Kubota
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 532
- 1,089
Mtoto wa kaka yangu alifeli kidato cha 4. Nataka nimfungulie ofisi. Je, kati ya saluni ya kiume na biashara ya mitumba ipi inalipa vizuri? Kiasi ninachotaka kumpa ni Tsh 3,000,000/. Na kama mtaona(wana-jf) kuwa labda hicho kiasi hakitoshi, naomba mnipe wazo mbadala ili tumuokoe kijana huyu. Maana amekosa uelekeo kabisa.
Biashara ni Elimu. Wengi wetu hunachukulia siku zote kufanikiwa kwenye biashara ni kama ngekewa hivi! Kumuingiza kijana kufanya biashara bila kuyajua vema mazingira ya biashara itarajiwayo lazima mwanzo apige mieleka mingi tu maana anakuwa anajifunza kwa makosa! Asipokuwa mvumilivu anabwaga manyanga.
Ushauri wangu mkishakubaliana nae juu ya aina ya biashara atakayoipenda yeye mwenyewe, mwombee akajishikize kwanza awe kama msaidizi kwenye hiyo kazi iwe ni saluni, mgahawa, kilimo au mitumba! Akajishikize kwanza miezi 3 hadi 6 hata kama ni kwa kujitolea au kwa yeye kulipia kitu kidogo! Huu ni mtazamo ambao wengi hawajauchangamkia. Atakapokuwa amejishikiza atajifunza mambo mengi sana kiasi kwamba utakapoamua sasa akasimame mwenyewe hiyo aina ya biashara uhakika wa yeye kusonga mbele utakuwa mkubwa. Ndiyo maana Mkuu Chasha alishadokezea kuwa, mtu mwenye taaluma fulani ni rahisi kufungua biashara kulingana na taaluma yake maana anajua mambo mengi yanayoendana na kitu hiyo.