaamini atangoka tu maana limemkalia vibaya sana.

Mtu huyu anayeitwa Dick Mulungu mimi binafsi namfahamu vizuri. Alikuwa mwalim wangu wa Historia miaka kati ya 2001 hadi 2003 pale Mzumbe Secondary School. Ana BA with Education, MA na sasa anafanya PhD pale UDSM sina hakika kafikia wapi kwa hiyo programme yake ya PhD. Kwa sasa ni Assistant Lecturer pale Mkwawa University College na pia ni part time lecturer wa RUCO. Taarifa zote za kwamba kasoma Songea Boys na ni wa Mbeya ni kweli. Kama naye alishirika katika dili hili, he has also to be implicated with this scandal. Lakin Bongo kama kawaida issue ikisha mgusa waziri tena toka chama tawala, basi yoyote yule asemaye hivyo ni adui wa kisiasa. We don't look at things objectively. Hilo ndo tatizo la msingi katika mambo mengi sana hapa Tanzania.
 
Waziri kilaza na mwizi, nini tunategemea hapo? Kama baba ni mwizi wa sukari ndani watoto wafanyeje,? Hiyo ndo mitaala ya elimu Tanzania
 
Watu sampuli ya naibu waziri Mulugo wako wengi sana ndani ya ccm kwakuwa huko ndiko usalama wao ulipo.

Lakini kwakuwa sasa mambo yake yamewekwa hadharani hana budi kujiengua mwenyewe, hana sababu ya kusubiri aenguliwe kwakuwa hii kashfa ni nzito sana kwake na kwa wizara ya elimu pamoja na serikali nzima.

Suala la yeye kurudia shule ya msingi si hoja sana lakini watetezi wake watambue kuwa hoja ya msingi ni yeye kutumia cheti cha mtu (Dick Mulungu) kujipatia ajira baada ya kufeli kidato cha sita na hivyo kuwanyima fursa waliostahili ajira hiyo.

Hivi huyo Dick Mulungu nae hana hatia katika sakata hili? Kwa kufacilitate kufanyika kwa makosa ya udanganyifu katika ajira ya Mulugo?
 
Back
Top Bottom