Hivi hili lijitu inakuwaje linaachiwa achiwa tu.....hivi kweli sisi Watanzania wote tumekuwa Mipumbavu kiasi cha kuachia UOZO ulio wazi kama huu wa "Mulugo"............halafu anajigamba kuwa na "vyeti".......hivi watu wote wenye bongo zao wenye jukumu la kucheck hivyo vyeti........bado mmekaa kimya tu..........
Mpuuzi mwingine kutoka NECTA eti anasema matokeo ni siri ya mtahiniwa........shame on you.....hili lijitu limepewa Public Office.....kwa nini iwe siri.........hivi kwanini sisi wabongo tunaendekeza UPUUZI.......maneno meeengi.....kila kukicha......unasikia upuuzi tu.........can someone out there put STOP to these stupid things...........damn!
Mmoja wa wakuregenzi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (jina tunalihifadhi) alisema: "Ili mwalimu wa sekondari awe headmaster (mkuu wa shule) ni lazima awe na shahada ya kwanza kutoka kwenye chuo kikuu kinachotambulika. Anatakiwa pia kuwa na uzoefu wa kazi wa miaka isiyopungua minane."
Kuhusu kughushi vyeti mkurugenzi huyo alisema, ikigundulika kuwa mwalimu ameghushi cheti anafukuzwa kazi mara moja, lakini alikiri kwamba katika shule binafsi inawezekana walimu wasio na sifa wakapenya, lakini wakaguzi wakibaini hutoa maelekezo wafukuzwe.
"Kwanza siku hizi ili mwalimu aajiriwe ni lazima akabidhi vyeti vyake wizarani na hupelekwa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) ili kuhakikiwa. Zamani ukaguzi haukuwa makini kwa hiyo inawezekana kuna watu wasio na sifa walipenya," alisema.
Kuhusu kurudia darasa la saba, alisema sheria haijawahi kuruhusu watu kurudia darasa la saba na kwamba wale waliorudia hutumia mbinu zao kufanya hivyo.
"Sheria haijawahi kuruhusu watu kurudia darasa la saba. Ni kweli wengi wamerudia sijui wanatumia mbinu gani, lakini hairuhusiwi. Ukishafanya mtihani wa darasa la saba mara moja ndiyo basi," alisema mkurugenzi huyo.
Nitumie nafasi hii kumbumbusha bosi wa Mulugo Rais Kikwete. Mwezi uliyopita Mwakyembe aliwafukuza /kuwasimamisha kazi wafanyakazi 11 wa bandari ya Tanga kwa kosa la kufoji au kutumia vyeti visivyo vyao kupata hajira Bandari ya Tanga (Kama aliyofanya Bwana Mulugo kutumia cheti cha Dick Mulungu). Kosa hilo linafanana kabisa la Naibu waziri wako Philipo Mulugo ambaye pia anafahamika kwa majina mengine kama Hamimu Augustino/ Hamimu Augustino/ Philipo Hamimu/ Dick Augustino/ Mulugo EDM na pia kama Mulugo D. Philip. Usipomfukuza uyu kazi means wale wote waliofukuzwa huko nyuma kwa kuwa na vyeti bandia warudishwe kazini.
Nape na secretariat yako pia inawahusu: mkimwacha uyu mtu aendelee na ubunge na vyeo vingine vya CCM means mnabariki vyeti bandia. Hiki ni kipimo kizuri cha ccm. Wazee wa TISS pia hii ni haibu yenu, je uwa hampitii mafaili/profile ya wateuliwa wa rais kwa ngazi za juu kama hizi kabla hawajateuliwa?.
Hizi tuhuma dhini ya Mh. Mulugo zinaonekana kuna ka-ukweli ndani yake, yaani watu wote wamsingizie, Mh. Mulugo hebu jitokeze utueleze ukweli maana katika 'public office' vyeti vyako vyote umma unastahili kupata ukweli hutakiwi kujitetea ktk 'vikao vya ndani' au 'kupitia wizara elimu ambapo pia wewe ni boss', jitokeze Mheshimiwa uueleze umma kuhusu mtiririko wa vyeti vyako.
Halafu inaundwa tume ya kuchunguza mass failure F4 huku NaibuWaziri ni kihiyo.