Iko hivi, ukweli ni kwamba walio na Yesu wanatumaini. Hata wakipitia changamoto, Yesu Kristo hufanya huwasadia. Changamoto zipo kwa kila mtu, ila walio na Yesu, wanashinda zaidi ya kushindwa. Wakiugua hospital zikishindwa, bado wana msaada wa Mungu alio hai. Hiyo ndio tofauti.
Kingine, kila kitu chema chatoka kwa Mungu. Mungu ana penda watu wote ndio maana mvua na jua huwapatia wema na waovu. Kwa hiyo vyote walivyonavyo wema na waovu vyatoka kwa Mungu pekee.
Cha muhimu zaidi, walio na Yesu, wanatumaini hata baada ya kufa. Hii ni kwasababu wanae Yesu ambaye ni ufufuo na uzima. Hata wakifa, wataishi milele na Yesu mbinguni. Wasio na Yesu, hata wakiwa na mali nyingi kiasi gani, mwisho wa mtu bila Yesu, ni kilio na kusaga meno. Ni hukumu ya kutisha na moto was milele.