Naibu Spika Zungu: Bodaboda wanakatisha tamaa, wasimamishwe

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
"Suala la bodaboda ni kero kubwa sana na hasa katika utumiaji wa sheria za barabara, mimi ni mtetetezi mkubwa sana wa bodaboda lakini matumizi yao kwenye barabara yanakatisha tamaa lazima muwe na mkakati maalum wa kudhibiti ajali wanazozifanya na lazima muwe na sheria kali za kuwadhibiti na hata kuwasimamisha, sababu ukienda MOI sasa hivi asilimia 90 ni vijana," - Mussa Azan Zungu

20240205_122004.jpg

Credit-EastAfricaTv
 
View attachment 2894963

Credit-EastAfricaTv

Kwa hili namuunga mkono mh Naibu Spika.

Boda Boda waliowengi wapo rough sana katika uendeshaji wao na kibaya zaidi hawafuati sheria za barabarani.

Ajali zimekuwa nyingi tena wakati mwingine wanasababishiana boda boda kwa boda boda yaani unakuta mwingine anaendesha kistaarabu kisha mwingine tena bila tahadhari anakwenda kama mwendawazimu na kuleta ajali.

Wengi ni vijana wadogo na wahuni wanaotumia pombe, Sigara, bangi na vilevi vingine.

Ni watu wasiofuata utaratibu kabisa na sasa hivi ndiyo zinazidi kuongezeka maana boda boda kwa sasa imekuwa kimbilio la wengi.

Najaribu kutafakari baada ya miaka 15 hii hali ikiendelea sipati picha idadi ya hizo boda boda humo barabarani.

Sasa hivi hata kama una mtoto kumtuma hata dukani unapata mashaka makubwa, kila leo Ajali watoto wa shule za msingi wanagongwa na hizi boda boda.
 
Tatizo siasa za hovyo zimeiharibu hii nchi.

Zungu ameongea ukweli hawa vijana wa boda boda ni tatizo kubwa sana mabarabarani wanatakiwa kudhibitiwa kwa sheria kali mno ili waheshimu sheria za barabarani.
 
"Suala la bodaboda ni kero kubwa sana na hasa katika utumiaji wa sheria za barabara, mimi ni mtetetezi mkubwa sana wa bodaboda lakini matumizi yao kwenye barabara yanakatisha tamaa lazima muwe na mkakati maalum wa kudhibiti ajali wanazozifanya na lazima muwe na sheria kali za kuwadhibiti na hata kuwasimamisha, sababu ukienda MOI sasa hivi asilimia 90 ni vijana," - Mussa Azan Zungu

View attachment 2894963

Credit-EastAfricaTv
Lema alisema ni laana hiyo biashara
 
Tatizo siasa za hovyo zimeiharibu hii nchi.

Zungu ameongea ukweli hawa vijana wa boda boda ni tatizo kubwa sana mabarabarani wanatakiwa kudhibitiwa kwa sheria kali mno ili waheshimu sheria za barabarani.
Tatizo RUSHWA huyo aliepewa dhamana ya kusimamia ndio kwanza anajenga kupitia bukubuku zao
 
Kwanza ni bodaboda wangapi wana leseni za udereva, hilo tu serikali imeshindwa kufuatilia. Hii nchi yetu kila kitu kinajiendea tu.

Vijana wengi katika hii ahira wamekuwa wanywa smart gin, hali inazidi kuwa mbaya.
 
"Suala la bodaboda ni kero kubwa sana na hasa katika utumiaji wa sheria za barabara, mimi ni mtetetezi mkubwa sana wa bodaboda lakini matumizi yao kwenye barabara yanakatisha tamaa lazima muwe na mkakati maalum wa kudhibiti ajali wanazozifanya na lazima muwe na sheria kali za kuwadhibiti na hata kuwasimamisha, sababu ukienda MOI sasa hivi asilimia 90 ni vijana," - Mussa Azan Zungu

View attachment 2894963

Credit-EastAfricaTv
Nilishaacha kupanda boda kitambo; bora nichape lapa!
 
Ila kiukweli kunahitajika mkakati madhubuti kwa hawa vijana. Aisee ajali ni nyingi. Halafu wengi wao hawafuati kabisa sheria za usalama barabarani.

Wanaendesha bila tahadhari na wala hawajihurumii na kuwahurumia waliowabeba.

Ukiangalia statistics ya vifo vinavyotokana na boda boda hali inatisha.

Kuna rafiki yangu ni Daktari pale KCMC huwa ananiambia kila week lazima wapate mtu aliyepata Ajali ya boda boda iwe amejeruhiwa au kupoteza maisha.
 
Back
Top Bottom