Preta mi nafkiri jamaa amemaanisha kuwa ni KAAAAZI KWELI KWELI.
Anyway, hizi nyimbo kwa kweli hata mi nilipata wakati mgumu mno kujua zinaitwaje kwa kweli.
Ni hizi nyimbo za vitoto vya siku hizi vya kihuni. Wenyewe wanaita nyimbo sjui za vigodoro kama skosei. Sjui ni nyimbo za mahadhi gani aisee, na hata maneno wanayotumia humo mmmmh, acha tu.
Sioni ladha ya kuskiliza hizi nyimbo kwa kweli kwanza hata temple (speed) ya nyimbo zenyewe tu jinsi zinavyoenda kwa kweli acha tu.
Vijana wa sasa huwaambii kitu kwa hizi nyimbo niliuliza juzi ndio nikaambiwa zinaitwa hivyo sjui ni something like SENGELI au SINGELI watajua wenyewe, na nafkiri hii kitu wameasisi toka kwa MSAGASUMU.
Kuna katoto kamoja hapa mtaani kenyewe kanasema kuwa kamerekodi nyimbo kama 20 hivi nikawauliza mnarekodi vipi wakasema elf 5 unarekodi nyimbo 3 i was like (whaaaaat) ?, wakasema wanarekodia sjui virtual dj by looping any beat.
Ngoja wadau wataweka hapa hizo nyimbo mleta mada ngoja waje wenye nazo sjui wamelala saa hizi maana ni watu wa vigodoro na hata wa bodaboda nawaskia wakizipiga siku hizi, nasubiri ziingie kwenye KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS.