Nahitaji Kujiunga na upadre

Nahitaji Kujiunga na upadre

Itakuwa ngumu sana, umri umeenda mno! Hapo utaenda ukashauriwe uwe Buruda "Brother". Wale ambao hawajapitia seminari mara nyingi wanachukuliwa wanapomaliza form IV au Form VI. Na hapo unawakuta wako kwenye age ya 20-22. Kwako mkuu itakuwa ngumu sana! Jaribu kwa Paroko ukasikie atakupa majibu gani!!
Hao brother wanakuwaje mkuu?? Wanafanya ishu gani??
 
Kama unataka kiwa padre na hujui mashirika ya kimisionari mpaka sasa....usijihangaishe.
Nakushauri ujiunge na CCM tu.
Mashirika nayajua sema ndo ya kuyatafuta sana na tochi ishu zao , kama holly cro, apostel of jesus, jesuit na mengine kibao
 
Yaani maswali kama haya anatakiwa apate mtu anayesomea komunyo ya kwanza, ila kwa kuweka rekodi sawa, sakrameti ni kama ubatizo, kitubio, ekaristi, kipaimara, daraja takatifu, mpako mtakatifu, ndoa,%¢ alama za kanisa ni 1, takatfu, katoliki, la mitume na misionari.×...daraja takatfu ni kuwekwa wakfu kwa ajili ya kazi ya Mungu,× ushirika wa wataktifu ni uhusiano uliopo kat ya roho za watu waliopo mbinguni, toharani na duniani,√ nadhani nimekujibu
Katika majibu yako umepata jibu moja tu la mwisho. La kwanza umokosea mpangilio; huwezi ukaulizwa hatua za ukuaji ukajibu , (Kutembea,tambaa,mimba,simama n.k)
Inabidi uanze mafundisho kwanza kanisani hufai kuwa padre wewe! Haiwezekan maswali matano upate moja tena Kwa Ku "Google"
 
Kama nimekosea hapo ww utakuwa mdau wa SDA maana ndo mnapambana na ukatoliki
 
Kama nimekosea hapo ww utakuwa mdau wa SDA maana ndo mnapambana na ukatoliki
Kama unataka kumtumikia Mungu jaribu hata kuwa kwayamaster kanisan, lakini upadre huna wito huo na baadhi ya mafundisho umeruka ambapo hutapokelewa! Endapo ukifosi ukawa padre baadae utakumbuka maneno yangu kwamba hufai, kwasababu utasoma halafu ufukuzwe mwaka Wa mwisho Wa malezi uwe kama Deo kisandu!
Kama kweli unataka kumtumikia bwana jaribu ukwaya master n.k
 
Yaani maswali kama haya anatakiwa apate mtu anayesomea komunyo ya kwanza, ila kwa kuweka rekodi sawa, sakrameti ni kama ubatizo, kitubio, ekaristi, kipaimara, daraja takatifu, mpako mtakatifu, ndoa, alama za kanisa ni 1, takatfu, katoliki, la mitume na misionari....daraja takatfu ni kuwekwa wakfu kwa ajili ya kazi ya Mungu, ushirika wa wataktifu ni uhusiano uliopo kat ya roho za watu waliopo mbinguni, toharani na duniani, nadhani nimekujibu
Mdogo'angu tayari umesha-fail mtihani mmoja mdogo sana,kipengele cha hekima na busara pia una kitu kujikweza{mtu akikusoma katikati ya misatari ataelewa nilichomaanisha}.jibu lako hiyo sentence ya mwanzo haikutakiwa iwepo ilikuwa ni kiasi cha kuanza kujibu tu maswali uliyoulizwa.angalia kama utapata nafasi una la kujifunza ktk kujirekebisha
 
Kama kwel unania nenda kamuone paroko wa parokia unaposali atakwambia nini chakufanya, haijalishi kama umepita seminari au laa ,kabla ya kuanza masomo lazima upite nyumba ya malezi utakaa kwa miezi6 au mwaka uone kama kwel utaweza kuendelea na hatua inayofata
 
Mkuu inaonekana una maarifa na hizi mambo embu toa experience mkuu, maana najua humu watu wa kila idara wapo
Uwe tayari kutumika kwa hasara ya duniani yaani pasipo faida za kidunia. Ikiwa unayaweza basi jikane mwenyewe na uuchukue msalaba wako ili umfuate Kristo.
 
Mdogo'angu tayari umesha-fail mtihani mmoja mdogo sana,kipengele cha hekima na busara pia una kitu kujikweza{mtu akikusoma katikati ya misatari ataelewa nilichomaanisha}.jibu lako hiyo sentence ya mwanzo haikutakiwa iwepo ilikuwa ni kiasi cha kuanza kujibu tu maswali uliyoulizwa.
Asante sana mkuu! ...HAFAI kuwa padre hata kidogo, ana mikogo ambayo akihudhuria malezi sijui hata kama ataufikia ushemasi hajafukuzwa!
Lakini Kwa kutambua mikogo yake nimemshauri awe kwaya master maana hao ndio wanakuaga na mikogo
 
Uwe tayari kutumika kwa hasara ya duniani yaani pasipo faida za kidunia. Ikiwa unayaweza basi jikane mwenyewe na uuchukue msalaba wako ili umfuate Kristo.
Nipo tayari mkuu, mi nishakataa kila kitu kwa ajili ya bwana Yesu
 
Asante sana mkuu! ...HAFAI kuwa padre hata kidogo, ana mikogo ambayo akihudhuria malezi sijui hata kama ataufikia ushemasi hajafukuzwa!
Lakini Kwa kutambua mikogo yake nimemshauri awe kwaya master maana hao ndio wanakuaga na mikogo
Hahahhahahha duh sio kwa tabiri hizo mkuu, hapa watu wengi wazinguaji ndo maana tunajaribu kukopu nao, ndio maana tunatafuta shirika kama jesuit ambalo linataka mtu anayeweze kuenenda na mazingira vizuri
 
Ni msaada mkuu, siunajua unakuwa unapitia mambo mengi mpaka unajitambua mkuu??
sasa hayo mambo mengi huko kwenye upadre hawataki..wanataka kijana wanae mkuza wenyewe....ndio maana kuna seminary zao..wanaanza nao kuanzia sekondary...wanawamonitor mpk wakienda likizo huripoti kwa maparoko wao...
sasa wewe umeshafika miaka 24 mtu mzima...ushachelewa
 
Kama kwel unania nenda kamuone paroko wa parokia unaposali atakwambia nini chakufanya, haijalishi kama umepita seminari au laa ,kabla ya kuanza masomo lazima upite nyumba ya malezi utakaa kwa miezi6 au mwaka uone kama kwel utaweza kuendelea na hatua inayofata
Ni sawa kabisa mkuu, nikajipimie mwenyewe au so
 
sasa hayo mambo mengi huko kwenye upadre hawataki..wanataka kijana wanae mkuza wenyewe....ndio maana kuna seminary zao..wanaanza nao kuanzia sekondary...wanawamonitor mpk wakienda likizo huripoti kwa maparoko wao...
sasa wewe umeshafika miaka 24 mtu mzima...ushachelewa
Kwa elimu yangu na huo umri kwa tz ni sawa tu maana wanachukua hadi miaka 35 mkuu
 
Back
Top Bottom