Nafikiria kuzaa mtoto wa nje, mke wangu anaharibu watoto kwa kigezo cha "upendo"

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
9,144
Reaction score
19,689
Mimi na mke wangu tumebarikiwa kuwa na mtoto mmoja, ana miaka 6 mpaka sasa
Tatizo la huyu mtoto ni mtoto ambaye hana uvumilivu, akitaka kitu fulani ni lazima mama yake ampe la sivyo atakuwa analia mpaka akipate, akipewa chakula fulani asipokipenda itabidi mana yake ampikie kingine au mkamnunulie kingine ili kuepuka kelele, akitaka kuangalia channel fulani kwenye TV ni lazima awekewe

Nimeona ni malezi ya kipuuzi ambayo siwezi kuyaendekeza, kwa kuwa yatamharibu mtoto (dunia haiendi na haipo hivyo)

Ila kila nikijaribu kumkazia nakuta mama yake tayari amemfanyia alichokua ana demand nakuta mama yake amemfanyia hadi hii inaleta ugomvi.

Sasa nimewaza kwenda kuzaa mtoto wa nje, watoto wa nje.
Kuna dada mmoja aliniomba kuzaa nae ila nikawa nasita kuwa na mtoto wa nje, ila sasa naona ni wazo zuri kwa kuwa nikiwa nae pengine atakuwa na nidhamu zaidi ya huyu,

Watoto wa nje wanakuwa na nidhamu kidogo kwa kuwa mzazi wake mmoja anakuwa hana rasilimali nyingi sana za kuendekeza upumbavu
 
Enhee jamani tena,, ingawa ni kweli uyo mke kwa namna fulani anakosea,apo anamjengea mtoto kua katika dunia hakuna kukosa ni kupata tu,na sio vizuri kabisa sababu anakua huyo.

ila ayo maamuzi yako mmmh.......
 
Kinachoonekana hapo mke wako ni muajiriwa au mfanya Biashara hivyo anakipato halafu akabahatika kupata mtoto mmoja tu na kwa sababu ni huyo huyo, lazima amuangalie kama mboni ya jicho.
Kama mkeo anauwezo wa kuzaa, mngezaa wafike watatu hiyo hali ingeisha yenyewe na kama hana uwezo wa kuzaa, nivugumu sana kubadili hiyo hali kwani mwanamke mwenye kipato, anauweza wa kumnunulia mtoto wake chochote apendacho na hata huyo mtoto ameshajua kuwa, yupo mwenyewe hivyo anadeka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…