Laki 4 Kwa mwezi, mitaa ipi naweza kumudu maisha Dar?

David Goliath

JF-Expert Member
May 16, 2018
928
1,799
Habari ndugu zangu, mimi ni kijana wa miaka 28 kwasasa nina mke na mtoto mmoja wa mwaka na miezi 6. Baada ya kuhitimu Shahada ya Kwanza ya Elimu katika chuo cha Tumaini Makumira mwaka 2019 niliamua kusalia hapa jijini Arusha kusaka maisha Kwa kujichanganya mtaani.

Nilianza na kuendesha bodaboda baadae nikahamia kwenye bajaji, kwasasa kuna kazi nimepata jijini Dar natakiwa kuripoti tar 7 mwezi huu maeneo ya kazini ni Posta, Je ni mitaa ipi vyumba ni Bei nafuu yaani chumba Cha elfu40 au 30 naweza pata na usafiri wa kufika Posta ni rahisi na huduma nyingine kama masoko ya vyakula yanapatikana, na vipi kwa huo mshahara nitaweza kutoboa na familia? Nafuatilia maoni yenu🙏🙏
 
Mbagala
Ndugu yangu analipia room elf 20, na ni pale mission tu...usafiri mda wote unapatikana. Mbagala panaonekana pana maisha rahisi sana sema me siwez kuishi kule asee.
Kwa nini??
 
Back
Top Bottom