Naibu Spika: Bunge litapitia Kanuni za Tozo za Miamala zilizoandaliwa na Waziri wa Fedha kuona kama hazikiuki Sheria!

Naibu Spika Dr Tulia Ackson amesema bunge litazipitia kanuni za sheria ya tozo za miamala ya simu zilizoandaliwa na waziri wa fedha ili kujiridhisha kama hazikinzani kazi itakayofanywa na kamati ya sheria ndogo ya bunge.

Endapo itaonekana kanuni ziko sawa basi sheria itapelekwa kwenye bunge zima

Source: ITV habari
Lini ataziondoa??
 
Naibu Spika Dr Tulia Ackson amesema bunge litazipitia kanuni za sheria ya tozo za miamala ya simu zilizoandaliwa na waziri wa fedha ili kujiridhisha kama hazikinzani kazi itakayofanywa na kamati ya sheria ndogo ya bunge.

Endapo itaonekana kanuni ziko sawa basi sheria itapelekwa kwenye bunge zima

Source: ITV habari
Mmmhgh wanataka wambebeshe MTU mzigo wa dhambi
 
Nchi hii bana. Madelu na Ndugulile si walisema wmeagizwa na Samia wazipitie upya hizo tozo?

Maza anaagiza tuuuu huku alirembua macho badala kutoa decisive guidance na directions with clear timelines. Huyu hawezi na wala hafai kuwa Amiri Jeshi Mkuu
 
Tulia yupo sawa. Sheria hutungwa na bunge, ila kununi/Sheria ndogo hutungwa na waziri wa wizara husika
Mwigulu alituambia kwamba sheria imetungwa na bunge siyo yeye, na kwa kuwa imetungwa na kupitishwa na bunge hakuna wa kubadilisha kitu
 
Siku zote alikua anafikiria kusema neno hilo tu? au amewashwa ndo ikabidi neno hilo limtoke?
Ujinga wa viongozi wetu ni mzigo kwa wananchi.
 
Lakini walipitisha mapendekezo ya bajeti yenye mapendekezo hayo ya tozo?
Ndiyo. Wao walipitisha Sheria kwamba tozo iwepo ila Sheria yenyewe inampa waziri wa fedha mamlaka ya kutunga kanuni ambazo, pamoja na mambo mengine, zinaainisha kiwango cha tozo
 
Nchi imekua vururu vururu, bunge la chama kimoja ni baya sana kwa Ustawi wa nchi. Tulia ulikua mstali wa mbele kuhakikisha bunge linakua la MACCM peke yenu, Ona sasa kikowapi cha maana mnafanya, zaidi ya kujambiana tu bungeni.
Mwigilu anasema bunge mmepitisha mawazo yake kuwa sheria.
leo tena ndio mnakumbuka kuangalia baada ya kupitisha.
Mnatuonea sana watanzania
 
Back
Top Bottom