Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Tumemsikia Naibu Spika, Mussa Zungu, akielezea kuhusu tozo zilizolalamikiwa Sana na wananchi, hadi Serikali ikasalimu amri na kuahidi kuzipunguza tozo hizo kuanzia tarehe 1 mwezi ujayo.
Katika maelezo yake alidai eti wananchi wanachujua ni kuilalamikia Serikali kuhusu tozo wanazotoza kwenye miamala hiyo ya simu, lakini wanasahau kuwa makampuni hayo ya simu na mabenki ndiyo yanayotoza kiwango kikubwa zaidi!
Akaendelea kudai kuwa eti tozo tunazolalamikiwa na wananchi ni kwa manufaaa yetu, kwa kuwa ndizo zinazojenga madarasa na vituo vya afya!
Hivi huyu Zungu, anatufanya sisi watanzania wote ni wajinga kiasi hicho, ambacho anaweza kutudanganya atakavyo?
Hivi Hawa CCM wanaopenda kutumia hii propaganda ya kuwa hizo tozo ndizo zinazojenga madarasa na vituo vya afya, nipende tu kuwauliza swali moja, hivi hizi pesa za mikopo ya World Bank na IMF, ambayo tulikuwa tunaambiwa kuwa wamekopa Ili kujengea madarasa na vituo vya afya, pesa hizo zimefanya Kazi gani?
Hawa watawala wetu wanaopenda kutuibibia sisi wananchi wao kwa kupitia hizo tozo, Ili wao waishi Katika Maisha ya kifahari ya kupindukia!
Hivi inawezakanaje wawakilishi wetu ambao ni wabunge, watembelee magari ya anasa Sana ya mavi-eite ya shilingi milioni 400, yakiwa yanagharimikiwa kila kitu na walipa kodi wa nchi hii masikini Sana, halafu asingizie kuwa wanajenga madarasa na vituo vya afya?
Hivi huyu Zungu anawezaje kuilinganisha Serikali na hayo makampuni Katika utozaji wa tozo hizo?
Hivi anajua gharama za makampuni ya simu hapa nchini, ikiwemo kujenga minara, ofisi kwa ajili ya uendeshaji na kuwalipa mishahara wafanyakazi wake, pamoja na kuwalipa kodi mbalimbali kea Serikali hiyo hiyo?
Hivi anawezaje kujilinganisha na makampuni hayo na Serikali, wakati inajulikana wazi kuwa hao Serikali, wanachojua ni kuchukua tozo hizo, wakati hawajawekeza chochote?
Kwa hiyo ni dhahiri huo ni ulafi wa kupitiliza unaowakabili viongozi we serikali hii kandamizi ya CCM, ndiyo unaomfanya huyo Naibu Spika Mussa Zungu, atetee kwa nguvu zote hizo tozo, ambazo zimekataliwa kwa nguvu ya Umma wa wananchi wa nchi hii.
Kifupi tu mwisho wa matozo ya nchi hii, ni kuandika Katiba mpya ya wananchi, itakayoyokana na maoni yetu tuliyoyatoa kupitia kwenye Rasibu ya Warioba.
Mungu ibariki Tanzania