Nahamia Mwanza kusaka maisha ni mitaa ipi nitapata chumba cha elfu 30 ambapo pia huduma za kijamii zinapatikana kwa urahisi?

Nimeishi mwanza na Kahama miaka minne iliyopita.

Kwa Mwanza nenda Igoma au Nyakato sokoni, ukishindwa kabisa nenda Buswelu. Nauli ni 500 to town.

Kahama (ya Shinyanga)pia pako vizuri, japo muda mwingi nilikuwa pale kwa mabeberu lakini niliona mtaani mzunguko wa biashara ni mkubwa sana na mambo yanaenda. Just think about.
Nakazia hii, haya maeneo yako poa sana akaribie mitaa hii.
 
Wakuu,

Nimeamua kubadilisha mazingira ya utafutaji kutoka Dar kwenda Mwanza.

Mwanzoni mwa mwezi wa pili natarajia kusafiri, naomba msaada wa kufahamu ni mitaa ipi nitapata chumba cha elfu 30 na kuna huduma za maji, umeme na usafiri wa kwenda mjini ni nafuu na wa uhakika, na hakuna vibaka na wahuni wengi.

Nawasilisha
Bugarika,Igogo,Mabatini ni karibu na City center unaenda kwa mguu kufanya shughuli zako
 
Kapange kirumbaa ama ghana waweza pata vyumba kwa bei hiyo na ni sehemu ya karibu na mjini,,,,,,,,,,ukitaka nje ya mjini nenda buhongwaaa maisha ni marahisi kuna soko la vyakula linalolisha sehemu kubwa ya Mwanzaa utajifunza mengi,na vyumba vipo vya bei hio ,nauli to town tsh400

Kila la kheri
Kwelii asiachee kututafta madalalii buhongwa
 
Asante mkuu ila hilo la shughuli lisikupe tabu boss mimi nataka tu sehemu ya kukaa, yenye unafuu
Sasa shughuli ya kufanya isimpe tabu alafu unaulizia mzunguko upo vipi ?

Zanzibar kunaweka kuwa na mzunguko ila huenda unaenda kuuza bia au kitimoto karibia na misikiti....

Migodini kunaweza kukawa kuna uhitaji wa madada poa na kinywaji ila wewe unaenda kutangaza injiri.....

Kwa waganga wa kienyeji huenda kukawa na uhitaji wa miti shamba ila wewe unaenda kuuza panadol...
 
Soma vizuri uzi wangu mkuu sijauliza mzunguko uko vipi,
 
Wakuu,

Nimeamua kubadilisha mazingira ya utafutaji kutoka Dar kwenda Mwanza.

Mwanzoni mwa mwezi wa pili natarajia kusafiri, naomba msaada wa kufahamu ni mitaa ipi nitapata chumba cha elfu 30 na kuna huduma za maji, umeme na usafiri wa kwenda mjini ni nafuu na wa uhakika, na hakuna vibaka na wahuni wengi.

Nawasilisha
Njoo igoma boss chumba 30000 na huduma zote muhimu zipo karibu na wewe nitakupangisha mwenyewe
 
Back
Top Bottom