habari zenu jf...
kwanza kabisa mimi ni KE msishange hii ID...(ni jina lilonijia kwa haraka...mana aliekua mpenzi wangu ni Leo sign)
Am heart broken mwenzenu...mpenzi wangu KANIACHA
nimedumu naye kwa mwaka mmoja na nusu...
Jamani alinipenda sana na hajawahi kuonesha hata dalili za kucheat...mda wote simu yake nashika plus matendo yake kabisa yanaonesha he is honest...yani tangu siku ya kwanza kaniona akanitongoza yani mpaka mwisho wetu everything was too real yani...
Nilimpenda pia tena sana...nashangaa tu from nowhere ananiambia hatuwez kua pamoja tena...nkimuliza why anasema hataki kuoa kwa sasa...namwambia am okay with that hata usiponioa nataka tu niwe na wewe mana ndo furaha yangu...anasema hataki kunipotezea mda...akaniblock kote kote...kwa madai itanisaidia mm kumove on...
Dadangu alimpigia simu akamjibu kua hata ye inamuuma ila anataka kua single kwa sasa kuna vitu anataka atimize kwenye maisha yake so inamuhitaji awe single...nililia sana hadi hapa naandika nalia...naumia sana...
Hana kazi tumemaliza wote chuo...kuna mda alikua anasema kuna vitu natamani nikupe ila sina uwezo inaniuma...namwambiaga you know me better...nakuelewa na pesa sio kikwazo tutatafuta tutapata tu...hua nampa moyo hata matangazo ya kazi namtumia...plan za biashara pia hua tunaongelea...
Najiuliza maswali mengi sana kwa upendo mkubwa alonionesha amepataje nguvu ya kuniacha[emoji24][emoji24][emoji24]...na kuniumiza mimi...alisema me ndo furaha yake...sasa why aniache...he was so honest..loving...sio muhuni...hanywi..havuti...yani tuliendana sanaaa..yani kuna mda pia nilikua nasema this is too good to be true...
Guys niambieni how many heartbreaks does it take mpaka kupata the right one...huyu ni mwanaume wangu wa pili but nilimpenda sana kuliko wa kwanza we were just too perfect yani...kinachouma zaidi hatukugombana kusema kwamba ndo aniache...hata hakuna kosa nlilofanya...
Nawaomba msinikejeli please...niko katika wakati mgumu...nahitaji faraja zenu...