Naibu Waziri Elimu katika kashfa vyeti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu Waziri Elimu katika kashfa vyeti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MALIKITI, Mar 25, 2013.

 1. M

  MALIKITI Member

  #1
  Mar 25, 2013
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo anadaiwa kutumia ujanja katika wasifu na elimu yake ambapo katika maisha yake ya kielimu ametumia majina manne tofauti. Philipo Augustine Mulugo ndiyo jina lake halisi ambalo alilisomea mpaka alipohitimu darasa la saba kwa mara ya kwanza 1988, lakini kutokana na kwamba hakufaulu kwenda sekondari alirudia darasa hilo.

  Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwa takriban miezi mitatu sasa umebaini kuwa 1989, Mulugo alirudia darasa la saba katika Shule ya Msingi Rukwa ya mkoani Mbeya akitumia jina la Hamimu Hassan.

  Imebainika kuwa kabla ya kuhitimu darasa la saba kwa mara ya pili, alibadili jina hilo (kutoka Hamimu Hassan) na kuwa Hamimu Augustino ambalo aliendelea nalo wakati akisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari kutwa ya Mbeya (Mbeya Day) mwaka 1990.

  Hata hivyo, Mulugo mwenyewe akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam alipuuza tuhuma hizo kwa kusema kuwa ni njama za kisiasa zinazofanywa na maadui zake. Mulugo anasema madai hayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na amekuwa akiyajibu kwa kuwaonyesha vyeti vyake halali vya shule.

  “Hayo madai ni ya muda mrefu, wewe sijui utakuwa mtu wa 20 kuuliza swali kama hilo. Mimi vyeti ninavyo na hata ukitaka ushahidi nitakuonyesha,” alisema Waziri Mulugo na kuongeza:

  “Haya mambo kabla hata sijachaguliwa kuwa Mbunge, tulivyokuwa bado kwenye mchujo wa ndani, usiku wa manane watu walisambaza huu uvumi na nilivyoenda kwenye kikao nikatoa vyeti vyangu, wakaviona.”

  Waliomfundisha

  Baadhi ya walimu waliomfundisha Mulugo, watu waliofanya kazi naye pamoja na wakazi wa Kijiji cha Udinde alikozaliwa, maelezo yao yanathibitisha mabadiliko ya majina ya Mulugo kwa nyakati tofauti pia ngazi mbalimbali za kielimu.

  Uchunguzi unabainisha kuwa baada ya kuhitimu kidato cha nne, alifaulu kwenda Shule ya Sekondari ya Wavulana, Songea ambako alisoma kati ya 1994 na 1996 akiendelea kutumia jina la Hamimu Mulugo.

  Baada ya kuhitimu kidato cha sita, uchunguzi ulibaini kuwa Mulugo alirejea Mbeya na 1998 alilazimika kubadili tena jina pale alipotumia cheti cha mtu aitwaye Dickson Mulungu, kuombea kazi ya kufundisha katika Shule ya Sekondari ya Southern Highlands.

  Habari zinasema Mulugo alichukua hatua hiyo ili kumshawishi mmiliki wa shule hiyo mfanyabiashara, Gulnoor Dossa (sasa ni marehemu), kumpa nafasi ya kufundisha shuleni hapo.
  “Mulugo alilazimika kutumia cheti cha rafiki yake aliyekuwa akiitwa Dick Mulungu ambaye alipata daraja la pili katika Shule ya Sekondari ya Songea Boys, hivyo ikawa rahisi kwake kupata kazi ya ualimu katika shule hiyo,” alisema mmoja wa waliofanya kazi naye shuleni hapo (jina tunalihifadhi kwa sasa).


  Aliongeza kuwa Mulugo alianza kama mwalimu wa kawaida, lakini baadaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Shule (headmaster) wakati hakuwa hata na cheti cha ualimu. Alichukua nafasi hiyo ya ukuu wa shule baada ya aliyekuwapo kufariki dunia.

  “Unajua wale wahindi (wamiliki) walikuwa ni wafanyabiashara kwa hiyo hawakufuatilia kiwango cha elimu ndiyo maana walimpandisha tu madaraja bila kujali kuwango cha elimu,” alisema rafiki yake huyo na kuongeza:

  “Nilimshauri aachane na cheo hicho kwani kama ungefanyika ukaguzi wa Serikali na kumkuta bila vyeti vya ualimu angechukuliwa hatua, hivyo alinisikiliza na akaachia nafasi hiyo na kujipa cheo cha umeneja wa shule.”

  Suala la uwezo na elimu ya Mulugo liliibua mjadala siku chache zilizopita baada ya kutoa kauli nchini Afrika Kusini aliponukuliwa akisema Tanzania ni muungano wa nchi mbili ambazo ni Tanganyika na Zimbabwe badala ya Zanzibar.  Alikotokea
  Uchunguzi wa gazeti hili ulianzia katika kijiji alichozaliwa cha Udinde, Kata ya Kapalala wilayani Chunya mkoani Mbeya na alisoma Shule ya Msingi ya Rukwa.

  Mmoja wa walimu waliomfundisha aliyejitambulisha kwa jina la Nyoni anasema anakumbuka kwamba Naibu Waziri huyo 1989 na wakati huo alikuwa akijulikana kwa jina la Hamimu Hassan.

  “Mimi nilihamia hapa 1989 nikitokea Shule ya Msingi Kapalala. Kulikuwa na mwalimu mmoja tu kwa hiyo nikawa wa pili. Namfahamu Mulugo wakati huo akiitwa Hamimu Hassan. Sijui kabla hapo alikuwa akitumia jina gani,” alisema Nyoni anayetarajia kustaafu kazi ya ualimu mwakani.

  Mmoja wa ndugu wa karibu wa Waziri Mulugo anayeishi kijijini hapo ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini alikiri kuwa awali waziri huyo alikuwa akiitwa Philipo Augustino Mulugo.

  “Philipo amesomea hapo Rukwa, ambayo ni Shule ya Msingi na alikwenda Kijiji cha Mkulwe kabla ya kwenda Mbeya kuwa Mwalimu. Sijui kama alirudia shule,” alisema ndugu huyo.

  Mkazi mwingine wa kijijini hapo, Peter Kayuti alikiri kumfahamu Waziri Mulugo tangu enzi za utoto na kwamba alirudia darasa la saba, lakini alisema hakumbuki jina la pili alilolitumia. “Ni kweli Philipo alirudia shule, lakini sijui kama alitumia jina jingine zaidi ya hilo la sasa,” alisema Kayuti.

  Mwalimu aliyemfundisha katika Shule ya Sekondari Mbeya ambaye pia aliomba jina lake lihifadhiwe, alikiri kumfahamu kwa jina la Hamimu Augustino, lakini akasema hafahamu lilibadilika lini.

  “Ni kweli, nilimfundisha Waziri Mulugo na alikuwa akiitwa Hamimu Agustino. Sidhani kama ni jambo geni kwa wanafunzi hasa wa zamani kurudia shule… Zamani ilikuwa kawaida kwa kuwa shule zilikuwa chache. Sijui alibadilisha jina hilo lini, lakini hilo ni suala la kisheria tu,” alisema mwalimu huyo.

  Utata wa majina


  Mwalimu mwingine aliyewahi kufanya kazi na Waziri Mulugo katika Shule ya Southern Highlands alisema waziri huyo alikuwa na tabia ya kuchanganya majina yake ya awali ili kuficha cheti alichoombea kazi.

  “Yule alikuwa mjanja sana, ndiyo maana ukiangalia kadi zake zilikuwa na majina mengi tu na yana badilika. Leo atasaini barua kwa jina hili kesho lile. Mara utaona ameandika kifupisho cha PHDA, yaani Philip Hamimu Dick Agustino, mara Mulungu EDM, mara Mulugu D. Philip,” alisema mwalimu huyo na kuongeza:

  “Amekuwa akijaribu kulibadilisha jina la Mulungu kuwa Mulugu mwisho amelipeleka kuwa lake la awali la Mulugo. Yote hayo ni kuficha tu ukweli kwamba alitumia cheti cha Dick Mulungu,” alisema mwalimu huyo.

  Mmoja wa wakuregenzi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (jina tunalihifadhi) alisema: “Ili mwalimu wa sekondari awe headmaster (mkuu wa shule) ni lazima awe na shahada ya kwanza kutoka kwenye chuo kikuu kinachotambulika. Anatakiwa pia kuwa na uzoefu wa kazi wa miaka isiyopungua minane.”

  Kuhusu kughushi vyeti mkurugenzi huyo alisema, ikigundulika kuwa mwalimu ameghushi cheti anafukuzwa kazi mara moja, lakini alikiri kwamba katika shule binafsi inawezekana walimu wasio na sifa wakapenya, lakini wakaguzi wakibaini hutoa maelekezo wafukuzwe.

  “Kwanza siku hizi ili mwalimu aajiriwe ni lazima akabidhi vyeti vyake wizarani na hupelekwa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) ili kuhakikiwa. Zamani ukaguzi haukuwa makini kwa hiyo inawezekana kuna watu wasio na sifa walipenya,” alisema.

  Kuhusu kurudia darasa la saba, alisema sheria haijawahi kuruhusu watu kurudia darasa la saba na kwamba wale waliorudia hutumia mbinu zao kufanya hivyo.

  “Sheria haijawahi kuruhusu watu kurudia darasa la saba. Ni kweli wengi wamerudia sijui wanatumia mbinu gani, lakini hairuhusiwi. Ukishafanya mtihani wa darasa la saba mara moja ndiyo basi,” alisema mkurugenzi huyo.

  Msemaji wa wizara hiyo, Mtandi Bunyanzu kwa kila swali aliloulizwa alisema hana uhakika hivyo asingeweza kutoa jibu lakini kwa suala la kughushi vyeti, alisema ni kosa la jinai siyo kwa walimu tu bali kwa kila mtu atakayebainika.

  “Kughushi vyeti ni kosa la jina siyo kwa walimu tu, hata waandishi wa habari,” aliongeza Bunyanzu.

  Kwa upande wake, Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) halikuwa tayari kutoa matokeo ya mitihani ya Mulugo na badala yake msemaji wa baraza hilo John Nchimbi alisema matokeo hayo ni siri ya mtahiniwa na hawezi kupewa mtu mwingine.


  Chanzo: Gazeti la Mwananchi, Machi 25, 2013

  Hii ni habari inayoambatana na anguko la elimu nchini mwetu

   
 2. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #2
  Mar 25, 2013
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,913
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
  Ufundi, Philipo Mulugo anadaiwa kutumia
  ujanja katika wasifu na elimu yake ambapo
  katika maisha yake ya kielimu ametumia
  majina manne tofauti.
  Philipo Augustine Mulugo ndiyo jina lake
  halisi ambalo alilisomea mpaka alipohitimu
  darasa la saba kwa mara ya kwanza 1988,
  lakini kutokana na kwamba hakufaulu
  kwenda sekondari alirudia darasa hilo.
  Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwa
  takriban miezi mitatu sasa umebaini kuwa
  1989, Mulugo alirudia darasa la saba katika
  Shule ya Msingi Rukwa ya mkoani Mbeya
  akitumia jina la Hamimu Hassan.
  Imebainika kuwa kabla ya kuhitimu darasa
  la saba kwa mara ya pili, alibadili jina hilo
  (kutoka Hamimu Hassan) na kuwa Hamimu
  Augustino ambalo aliendelea nalo wakati
  akisoma elimu ya sekondari katika Shule ya
  Sekondari kutwa ya Mbeya (Mbeya Day)
  mwaka 1990.
  Hata hivyo, Mulugo mwenyewe
  akizungumza na gazeti hili jijini Dar es
  Salaam alipuuza tuhuma hizo kwa kusema
  kuwa ni njama za kisiasa zinazofanywa na
  maadui zake. Mulugo anasema madai hayo
  yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na
  amekuwa akiyajibu kwa kuwaonyesha
  vyeti vyake halali vya shule.
  “Hayo madai ni ya muda mrefu, wewe sijui
  utakuwa mtu wa 20 kuuliza swali kama hilo.
  Mimi vyeti ninavyo na hata ukitaka ushahidi
  nitakuonyesha,” alisema Waziri Mulugo na
  kuongeza:
  “Haya mambo kabla hata sijachaguliwa
  kuwa Mbunge, tulivyokuwa bado kwenye
  mchujo wa ndani, usiku wa manane watu
  walisambaza huu uvumi na nilivyoenda
  kwenye kikao nikatoa vyeti vyangu,
  wakaviona.”
  Waliomfundisha
  Baadhi ya walimu waliomfundisha Mulugo,
  watu waliofanya kazi naye pamoja na
  wakazi wa Kijiji cha Udinde alikozaliwa,
  maelezo yao yanathibitisha mabadiliko ya
  majina ya Mulugo kwa nyakati tofauti pia
  ngazi mbalimbali za kielimu.
  Uchunguzi unabainisha kuwa baada ya
  kuhitimu kidato cha nne, alifaulu kwenda
  Shule ya Sekondari ya Wavulana, Songea
  ambako alisoma kati ya 1994 na 1996
  akiendelea kutumia jina la Hamimu Mulugo.
  Baada ya kuhitimu kidato cha sita,
  uchunguzi ulibaini kuwa Mulugo alirejea
  Mbeya na 1998 alilazimika kubadili tena jina
  pale alipotumia cheti cha mtu aitwaye
  Dickson Mulungu, kuombea kazi ya
  kufundisha katika Shule ya Sekondari ya
  Southern Highlands.
  Habari zinasema Mulugo alichukua hatua
  hiyo ili kumshawishi mmiliki wa shule hiyo
  mfanyabiashara, Gulnoor Dossa (sasa ni
  marehemu), kumpa nafasi ya kufundisha
  shuleni hapo.
   
 3. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2013
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,920
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kitendo cha kutumia jina la mtu mwingine kuomba kazi ni udanganyifu na ni Tanzania tu mtu aliefanya udanganyifu kama huo anaendelea kufanya kazi serikalini.
   
 4. m

  manucho JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2013
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa pamoja na kutumia vyeti vya mtu mwingine, uwezo wake ktk hali ya kawaida ni mdogo sana. Nadhani amezaliwa hivyo ila mambo ya kupeana uongozi ndiyo haya sasa.
   
 5. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2013
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Form six alipata div.4
   
 6. tetere

  tetere JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2013
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 962
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kwa nini mwajiri wa Mulugo ndio wababaishaji kuliko hata Mulugo mwenyewe! Kwa nini boss wake hatoi tamko juu ya hii sintofahamu??????

  Au Mulugo ana akili sana - taifa litakosa mchango wake kwenye wizara hii nyeti ya Elimu hasa kipindi hii ambacho wanahitaji mtu mwenye uwezo kama Mulugo kuweza kuwaondoa kwenye kitanzi cha kufeli!!!!!!!!1 Wizara ya Elimu ni kitovu cha Uzembe.
   
 7. Msenyele

  Msenyele JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2013
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  ukiona mtu wa dizaini ile ujue ni kilaza.
   
 8. Nyahende Thomas

  Nyahende Thomas Verified User

  #8
  Mar 25, 2013
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wala issue si kufanya kazi serikalini tu. Ni kwamba mtu mwenye elimu ya mashaka, mwenye elimu ya kuungaunga ndiye naibu waziri wa elimu!

  Hii inawezekana Tanzania tu kwamba mburura ndo wanaongoza wizara ya elimu halafu tunatarajia matokeo mazuri.
   
 9. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2013
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Hii nchi yetu ni ya ajabu! Elimu ya watu wengi walio kwenye majukumu muhimu ya kuhakikisha ustawi na maendeleo ya nchi hii ni ya mashaka. Tusishangae kkuwa mambo hayaendi vyema, toka juu huo mti unateremka hivyo hivyo...vilaza ndio tumewapa majukumu. Ninadhani wanachofanya ni kutukomoa kwa kuwa tuliwaburuza shule, na hawataki kusikia ushauri hata kidogo.
   
 10. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2013
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,813
  Likes Received: 804
  Trophy Points: 280
  huyu atupishe wala haitaji maandamano, hana moral authority ya kuwa naibu waziri wala kuwa kiongozi wa umma
   
 11. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2013
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,421
  Likes Received: 484
  Trophy Points: 180
  Hah hivi umri wake ndio huo? Ss tuliosoma vidato na vyuo tuko bomba kuliko huyu ms****ng***** mwizi
   
 12. m

  manucho JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2013
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii ni hatari sana kwa taifa, haina tofauti na form IV/VI Div 0 ndiyo anakwenda kusomea ualimu tena wa vodafasta nini kitatokea hapo. . . .
   
 13. m

  manucho JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2013
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hivi huyu nae anateuliwa na Rais au!
   
 14. p

  politiki JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2013
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,332
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  suala la mulugu tulilifanyia kazi sana lakini tulikwamishwa na mtu wizara ya elimu anaitwa mtandi bunyanzi. pale wizarani yaani huyu mtu ni mkorofi sijapata kuona kwa kukataa kujibu maswali simple kama mulugu alikuwa mwalim mwalim huko mbeya je alisomea ualimu wapi?? kulingana na info. tulizo nazo ni kuwa dick mulugu alipata division one mwaka 1996 je ilikuwaje asiende university mpaka mwaka 2004 aje kujiunga na open university tena kwa kujilipia yeye mwenyewe wakati angeweza kwenda udsm na kulipiwa ingawa ni mkopo ?? je alipokuwa sekondari ya highland alifukuzwa kazi je alifukuzwa kazi kwa ajili ya kufanya nini ?? ingawa vyanzo vyetu vinasema alifukuzwa kwa wizi. je mtu huyu anawezaje kuwa naibu waziri wa elimu wakati shule yake aliyokuwa akiongoza ilifungiwa na serikali kwa kughushi mitiani? mulugu ni mfanyakazi wa umma kwahiyo taarifa hizi zote inabidi zipatikane kwa wananchi. he is not a private citizen. unapokuwa mtumishi wa umma watu wana haki kujua taarifa zako muhimu kama hizi kwahiyo chadema wanaweza wakamghaghania mulugo kupitia suala hili na nimaamini atangoka tu maana limemkalia vibaya sana.
   
 15. m

  manucho JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2013
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii ni hatari sana kwa taifa, haina tofauti na form IV/VI Div 0 ndiyo anakwenda kusomea ualimu tena wa vodafasta nini kitatokea hapo. . . .
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2013
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,599
  Likes Received: 5,928
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana mimi sipendi mambo ya majina manne manne kama ukoo wa kifalme wa Hispania.

  Sijui Mizengwe Kaanza Kupita Pinda, watapindisha mengi hawa.
   
 17. Mad Max

  Mad Max JF-Expert Member

  #17
  Mar 25, 2013
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,410
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 180
  Hata majina yatahitaji DNA test sasa. Dah..
   
 18. m

  manucho JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2013
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mulugo, Mulugu ondoka mwenyewe tu
   
 19. p

  politiki JF-Expert Member

  #19
  Mar 25, 2013
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,332
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  kuwa na Elimu ya kuunga sio tatizo binafsi ila basi hata hiyo ya kuunga iwe ya ukweli basi
   
 20. m

  manucho JF-Expert Member

  #20
  Mar 25, 2013
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mulugo, Mulugu ondoka mwenyewe tu
   
Loading...