Nahisi Mungu ni mbinafsi

Nahisi Mungu ni mbinafsi

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
25,257
Reaction score
34,551
Nahisi Mungu ni mbinafsi kwa sababu zifuatazo

1)humpa amtakaye, Mungu kupitia vitabu vya dini amekuwa akisema mara kwa mara kwamba yeye humpa neema na humfanikishia mahitaji mja amtakaye, hapa moja kwa moja ana dhihirisha sifa ya ubinafsi kwa maana kama hakupendi hata umuombe namna gani hutofanikiwa abadani asilani.

2)humuongoa au humuepusha na maasi mtu amtakaye , hapa pia ana dhihirisha ubinafsi wake, kwa kuwa kama mja fulani anatenda dhambi Mungu atafanya juu chini kumuepusha hata kama huyo mtu hakuwa mtu wa ibada, lakini wakati huo huo wengine wakitenda maovu anawaacha wateketee na hawapi msaada wowote, hapa inaonesha kwa kiasi gani ana ubinafsi.

3)kuna mwengine hata afanye mema kiasi gani, malipo atakayopewa ni madogo sana, lakini mwingine akifanya mema kidogo ana shushiwa lundo la thawabu.

4)Ana waonea sana wanawake, hataki wawe viongozi, kwenye umiliki wa mali hasa Mirathi anataka wanaume tu ndio wapewe vipaumbele vya kumiliki.

5)kuna wengine tangu anazaliwa mpaka anafariki hajawahi kuonja raha yoyote ya dunia na wala hajui dunia ikoje, kwa sababu utakuta amezaliwa kipofu na maradhi tele mwilini na hajawahi kupata nafuu kuanzia ana zaliwa mpaka anafariki.
 
Weka vifungu vya vitabu hivyo... biblia na koran
 
Nimejaribu kuangalia sehemu yoyote ambayo walau ina ukweli kuhusu andiko lako sijaliona, nimefikia conclusion kuwa una uelewa mdogo sana kuhusu maandiko yanayomuelezea Mungu hasa biblia, jipe muda ujaribu kusoma utaona kile ulichoandika sio sahihi
 
Nachojua mimi, neno la Mungu linasema yeye hunyeeshea mvua na kupiga jua watu wote, waovu na wenye haki

"For He makes the sun to rise on the evil and on the good, and sends rain on the just and on the unjust!"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Neno mbinafsi sio sahihi kwa sababu ili yeyote awe mbinafsi sharti kuwe na wengine. sasa lama Mungu ni mmoja anambinafsia nani
 
40143_Come.jpg

Nahisi Mungu ni mbinafsi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom