Naibu Spika Zungu, ongoza vikao na acha ukiranja

El Roi

JF-Expert Member
May 29, 2020
263
502
Nikiri kwanza kwamba, baada ya uchaguzi mkuu uliopita 2020, morale ya kufuatilia siasa za nchi hii imeshuka sana kwangu, ukiachia mbali kufuatilia bunge lenyewe. Namna siasa zinavyotafsiriwa na kufanywa kwenye nchi hii, haitii raha kabisa, kama tunakuwa wakweli wa dhamira zetu.

Tunamuomba tu Mungu Sasa ( maana ndo kimbilio lililobaki), tuwe na siasa za usawa, chaguzi za kizalendo na utu na kuacha haki ichukue mkondo wake.

Hata hivyo pamoja na hiyo hang over ya maumivu ya siasa zetu, mara chache napata muda kidogo kufuatilia baadhi ya mambo.

Kwa nyakati kidogo ninazopata kulitizama bunge, Nina bahati fulani sijui njema au mbaya kumkuta kiongozi wa bunge au vikao akiwa naibu spika Mzee Zungu.

Nashindwa kujua sababu kwa Nini anakuwa kila mahali ( He is all over ) kwa kila jambo. Humuoni akiwa amewaacha wabunge kuchangia mawazo Yao, bali unamuona kama kiranja anayetaka mambo yawe kama anavyoona yeye.

Najua Zungu ana umri mkubwa, factor inayoweza kuchangia yeye kuwa muamrishaji badala ya kiongozi, lakini kwa maana ya hicho chombo cha uwakilishi anatakiwa ajifunze kuacha wawakikishi watoe mawazo yao

Ana haki ndiyo ya kusimamia mijadala, lakini hatakiwi kutawala(control) mijadala kwa kiwango Cha kufanya iwe yake na siyo mawazo ya hadhira yake ambayo ni wabunge.

Bunge sasa linajadili mpango wa dira ya maendeleo wa Taifa. ambao kimsingi ni mawazo ya serikali. Hivyo basi, Ili kuimarisha na kuuboresha mpango huo, kuukiranja (limit) uchangiaji kama ninavyoona afanyavyo Zungu, ni kufifisha uchangiaji huo.

Zungu ajifunze kuacha mjadala ujiendeshe wenyewe kwa maana ya kuacha mawazo huru na siyo apendavyo yeye.

Wakati Prof. Muhongo anachangia hoja asubuhi ya Leo, kwa kuwa tu alichangia Kwa tone ya naibu spika, aliongezwa dakika za ziada yeye pamoja na Dr. Kimei Ili wamalize hoja zao. Ambayo nikiri mchango wao ulikuwa wa maana na Mpana.

Baada ya michango Yao ungemuona mwenyekiti wa kikao akiingilia mjadala hata kabla ya mchangiaji kusema neno la mwisho la mchango wake. Asingetaka mtu aongee hata dakika moja ya ziada ya ziada labda kama angeakisi radha yake.

Namshauri Zungu awezeshe mijadala mipana na aepuke syndrome ya ukiranja Ili bungeni kuwe a breeding forum for different flavours of Ideas.

Na aidhulu kama Huwa ana mawazo yake, yeye ana muda wake wa kufanya hivyo.

Acha watu watoe michango yao Kwa uhuru na serikali ambayo ndo walioleta mpango wata react Kwa wakati wao. Wewe sasa ni kiongozi wa bunge na siyo yule waziri aliyepita.
 
Kwa bunge ambalo liko controled na serikali, ni lazima spika adhibiti mijadala. Atakapoacha mijadala huru serikali itaingia matatizoni. Hiyo ndiyo maana halisi ya bunge kibogoyo.
 
Back
Top Bottom