Nahamia Mwanza kusaka maisha ni mitaa ipi nitapata chumba cha elfu 30 ambapo pia huduma za kijamii zinapatikana kwa urahisi?

Kwanini unaondoka Dar mkuu?, kama ni biashara imekuwa ngumu Dar basi sikushauri kabisa kuchomoka hapo. Labda kama una sababu tofauti au biashara unayoenda fanya Mwanza ina link na Dar hapo sawa

Ila vinginevyo, komaa na Dar tu.
Chief!

Hela ipo kila sehemu, ni wewe Tu na jinsi utakavyojipanga
 
Nakushauri ukakae buhongwa pamecangamka sana na mishe mishe ni muda wote,pia ni karibu na soko la nafaka.Nauli to town 500.Kule unapata vyumba mpaka vya 15 vina umeme na maji muda wote.
Buhongwa maji yalikuwaga ni inshu ila sijui kwa sasa
 
Kwanini unaondoka Dar mkuu?, kama ni biashara imekuwa ngumu Dar basi sikushauri kabisa kuchomoka hapo. Labda kama una sababu tofauti au biashara unayoenda fanya Mwanza ina link na Dar hapo sawa

Ila vinginevyo, komaa na Dar tu.
Shida ya hili jiji biashara na wafanyabiashara Wamekuwa wengi mno. Kwa hiyo biashara sio kiviile sana maana naona Sana sna mtu hukosi hela ya kula
 
Kapange kirumbaa ama ghana waweza pata vyumba kwa bei hiyo na ni sehemu ya karibu na mjini,,,,,,,,,,ukitaka nje ya mjini nenda buhongwaaa maisha ni marahisi kuna soko la vyakula linalolisha sehemu kubwa ya Mwanzaa utajifunza mengi,na vyumba vipo vya bei hio ,nauli to town tsh400

Kila la kheri
Bugarika je vipi sio karibu na mjini
 
Katoro ilikuwa zamani sasa hivi mzunguko wa hela ni mdogo sana. Usikariri.
Pia nu bora uende katoro geita kumechangamka sana na kuna mzunguko mkubwa wa pesa pia ni karibu na kitovu cha utalii kanda ya ziwa chattle
 
Nakushauri ukakae buhongwa pamecangamka sana na mishe mishe ni muda wote,pia ni karibu na soko la nafaka.Nauli to town 500.Kule unapata vyumba mpaka vya 15 vina umeme na maji muda wote.
Buhongwa nauli mia 4 tu mkuu
 
Back
Top Bottom