Nahitaji msaada wa mawazo ya biashara/ujasiriamali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahitaji msaada wa mawazo ya biashara/ujasiriamali

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Mbavu za Mbwa, Feb 5, 2012.

 1. M

  Mbavu za Mbwa JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Mtoto wa kaka yangu alifeli kidato cha 4. Nataka nimfungulie ofisi. Je, kati ya saluni ya kiume na biashara ya mitumba ipi inalipa vizuri? Kiasi ninachotaka kumpa ni Tsh 3,000,000/. Na kama mtaona(wana-jf) kuwa labda hicho kiasi hakitoshi, naomba mnipe wazo mbadala ili tumuokoe kijana huyu. Maana amekosa uelekeo kabisa.
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Kwenu wapi? yaani sasa hivi mnaishi wapi au mko wapi?
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Pole mbavu za mbwa kwa kufeli form 4 ila sio kwamba umefeli maisha sikushauli ufungue saloon au mitumba,kwanin usiinvest kwenye kilimo cha mpunga? Tafuta heka 20 za kukodi morogoro(laki 4) kulimisha heka moja ni elfu 30 kwa trekta(laki6) kupanda kwa heka 1 ni elfu20(laki4),kulitunza na mengineyo elfu40 kwa heka(laki 8) ukipiga total ni kama mil2.2 hiyo laki nane unahija kama balance ya chochote kitachotokea kwa miezi 6 hadi 7 unavuna kwa heka 20 utapata magunia ya mpunga 160 hadi 180 na ukikoboa na kupata mchele utapata gunia 128 hadi 144 eavarage magunia 136 na gunia moja dar ni sh laki mbili sasa piga laki mbili mara 136 unapata ngapi? Unapata milion 27.2 upo hapo?
   
 4. M

  Mbavu za Mbwa JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Kwa sasa tupo Moshi mjini, mkuu Malila
   
 5. Senior Boss

  Senior Boss JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 3,285
  Likes Received: 2,025
  Trophy Points: 280
  This is a Brilliant idea....tena uki export ts worth more than dat !!!
   
 6. M

  Mbavu za Mbwa JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  thanx. Ni katika wilaya gani hapo morogoro? Ni wazo zuri.
   
 7. M

  Mbavu za Mbwa JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Kwa sasa tupo Moshi mjini, mkuu Malila
   
 8. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Kilombero
   
 9. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #9
  Feb 7, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  wakuu samahani kama nitatofautiana na nyie,

  Katika swala zima la biashara si kitu cha mchezo na biashara ni hoby wakuu

  - JAMAA LAZIMA KWANZA AKAE CHINI NA DOGO AMFANYI MTIHANI WA KUMUASES, KUNA MASWALI MENGI SANA YA KUMUULIZA KWANZA KABLA YA KUMINGIZA DOGO KWENYE BIASHARA LA SIVYO UNAWEZA MUANZISHIA BUSINESS KUMBE YEYE HUKO HAYUKO KABISA.

  MASWALI MUHIMU SANA YA KUMUULIZA HUYO DOGO

  1. JE AMEJIANDAA KUTUMIA MUDA MWINGI SANA NA PESA KATIKA BIASHARA?

  2. JE ANATAKA BIASHARA YA AINA GANI?

  3. BIASHARA ANAYO IPENDA ANGEPENDA ITOE HUDUMA IPI AU PRODUCT IPI?

  4. KWA NINI ANAPENDA BIASHARA? KWA NINI ANZISHE BIASHARA?

  5. ATATAGETI SOKO/MASOKO YAPI ENDAPO ATAANZA BIASHARA?

  6. JE ANAFAHAMU KATIKA BIASHARA ANAYO PENDA KUNA WASHINDANI WAPI?

  7. BIASHARA ANAYO IPENDA ITAKUWA NA UTOFAUTI UPI NA ZA WENGINE?

  8. NA AKIANZA HIYO BIASHARA ITAMCHUKUA MUDA GANI HADI HIYO BIASHARA YAKE IWE IMESIMAMA YENYEWE NA KUJULIKANA?

  9. ANA HITAJI PESA KIASI GANI?

  10. ZAIDI YA KUMPA MTAJI JE ANAFAHAMU NJIA NYINGINE ZA KUFAINENSI BIASHARA YAKE? ANAFAHAMU SOURCE ZINGINE?

  11. MUULIZE KAMA ATAHITAJI NA MKOPO AU LA

  12. MUULIZE ATATUMIA NJIA IPI KUPANGA BEI YA HUDUMA/PRODUCT ZAKE UKILINGANISHA NA WASHINDANI WAKE?

  13. MUULIZE ATAITANGAZAJE BIASHARA YAKE?

  14. ATAWEZAJE KUIMENEJI BIASHARA YAKE? ATATUMIA NIA ZIPI KUIMENEJI?

  15. WATU WATAKAO KUWA WANAMSAIDIA KWENYE BIASHARA ATAWAPATA VIPI? JE ATAKUWA AKIWALIPA?

  16. JE IKITOKEA TRA,BOT AU SEHEMU NYINGINE WAMEKUITA UKAFANYE KAZI UTAENDA? HAPA UNAMPIMA KAMA KWELI YUKO SIRIASI NA UNACHO MUANZISHIA

  HAYO NI MACHACHE MKUU ILA SWALI LA MUHIMU KULIKO YOTE LA KUMUULIZA MTU YEYOTE UNAE MU ASESE KABLA YA KUMFUNGULIA OFISI NI HILI

  1. Je kuna tofauti gani kati ya yeye na biashara yake ? muullize kama kuna tofauti au la
  2. Kwa nini huwa biashara ina pewa jina?
  3. Akipata pesa nyingi angependa kufanya nini? swali la mtego sana hili
  4. Je ndugu zake, marafiki zake na kazalika atawasaidi vipi wakati atakapo kuwa anaendesha biashara yake?
  5 . Pesa ya yeye kutumia atakuwa anaipata vipi kipindi biashara ikiwa bado changa?


  WAKUU BIASHARA SI SWALA LA MCHEZO NA TUSIKULIPUKE NA KUWAANZISHAI NDUGU/MKE/MME BAIASHARA BILA KUWA ASES KWANZA, WATU WENGI HUWA WANAJUTA BAADAE

   
 10. M

  Malila JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Kulima kama huna abc za kutosha ni mtihani wa pili huo,ninaposema kulima nina maana inabidi atoke Moshi aende mikoa jirani,kwa sababu hapo Moshi ardhi ni tatizo. Kama anaweza kujifunza ufugaji wa kuku na swine basi aende huko, na pengine aifanye shughuli yake rasmi ili imtoe, vinginevyo kumpa shughuli ya kuzugia itakuwa mnapoteza muda bure. Muda unakimbia si mchezo, huu sio wakati wa kujaribisha mambo.
   
 11. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280

  Analysis na business ideas kama hizi ni nzuri sana sometimes, lakini inategemea sana ukubwa wa biashara. Wajasiriamali wengi waliofanikiwa wamepita njia za tofauti na hii (wengi ni risk takers) hawafanyi critical analysis, kwa wachache ninaowafahamu. Si wengi ni wajuzi wa business plan kama hiyo hapo juu. By the way thanks for your good ideas
   
 12. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  katika ulopendekeza ..nguo mtumba utamtoa... Milioni na nunsu anaweza kuanza
  -auchukue moshi (grade A, B na C) aulete Dar... awe makini katikakuchagua wasimuingize mjini.. 300000 hadi 400000 anapata robota bomba
  -Atafute fremu eneo zuri au aingie ubia na wenye frem katika maeneo yenye mzunguko wa watu hapa dar (mwenge, ilala, kinondoni etc..).. ajipange na gharama ya eneo
  -Grade ya mwisho itembee na machinga mkononi... achukue buku 2 hadi 3 tu kwa kila nguo itakayouzika (atawapata wengi tu)..atarudisha gharama karibu yote ya kazi na faida kiasi ..
  -gredi A &B aiweke kwenye fremu... finyia uchunguzi bei.... hii ni faida zaidi..

  Nimeshea uzoefu na nilioupata kwa mtu anaefanya hii bishara. changamoto ni kupata mali safi, nidhamu ya biashara, uelewa wa sko la mtumba na fedha...

  Kazi ni kwako..
   
 13. S

  Shadya Member

  #13
  Feb 7, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mkeshahoi nisaidie basi nipate mawasiliano ya wanaouza hizo grd A za mitumba nifanye biashara na mimi huwa naitaka ila sijui wapi pa kupata mali safi
   
 14. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #14
  Feb 7, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280

  Mimi nilijaribu kuonyesha kwamba kabla ya kumuanzishia mtu biashara lazima umfanyie assesment kwa sababu huwezi jua yeye anataka nini,

  Mleta maada amesema anataka kumfungulia Dogo Ofisi so nimejaribu kumshauri amfanyie asesment kwanza, kwa sababu biashara si kitu cha mchezo na huwezi force mtu kuwa mfanya biashara, kama yeye hataki unamfungulia then baada ya muda utakuta maefunga kisa ndo kama hivyo
   
 15. T

  Tall JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Si wezi kuinvest pesa yangu kwenye kilimo. Kuna risk nyingi sana. Je umepatana na mungu kuwa mvua itanyesha???
   
 16. m

  muvimba Member

  #16
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 20, 2008
  Messages: 76
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  mpe mtaji aweze kulima kilimo cha muogo kwani kuna soko kubwa sana kuanzia june 2012
   
 17. bulldoza

  bulldoza Senior Member

  #17
  Feb 8, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Malila inawezekana kunipatia elimu ya ufugaji wa swine?napenda kujua do &dont za hii kitu au kama hapa haikubaliki tafadhali hata kwenye pm.
   
 18. G

  Gabriel william Member

  #18
  Feb 4, 2013
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nisaidien namba ya hao wanaochyukua bidhaa safi
   
 19. Job Richard

  Job Richard Member

  #19
  Feb 8, 2013
  Joined: Feb 8, 2013
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo patamu maisha popote
   
 20. chash

  chash JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2013
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Huyu mtoto mtafutie kozi ambayo inamfaa na ambayo anaweza kufikia hadi diploma au zaidi aendelee na masomo. Inaweza pia kuwa kozi ya ufundi fulani. Baada ya hapo utamfungulia biashara inayo endana na ujuzi wake. Worst case scenario ni kufeli biashara later in life na kutokuwa na kitu cha ku-fall back to wala ujuzi wa chochote.
   
Loading...