Masikini_Jeuri
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 6,827
- 1,310
Kwanza inabidi mzielewe sheria za uhamiaji za Marekani. Kama huzijui na kuzielewa ni rahisi sana kunilaani mimi na kuniona zumbukuku niliyejitakia yaliyonitokea. Jamaa alikuwa deported kutoka Marekani. Ukiwa deported kutoka Marekani unapigwa marufuku kurudi kwa miaka kadhaa, kama sijakosea (sina hiyo sheria hapa kwenye makabrasha yangu lakini inasema hivyo.)
Pili, hakumtekeleza huyo mama mtoto wake. Kwani hata baada ya kuwa deported jamaa aliendelea kumhudumia kifedha huyo mdada na hata mtoto alipozaliwa jamaa aliendelea na majukumu yake. Labda mimi sijui maana ya 'kutelekezwa' lakini sidhani hali iliyomkuta jamaa unaweza kuiita 'utelekezaji'.
Na baada ya jamaa kuwa deported mdada hakuwa tayari kuondoka na kumfuata huko alikoenda. Ndio hapo uhusiano wao ulipovunjika. Kwa hiyo siyo kwamba jamaa alimwacha mdada. Ni 'circumstance' tu ndizo zilizosababisha wasiwe pamoja. Baada ya jamaa kuwa deported akaendelea na maisha yake na akaanza kutoka na watu wengine. Mdada wangu naye akaendelea na maisha yake na ndipo alipokutana na mimi sasa.
Na nisingeweza kwenda nae. niende nae ili iweje? Hapana bana. Nina ego na mimi. Na ndio maana nikaweka bayana kuwa akienda uhusiano wetu unakufa akibaki unaendelea. Akaamua kwenda nami sikusita, nikavunja uhusiano. Sasa wengi wenu mmepuuzia uamuzi niliochukua ambao mimi nadhani ulikuwa wa kijasiri, thabiti na sahihi. Mmeng'ang'ania kusema eti kwa nini nilimwachia aende....sasa sijui mimi ningemzuiaje mtu mzima aliyekwishaamua kufanya hivyo. Mapenzi sio utumwa na unyapara, at least kwangu mimi. Ukikiuka matakwa yangu unapigwa chini na maisha yanaendelea kama kawa na hicho ndicho kilichotokea. Kwangu mimi kwenye mahusiano hakuna kulazimishana.
Narudisha kauli Mkuu!
Kwa kuwa mwanzo wewe hukujieleza namna hii!
Hivyo binafsi ulinipotosha nilielewa kuwa umetumia zaidi Uanaume wako katika kuamua hili na si mapenzi!
Ila sasa napata picha kuwa toka mwanzo kuwa huyo dada ni opportunist; sijui uliliona hilo tangu mwanzo she stayed with you with hopes kuwa things will work out in her favour! In the end ameamua kuendeleza uhusiano wa zamani!
Hapo sikulaumu hata mimi would have done the same!