Nahisi mama mkwe anatikisa kiberiti

Nahisi mama mkwe anatikisa kiberiti

Mzee Baba hujakosea na unatenda vyema kabisa, Mama na familia ya mchumba inafahamu mapema uwezo wako wa maamuzi na kujiamini, mama kama ana tafakuri nzuri asingeweza hata kuongea na ww kuhusu suala la kumuoa mwanawe, ila angeshauri kupitia mwanawe awe anakushauri kufunga ndoa mapema iwezekanavyo kwa kuwa tayari umeshaonesha nia ya kumuhurumia mchumba wako kwa kumfungulia biashara. Mapenzi hujengwa na huruma kwa wenza, ila mama amekariri maisha ya kibepari yaani yanataka mtu awe majini na mjanja katika biashara, ila amesahau ubinaadamu na hali anayotakiwa kuwa nayo kwa mtarajiwa mkwewe kama mama mkwe.

HONGERA KWA MSIMAMO WAKO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona kuna shida mahal!

Mchumba wako inaonyesha ni mbinafsi kwa majibu aliyokupatia wakati ukienda kutoa kopi kazini kwako. Sikuona kama alikuomba msamaha na pia sikuona wewe kumtaka aone kosa lake na kisha kukuomba msamaha. Sikuona juhudi zako ulizozifanya mara baada ya kumkuta kahamia kwako, ulifurahia labda!

Mahari kwa desturi za makabila mengi ya Kitanzania ni muhimu, hivyo kwa majibu yako kwa Mama Mkwe hakika ulikosea. Ninauona mushkeri katika familia ya mchumba wako! Hakuna wazee wa kiume? Mama Mkwe ndio anadai mahari? Huna washenga ambao ungewaachia jambo hilo kuliko kendekeza malumbano na wakwe zako?
 
Kuna comment kasema hawezi toa mahari bado anampima means hajawa na uhakika kama ndie mke anayemtaka.
Kwanini aruhusu binti aendelee kukaa kwake? Kwanini asisimamie maamuzi yake amwambie aondoke hadi pale atakapokua tayari?
Dada na familia yake wana makosa makubwa tu. Binafsi sikai na mwanaume ambae naona hanihitaji, nakaa na mwanaume ambae ananitaka hasa na si kujipeleka kilazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo ndio wadada huwa wanaharibu, unapohamia kwa mwanaumekwa kulazimisha unajishushia heshima wewe mwenyewe, mtu kama ana nia ya kukuona wewe subiri atakuja mwenyewe nyumbani atakuchukua , wazazi watadai cha kwao, na utaondoka nyumbani kwa shamrashamra, huyu ina maana hata hakufanyiwa hafla yeyote sio, alienda mwenyewe kimyakimya, hamana hata tarumbeta ?!!, ndio maana jamaa anawazodoa, yeye na mama yake wamejishusha sana, au ni wale wa uswahilini ?.
 
Tatizo la vijana wa sasa. Kwani umeshapeleleza ukajua mahari ni bei gani mpaka uanze kikataa?
Mimi ningekufanya kitu mbaya sanaaaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungemfanya kitu mbaya kwa kushindwa kulipa mahali ?, unatamani umpige jamaa !!?, huyo jamaa alikuwa sahihi aliposema hayuko tayari, kwa sababu mahari zinajulikana haiwezi kuwa 50K,100K wala 300K, lakini pia utoaji wa mahari unaenda sambamba na kuanda sherehe ya ndoa, naamini hii inaweza ndio maana ya mtoa mada.
 
Hapo ndio wadada huwa wanaharibu, unapohamia kwa mwanaumekwa kulazimisha unajishushia heshima wewe mwenyewe, mtu kama ana nia ya kukuona wewe subiri atakuja mwenyewe nyumbani atakuchukua , wazazi watadai cha kwao, na utaondoka nyumbani kwa shamrashamra, huyu ina maana hata hakufanyiwa hafla yeyote sio, alienda mwenyewe kimyakimya, hamana hata tarumbeta ?!!, ndio maana jamaa anawazodoa, yeye na mama yake wamejishusha sana, au ni wale wa uswahilini ?.
Sijakataa dada kujikosea heshima. Ila huyo ndugu yako heshima yake iko wapi kukubali kuendelea kuishi na mwanamke aliyejikosea heshima? Mateso ya nini na inaonyesha kabisa bado hayupo tayari kuishi nae au hayupo tayari na ndoa.
Wangeendeleza mahusiano wakiwa mbalimbali lkn jamaa pia hana msimamo.
Unawezaje kuishi na mwanamke ambae haupo proud nae unaona kabisa kajileta.
Mi naona wanaendana.

Halafu umfungulie biashara ya 4M ushindwe kulipa mahari? Haimake sense. Jamaa ni kwamba hajawa tayari kujicommit.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee wewe akili hamna Yaani umewekeza milioni tano kasoro alafu upo tayari kuipoteza kwa ajili ya mahari ya milioni mbili hahahaha kweli wewe ni jiniasi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijakataa dada kujikosea heshima. Ila huyo ndugu yako heshima yake iko wapi kukubali kuendelea kuishi na mwanamke aliyejikosea heshima? Mateso ya nini na inaonyesha kabisa bado hayupo tayari kuishi nae au hayupo tayari na ndoa.
Wangeendeleza mahusiano wakiwa mbalimbali lkn jamaa pia hana msimamo.
Unawezaje kuishi na mwanamke ambae haupo proud nae unaona kabisa kajileta.
Mi naona wanaendana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Demii, Huwezi kuwafananisha hao wawili akili zao, Jamaa ameshasema alikuwa na nia ya kumsaidia, kwa hiyo alipoona amehamia kwake kwa nguvu akashidwa kumfukuza, utamfukuzaje sasa mchumba wako ?, na si yeye tu wadada wengi sana huhamia kwa wanaume zao kwa kuforce, yaani unaondoka kwenda kwenye pilika zako jioni unashangaa unamkuta kashajaa na mabegi yake ameanza na kupika, mimi mwenyewe ilitokea kwangu, miaka 25 iliyopita mke wangu ambaye ninaye mpaka sasa aliamua mwenyewe tu kuhamishia mizigo yake kwangu, name sikuwa na hiana, niliona ananisaidia kunipunguzia usumbufu wa kula hotelini na kujifulia, nikamuacha akakaa kwangu nikaendelea kufanya maandalizi ya kukamilisha taratibu
 
Basi mnawapenda wanawake wanaojileta. Hampaswi kulalamika ooh wanajikosea heshima. Hlf eti ndo mkeo sasa kajileta mwenyewe, what a shame!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mpaka leo watu wanashindwa kutofautisha kati ya MAHARI na MAHALI?
MAHALI: Sehemu
MAHARI: Fedha/samani inayotolewa kwa ajili ya ndoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Documents ambazo uliweza kwenda kuziprinti ofsini kwako, tuamini kuwa hazikuwa nyingi kivile.

Umeenda kwa ofisi ya huyo unaita mchumba, ofisi ambayo wewe unadai ulimfungulia ila amegoma kukuprintia [no money, no service].... kuna mke hapo..?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom