Nahitaji passport ya kusafiria haraka iwezekanavyo

Nahitaji passport ya kusafiria haraka iwezekanavyo

Big Nyota

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2018
Posts
558
Reaction score
948
Wakuu wasalaamu!!

Kama kichwa kinavyojieleza nimepata safari ya haraka sana, sasa nimepitia nyuzi mbalimbali kuhusu kuchelewa kwa passport na usumbufu uliopo uhamiaji hasa ukiwa mkoani.

Ipo hivi nilianza kufatilia passport mwanzoni mwa mwezi wa 3 nikiwa mkoa A lakini cha ajabu nilikuwa nikienda ni mwendo wa kuzungushwa tu mara mtandao unasumbua, mara njoo kesho tuangalie, nikajaza fomu lakini wapi naishiwa kuambiwa subiri wiki ijayo.

Nina safari mwezi wa 5 tarehe moja na mdhamini wangu amechachamaa kwelikweli ananiona mzugaji tu.

Sasa nimeamua niende Dar nikafanyie process zote palepale Uhamiaji Kurasini, hivyo naomba msaada kwa mwenye namba za mtu mjanja anayeweza kunifanyia mchakato nikapata passport ya express ndani ya siku moja au mbili niwe nimeipata bila usumbufu maana nimemuandalia posho yake kabisa.

Cc Mshana Jr
Isanga family
[USER=30674]kalaga Baho
Nongwa
ZEE LA JIJI
Evelyn Salt
Smart911
[USER=127896]mwashamba
 
Nenda office za uhamiaji na barua ya dhumuni la safari,na nyaraka zinginezo huku utakutana na vishoka tu mwisho wakutapeli pesa zako
Kivipi mkuu nifungue maana hilo neno vishoka sio geni kwangu, kwamba nao ni maafisa wa uhamiaji lakini wanakutapeli tena??
 
Back
Top Bottom