Nahisi Mungu ni mbinafsi kwa sababu zifuatazo
1)humpa amtakaye, Mungu kupitia vitabu vya dini amekuwa akisema mara kwa mara kwamba yeye humpa neema na humfanikishia mahitaji mja amtakaye, hapa moja kwa moja ana dhihirisha sifa ya ubinafsi kwa maana kama hakupendi hata umuombe namna gani hutofanikiwa abadani asilani.
2)humuongoa au humuepusha na maasi mtu amtakaye , hapa pia ana dhihirisha ubinafsi wake, kwa kuwa kama mja fulani anatenda dhambi Mungu atafanya juu chini kumuepusha hata kama huyo mtu hakuwa mtu wa ibada, lakini wakati huo huo wengine wakitenda maovu anawaacha wateketee na hawapi msaada wowote, hapa inaonesha kwa kiasi gani ana ubinafsi.
3)kuna mwengine hata afanye mema kiasi gani, malipo atakayopewa ni madogo sana, lakini mwingine akifanya mema kidogo ana shushiwa lundo la thawabu.
4)Ana waonea sana wanawake, hataki wawe viongozi, kwenye umiliki wa mali hasa Mirathi anataka wanaume tu ndio wapewe vipaumbele vya kumiliki.
5)kuna wengine tangu anazaliwa mpaka anafariki hajawahi kuonja raha yoyote ya dunia na wala hajui dunia ikoje, kwa sababu utakuta amezaliwa kipofu na maradhi tele mwilini na hajawahi kupata nafuu kuanzia ana zaliwa mpaka anafariki.