Nahisi nimetapeliwa sijui nifanye nini?

Nahisi nimetapeliwa sijui nifanye nini?

Habar za humu wanajamvi? Ilikuwa siku ya jumamosi natoka kwenye harakati za vikao na clients wangu basi nikapita pale mwenge mpakani kulikuwa na mnada wavitu wakidai muuza duka alichukua mkopo kashindwa rejesha so vitu vya dukani vikawa vinapigwa mnada.
Basi pale nikaona simu aina ya IPhone 11 Pro max ambayo bei zake huwa ni 1.7m dukani,basi nikaikagua ile simu nikaona kama ipo poa basi nikatamka offer yangu 500,000tsh nikachukua baadae nafika home nakuta sio IPhone kabisa bali wameweka os inayoendana na iPhone isee nilichoka. Sasa je ninaweza kwenda kwenye mamlaka gani inisaidie nipate hela yangu maana hapo nimetapeliwa. Nina risiti ya efd na ya kawaida
Umbwa kala umbwa 🤣🤣🤣🤣
 
Matapeli hawaishi na wajinga pia hawaishi.
Jana wife kapigwa 760,000 kwenye laini za miamala na wale jamaa wanaoipigaga simu.
Yaani licha ya kumpa elimu yote huko nyuma kuwa asije akajaribu kuelekezwa kitu na akafanya kwenye simu za miamala bado alinasa tu.
Hv kalazwa yuko hospitali yaan hasara mara 2.
Damn Dunia ni chungu hii wakat mwingine

Aisee
 
Unahisi umetapeliwa au umetapeliwa mkuu.

Hata hivyo wao walikuuzia ile simu uliyoishika ukakagua na uzuri ulitamka mwenyewe ofa ya laki 5. Wewe ndio uliamua kuiita iphone 11 pro wenyewe walikuuzia ile uliyoinunua kwa laki 5 ambayo ukiwafuata saa hizi watakupa jina lake vizuri tu
Du nimecheka kweli.
 
[emoji23][emoji23] kinacho nichekesha ni hapo unaposema "unahisi umetapeliwa" yani Licha ya kuwa umetapeliwa lakin bado hauamini kama umetapeliwa
Hakuna mtu nayetapeliwa anakubali mapema kuwa ametapeliwa. Jamaa aliwekewa vipande vya mbao badala ya simu na alipofungua akaona ni mbao akabaki kuigeuza geuza karibu robo saa kama haamini macho yake huku anasema du wameniwekea dawa nini?
 
Back
Top Bottom