Nahitaji kubadili dini ili nioe

Nahitaji kubadili dini ili nioe

sawa nitamkazania abadili but nahtaj maombi haswa, kutokana na hali ya wazazi wake

Wewe kama bint anakupenda wazazi huwa hawana uamzi wowote, kama vipi vuta kwanza mzigo ndani halafu mengine yatafuatia, kubadili dini sawa lakini zalau za demu zitaanzia hapo ujiandae kuwa bushoke.
 
Kama kweli umesoma uislam utakua unajua maana ya MURTAD, labda nikusaidie na nitimize wajibu wangu

1. unaachana na kalima ya Laa ilaha ila llah... ( hakuna Mola apaswae kuabudiwa ila Mola/Mungu mmoja) sasa unatamani kuabudu miungu zaidi ya mmoja..... madhara ya kufanya hivyo unayajua

2. Kumbuka siku ya mwisho,, Qiyama,, mapenzi yako hayatakufaa kitu,, mbele ya Mola utasimama peke yako na utakua huna hoja kabisa kama ulimkadhibisha Allah

3. Mapenzi huisha kabisa ,,,, je ukisuswa utarudia dini yao ya zamani?? ingekua vyema kubadili dini kwa kuielewa dini husika lakini sikwa tamaa ya mwili


Nakushauli kabisa kijana wangu kuwa strong,, wanawake hupenda watu strong,, ukikubali kubadili huo ni udhaifu mkubwa sana na hata ku value kabisa .....

sawa mkuu, ushauri wako naufanyia kazi na nimekuelewa yote
 
By Makosakuumbwa
Kama unabadili dini kwa ajili ya Mwanamke sikushauri ila kama kwa ajili ya imani fanya hivyo. Utakuja kujuta maisha yako yote utapoteza ndugu na baadae mkeo.

Tahadhari iliyowekwa na huyu mdau hapo juu ni ya muhimu sana kama unakidhi tekeleza. Na kwa nyongeza, kama kweli huyo mwanamke amekuvutia kiasi hicho cha kutaka kubadilisha dini, basi ni bora ukaichunguza kwanza hiyo dini kwanza ukiridhia uijifunze, ukiielewa na kuikubali ndio ubadilishe. Jambo la mwisho kabisa liwe ni kuoa.
 
walioko ndani wanataka kutoka na walio nje wanataka kuingia!
 
Katika kupokea ushauri wa hapa zingatia yafuatayo:
Kunawanotumia busara,
Kunawanao consider uzoefu wa yalotokea,
Kunawanaoendeshwa na mihemko ya kidini..so kuwa mbayuwayu
 
Badili umuoe fasta, chelewa chelewa utakuta mwana si wako! Kumbuka mnaomwania huyo msichana mpo kadhaa, haupo peke yako. Utaumia sana roho ukija kupata taarifa kuwa uliyepanga naye kuishi pamoja amechukuliwa na mtu mwingine!
 
mwanaume habadili dini.sababu ya mwanamke,mwanamke ndio anabadili.sasa ukishabadili dini umfate mkeo kwa baba ake uishi nae huko.yani hata baba mkwe atakuona we lofa
 
Tokeahapo wewe c muislam na wala uislam huujui ni mtoto wa mitaani huna malezi ya kislam
 
Dini ilikuharibu, 23yrs unafikiri kubeba majukumu ya Mtu 30yrs.
Unajua nini kutunza familia?
Unajua kulea watoto?
Unajua kulea mimba?
Je, uchumi wa familia yako unayotaka kuanzisha ni tegemezi kwa asilimia ngapi?
Dini yako imekufundisha kukwepa Zinaa....!!!
Ngono kwa sana,
Usisahau kuuliza, nini baada ya kukwepa xxx?

Kijana Amka
Maisha yako yako mikononi mwa MAAMUZI yako na sio DINI AMA WAZAZI.....!!!
Wazazi watakufa na kukuacha...!!
DINI itakuacha.....!!
DINI itakuhukumu kwa sababu imekuacha...!!!

LAKINI , Dhamiri yako na Roho yako itabaki MUNGU WAKO ATAKUWA NA WEWE MILELE.

Wako wengi watakutisha na Dini zao Wazazi, Ndugu.

Lakini, niviumbe kama ulivyo wewe
Watakuangamiza ufanane na wao.

Wewe ni Kiumbe sahihi na chenye MAAMUZI kamili. FULL STOP
 
Fanya haraka badili dini utakuwa umepata mambo mawili kwa wakati mmoja.

Mosi utakuwa umepata mke umpendae

Pili utakuwa na uhakika wa kwenda mbinguni.
 
Sawa, jaribu kuuliza waliofunga Ndoa wakupe cheti cha Ndoa. Tafuta neno bila shuruti.
HICHO NDIO CHETI.
 
Back
Top Bottom