Naibu Spika Zungu na Serikali Waungwe Mkono, Bando Zinapaswa Kuwekwa Tozo

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,200
27,255
Hoja ya Zungu kwa wenye akili watafikiria vizuri na kuisupport, serikali imekua ikipoteza mapato kupitia bando. Sasa hivi matumizi makubwa yamehama kutoka kwenye voicecall na kuwa kwenye bando.

Hivyo ninaomba kwa wale wenye akili waunge mkono wazo Hilo la serikali kwa kufikiria na kuja na tozo kwenye bando.

Kama alivyosema zungu makampuni ya simu pamoja na banks zina ujanja mwingi sana kwa kupata kikubwa tofauti na serikali. Hii haikubaliki.
 
Hv huwa mnatumia kichwa cha binadam kufikr kweli, Kwanini msikaze kwenye ukwepaji mkubwa wa Kodi halali Kwa wafanya biashara badala ya kukimbizana na vi bando vya buku buku vya mwananchi.
 
0A1D91D9-A9E2-4DFB-8798-8B988B4AC29A.jpeg
 
Hv huwa mnatumia kichwa cha binadam kufikr kweli, Kwa nini msikaze kwenye ukwepaji mkubwa wa Kodi halali Kwa wafanya biashara badala ya kukimbizana na vi bando vya buku buku vya mwananchi
Nani kakweka Kodi?
 
Chama chetu cha CUK Baada ya katiba Mpya kupatikana na kupewa ridhaa kuongoza nchi kitahakikisha Tozo zote zinafuatwa na tutagawa vitambulisho kwa wajasiria mali kutokana na mitaji yao watavilipia kwa mwaka na Kodi zitapunguzwa kwa wale wenye vitambulisho Hivyo!
 
Namshangaa huyo Zungu "think tank" wa CCM ambae kila siku anawaza namna ya kumkamua mtanzania wa kawaida, akili yake haiendi mbali na hapo, kila siku yuko hapo hapo, ajabu bado wajinga mnampongeza.

Mtakapokata tozo kwenye data, maana yake matumizi ya data lazima yatapungua, kwanza yanazidi kupungua kwa kupandisha kwenu bei kila siku, halafu mnataka huyu mtumiaji anayejitahidi kujibana kupata data kwa matumizi yake, tena mje kumkamua tozo ya hiyo data kidogo aliyomudu kujinunulia.

Hili wazo litaenda kuathiri wengi, hasa wanafunzi wengi hasa vyuoni wanaotumia internet kwa ajili ya masomo yao, na wafanyabiashara wadogo wanaotangaza bidhaa zao mitandaoni, simply huu uamuzi wenu wa kijinga unaenda kuongeza ujinga na umasikini kwenye hili taifa respectively.
 
Namshangaa huyo Zungu "think tank" wa CCM ambae kila siku anawaza namna ya kumkamua mtanzania wa kawaida, akili yake haiendi mbali na hapo, ajabu bado wajinga wanampongeza.

Mtapokata tozo kwenye data, maana yakw matumizi ya data lazima yatapungua, kwanza yanazidi kupungua kwa kupandisha kwenu bei kila siku, halafu mnataka huyu mtumiaji anayejitahidi kujibana kupata data kwa matumizi yake, tena mje kumkamua tozo ya hiyo data kidogo aliyomudu kujinunulia.

Mnaenda kuathiri wengi, hasa wanafunzi wanaotumia internet kwa ajili ya masomo yao, wafanyabiashara wadogo wanaotangaza bidhaa zao mitandaoni, huu uamuzi wenu wa kijinga unaenda kuongeza ujinga na umasikini kwenye hili taifa respectively.
Ukiona gharama sana si unaacha tu?
 
Ukiona gharama sana si unaacha tu?
Tukiacha wote huoni mtakuwa mmefeli kwasababu ya maamuzi yenu ya kijinga?

Wanafunzi wakiacha kwasababu ya gharama...

na wafanyabiashara wadogo nao wakiacha kwa sababu ya gharama ya tozo...

Huzioni athari hasi mtakazoisababishia jamii mnayoitawala? yes naandika mnaitawala sio kuiongoza kwa sababu haya mawazo yenu ni ya mtawala tena dikteta asie na kitu kichwani.
 
Hv huwa mnatumia kichwa cha binadam kufikr kweli, Kwa nini msikaze kwenye ukwepaji mkubwa wa Kodi halali Kwa wafanya biashara badala ya kukimbizana na vi bando vya buku buku vya mwananchi
Usihangaike na huyu jamaa mkuu, hili group la kusifu kila upuuzi wa serikali inaonesha wazi wana jambo lao la siri huko kwenye chama chao dhidi ya mshika kiti.

Hao ni wafu, acha wazikane.
 
Hoja ya zungu kwa wenye akili watafikiria vizuri na kuisupport, serikali imekua ikipoteza mapato kupitia bando. Sasa hivi matumizi makubwa yamehama kutoka kwenye voicecall na kuwa kwenye bando.

Hivyo ninaomba kwa wale wenye akili waunge mkono wazo Hilo la serikali kwa kufikiria na kuja na tozo kwenye bando.

Kama alivyosema zungu makampuni ya simu pamoja na banks zina ujanja mwingi sana kwa kupata kikubwa tofauti na serikali. Hii haikubaliki
Hivi una akili au matope. Ona msg ya Voada kwenye 2000, wanakata kodi 303 almost 30% wanaichukua kama kod halafu unataka waongeze tozo ya kazi gani. Hii nchi ina wajinga wengi.

Break down for Tsh. 2000 airtime is: Cost: Tsh. 1690.68 VAT: Tsh. 304.32 Total: Tsh. 2000
 
Tukiacha wote huoni mtakuwa mmefeli kwasababu ya maamuzi yenu ya kijinga?

Wanafunzi wakiacha kwasababu ya gharama...

na wafanyabiashara wadogo nao wakiacha kwa sababu ya gharama ya tozo...

Huzioni athari hasi mtakazoisababishia jamii mnayoitawala? yes naandika mnaitawala sio kuiongoza kwa sababu haya mawazo yenu ni ya mtawala tena dikteta.
Huwezi amini bado sijakuelewa
 
Ukiona gharama sana si unaacha tu?
Kweli wewe akili yako ya kuvuka barabara, internet sasa hivi sio starehe, ni sehemu ya kujifunza, kufsnya biashara, kuwasiliana wakati dunia inahamia huko badala mhimize watu waende na kasi ya dunia watafute fursa huko mnaona kama wanafaidi mnawaza kuwazuia
 
Wachumi walioiva, wenye uwezo mkubwa wa kushawishi dunia kwa kile walichokisomea, wanatakiwa watoe ushauri sahihi wa kuimarisha uchumi na kupunguza mzigo kwa mlaji
 
Hoja ya Zungu kwa wenye akili watafikiria vizuri na kuisupport, serikali imekua ikipoteza mapato kupitia bando. Sasa hivi matumizi makubwa yamehama kutoka kwenye voicecall na kuwa kwenye bando.

Hivyo ninaomba kwa wale wenye akili waunge mkono wazo Hilo la serikali kwa kufikiria na kuja na tozo kwenye bando.

Kama alivyosema zungu makampuni ya simu pamoja na banks zina ujanja mwingi sana kwa kupata kikubwa tofauti na serikali. Hii haikubaliki.
***** zako kwani hizo bando tunazoweka kwenye simu si zinakatwa kodi, wewe unataka kodi gani tena?
 
Back
Top Bottom