Naibu Spika Tulia: Musukuma usiaminishe wanafunzi kuwa elimu ya darasa la 7 ni bora kuliko elimu ya juu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,568
108,911
Naibu Spika Tulia Ackson amemkosoa Mbunge Wa Geita Vijijini Joseph Msukuma, kuacha kuaminisha wanafunzi kuwa elimu ya darasa la saba ni bora kuliko elimu ya juu kwa kuwa Serikali inajitahidi kuboresha shule kwa ajili yao na hivyo ni muhimu kuwahamasisha kusoma kuliko kuwakatisha tamaa.

Naibu Spika ametoa kauli hiyo baada ya mbunge Msukuma kuchangia bajeti ya Wizara Ya Ulinzi na kutoa maoni kuwa JKT isiweke kigezo cha elimu na badala yake hata wenye elimu ya darasa la saba wachukuliwe kupewa mafunzo ya jeshi hilo.

Chanzo: Nipashe Online

Hayati wenu alimuharibu sana huyu Mpuuzi kwa Kumlea na Kumdekeza huku akijua ni Mpuuzi na hata hana Sifa za kuwa Mbunge kama alivyo sasa.

Yaani kwakuwa eti GENTAMYCINE sijasoma au ni masikini ndiyo niwadharau na niwachukie waliosoma sana na wenye Pesa ( Utajiri ) sana?

Na kwa Hasira alizonipandisha huyu Mbunge wenu Mpuuzi namshauri Mabadiliko ya Katiba yafanyike haraka sana nchini na Mgombea Ubunge yoyote nchini lazima awe na Elimu ya kuanzia Shahada ya Kwanza ili Mimi na Mangumbaru ( Wajinga ) wenzangu ( akiwemo na huyu Mbunge ) tulioishia Darasa la Saba tutafute Kazi zingine za Kufanya ambazo naamini ziko nyingi tu.

Kuna Vitu vinaboa na kukera sana tu.
 
Ndugai anawapa muda sana wa kuongea hawa wehu hasa Msukuma ndio anatumika kuwatukana mpaka wasomi Bungenim muangalie mzee Kishimba hana makuu na mtu yule mzee japo elimu yake ni chache ila analia sana na mfumo wetu wa elimu. Sio huyu mvuta mmea MPush
Nashukuru GENTAMYCINE sipo Bungeni ila kwa ninavyojijua na nisivyopenda Upumbavu ningekuwa nae karibu huyu Mpuuzi ningemuonyesha kuwa Kwetu Mkoani Mara ( Musoma ) kwa Wanamume na Mashujaa hatuishii tu Kuivuta kama afanyavyo Yeye Mpuuzi Mmoja, bali pia tunaisongea katika Ugali wa Ulezi, Mtama na Muhogo hadi kuiweka katika Mboga na Kuila yote tu.
 
Nashukuru GENTAMYCINE sipo Bungeni ila kwa ninavyojijua na nisivyopenda Upumbavu ningekuwa nae karibu huyu Mpuuzi ningemuonyesha kuwa Kwetu Mkoani Mara ( Musoma ) kwa Wanamume na Mashujaa hatuishii tu Kuivuta kama afanyavyo Yeye Mpuuzi Mmoja, bali pia tunaisongea katika Ugali wa Ulezi, Mtama na Muhogo hadi kuiweka katika Mboga na Kuila yote tu.
Kumbe njia moja na mm
 
Msukuma alishajifanya mtetezi wa watu walioishia darasa la saba, utafikiri kaingia humo bungeni kama mbunge wa viti maalumu kuwakilisha hao watu. Naunga mkono hoja ili kuondoa mediocre minds kama za akina msukuma na kibajaji mbunge awe na elimu ya kuanzia shahada...
 
Hakika mbunge Musukuma anafikirisha sana kutokana na mambo anayoyapigia mbiu bungeni. Alimdhalilisha Professor Muhongo na hakuna aliyemtetea bungeni. Professor Muhongo aliyeeelimisha waTZ kuhusu umuhimu na matumizi ya gesi asilia, aliyetuelimisha kuhusu umuhimu wa madini mengine nje ya tuliyoyazoea. Akilieleza taifa kuwa yapo nchini nje ya tuliyoyazoea na yana soko duniani. Pia aliboresha sekta ya madiji na nishati ajiwa waziri.
HAPANA hakumtendea haki Prof Muhongo na naona amemvunja nguvu kisaikolojia.

Mbunge Msukuma kazoea sana kuwadhalilisha wasomi. Kwenye halmashauri anayotoka wengi amewavunja moyo aidha kwa kuwafukuzisha kazi au kuhákikisha wanashushwa vyeo. Sasa kaanza kuambukiza tabia hii kwa halmashauri jirani km Sengerema. AHSANTE KWA KUANZOSHA UZU HUU KUHUSU MBUNGE MSUKUMA.Á
 
Back
Top Bottom